Mjapani alikuwa tishio sana sema lile Bomu la Nuclear liliwazima kabisa wakaona watulie
Yaani kile kizazi cha japan wale wahuni waliokuwa wanasumbua vita kuu ya pili ukisema uwarudishe leo washuhudie ndugu zao walivyotulia wanaweza kuwachapa makofi
Japan walikuwa na jeshi la ajabu yaani ukienda vitani lazima kujitoa muhanga adui afe, zile ndege za kamikaze zilikuwa marubani wanatarget sehem ya adui wanazigongesha kujitoa muhanga majamaa yalikuwa ni nuksi vibaya
Hapo Asia kulikuwa hakuna wa kumtandika japan kawachapa kama wote, inshort kama japan asingepigwa na mmarekani yale makombora leo hii huenda hapo Asia angekuwa na jeshi tishio yaani Huyo kiduku asingekuwa anathubutu kurusha makombora gake kwenye bahari ya Japan
Japan kilichomharibu ni kucheza na mmarekani yaani katika kosa kubwa ambalo alilifanya ni kwenda kuivamia ardhi ya marekani Direct kitu ambacho hakijawahi tokea alafu akauwa mamia ya wanajeshi na wananchi wa marekani watu kama 2500 walikufa pale
Hapo ndio mmarekani akamtandika na yale mabomu ya Nuclear alafu Japan akasurender, na baada ya kusurender mkataba ulimtaka kutolewa meno kwa jeshi lake lote na akakubali kuwa chini ya uangalizi wa marekani ndio maana hadi leo Jeshi la japan ni kama la wajerumani waliwekewa limit hakuna kuvuka sababu wanajulikana ni watata
Ila Wajapan wa leo na wajerumani waleo ni watu wastaharabu kupindukia yaani ukienda kuishi japan ni moja ya nchi zenye watu waaminifu na wastaharabu sana utasema ni vizazi viwili tofauti na wale ndugu zao