Kwanini Ukristo na Uislam unashamiri kwenye nchi masikini na duni kielimu?

Kwanini Ukristo na Uislam unashamiri kwenye nchi masikini na duni kielimu?

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
6,811
Reaction score
6,503
Tafiti na vipimo mbali mbali vya mahusiano kati ya maendeleo katika jamii na imani za kidini vimebainisha migawanyiko na mahusiano ya imani za kidini kati ya nchi moja na nyingine na mendeleo kwa kiwango kikubwa.

Kikubwa zaidi kilichonigusa ni mahusiano ya dini za imani ya Kikristo na Kiislamu mara nyingi kushamili katika nchi ambazo ni maskini na zenye elimu duni huku dini zingine zikishamili mara nyingi katika sehemu yenye utajiri na elimu ya kiwango cha juu.

Kupungua kwa kiwango cha juu cha imani ya dini yoyote katika nchi zilizoendelea na mfano halisi ni hapa Europe ambapo makanisa kwa sasa yanadoda na yanageuzwa kuwa ni sehemu ya kutalii (museum) na mengine yanageuzwa kuwa migahawa (cafe). imefikia hatua hapa wachungaji wake wengi wanakuwa imported kutoka nchi masikini kwa sababu wazawa wameacha kujiunga na vyuo vya kitawa.

Kuongezeka kwa wakimbizi wengi wa kisiasa kutoka nchi maskini na zenye elimu duni za mashariki ya mbali na pia zile ambazo zilikuwa na machafuko zimeongeza idadi ya waumini wa kiislamu hapa Ulaya lakini hawa pia kwa ujumla ni masikini na elimu yao ni ndogo.

Tanzania ikiwa ni nchi mojawapo masikini duniani kwa sasa Makanisa na Misikiti inashamili kila sehemu wakati kipato na elimu vikiwa vimedumaa kwa masikini au kuongezeka kwa kasi ndogo.

1) Maswali yanayojitokeza ni kutaka kufahamu, kwa nini Ukristo na Uslamu unashamili katika nchi hizi masikini na duni kielimu na pia ukipungua kwa kasi katika nchi tajiri na zenye elimu ya kiwango cha juu.

2) Nini kilicho nyuma ya hizi imani za dini ya Kikristo na Kiislamu katika nchi masikini na zenye elimu duni?.

TOP 17 GLOBAL INDEX OF RELIGIOSITY AND ATHEISM YEAR 2012
[TABLE="class: grid, width: 500"]
[TR]
[TD]COUNTRY[/TD]
[TD]TOTAL % OF
POPULATION[/TD]
[TD]GDP PER
CAPITA 2011 [$][/TD]
[TD]INDEX
NUMBER[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]GHANA[/TD]
[TD]96[/TD]
[TD]1580[/TD]
[TD]1[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]NIGERIA[/TD]
[TD]93[/TD]
[TD]1522[/TD]
[TD]2[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]ARMENIA[/TD]
[TD]92[/TD]
[TD]3076[/TD]
[TD]3[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]FIJI[/TD]
[TD]92[/TD]
[TD]4224[/TD]
[TD]3[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]MACEDONIA[/TD]
[TD]90[/TD]
[TD]5162[/TD]
[TD]5[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]ROMANIA[/TD]
[TD]89[/TD]
[TD]8875[/TD]
[TD]6[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]IRAQ[/TD]
[TD]88[/TD]
[TD]3478[/TD]
[TD]7[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]KENYA[/TD]
[TD]88[/TD]
[TD]833[/TD]
[TD]7[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]PERU[/TD]
[TD]86[/TD]
[TD]5904[/TD]
[TD]8[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]BRAZIL[/TD]
[TD]85[/TD]
[TD]12789[/TD]
[TD]9[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]GEORGIA[/TD]
[TD]84[/TD]
[TD]3210[/TD]
[TD]10[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]PAKISTAN[/TD]
[TD]84[/TD]
[TD]1199[/TD]
[TD]10[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]AFGHANISTAN[/TD]
[TD]83[/TD]
[TD]589[/TD]
[TD]11[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]MALDOVA[/TD]
[TD]83[/TD]
[TD]1969[/TD]
[TD]11[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]COLOMBIA[/TD]
[TD]83[/TD]
[TD]7114[/TD]
[TD]11[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]CAMEROON[/TD]
[TD]82[/TD]
[TD]1225[/TD]
[TD]12[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]MALAYSIA[/TD]
[TD]81[/TD]
[TD]10085[/TD]
[TD]13[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
WIN-Gallup International ‘Religiosity and Atheism Index' which measures global self-perceptions on beliefs is based on interviews with more than 50,000 men and women selected from 57 countries across the globe in five continents. The survey also provides trend data for shifts in attitudes since 2005.

A world-wide poll conducted by WIN-Gallup International, a network of the world's top most independent pollsters, asked exactly the same question in 57 countries across the globe:

The highest GDP per Capita in the world is $115,809
The Lowest GDP per Capita in the world is 112

NOTE:
Sikuweza kupata data za Tanzania kulinganisha na nchi zingine duniani lakini kwa kuangalia kwa mbali zinaweza kuwa karibu na data za Nchi ya Kenya.

cc Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, Mchambuzi, FairPlayer, Mkandara, Mohamed Said, THE BIG SHOW, Jasusi, Mag3, Nyambala, Boko haram
 
Last edited by a moderator:
Hili mkuu Kiranga kila mara hulizungumzia i.e umaskini na iman ya dini vinafungamana sana....kuna kipindi hata signature yake ilikuwa na ujumbe huo....kuna ukweli mkubwa sana lakn.
 
Dini zipo associated sana na moral development. Katika nchi zilizoendelea, watu wana maadili hata kama hawapractice dini. Rushwa, uzinzi, dhulma, uongo, wizi na mengine yanaitwa maovu katika jamii zilizoendelea lakini yanaitwa dhambi katika nchi zisizoendelea. Pengine hii inahusishwa pia na degree ya ustaarabu, ambapo mara nyingi ni kubwa katika jamii zilizo na elimu kuliko jamii ambazo hazijaelimika
 
Well said....
 
Kwa hiyo Tuko unamaanisha neno ustaarabu ni pamoja na maadili ambayo jamii iliyooendelea ndiyo nguvu kuu katika maisha yao wakati less developed countries zinakuwa na tatizo la ustaarabu katika maisha yao.
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo Tuko unamaanisha neno ustaarabu ni pamoja na maadili ambayo jamii iliyooendelea ndiyo nguvu kuu katika maisha yao wakati less developed countries zinakuwa na tatizo la ustaarabu katika maisha yao.

Kwa kweli inawezekana. Japokuwa sijui maana halisi ya ustaarabu, lakini naweza kusema ni hali ya mtu kuhakikisha anafuata taratibu zinazokubaliwa na jamii yake, na kutokufanya mambo yanayohusu wengine. Juzi wakati wa pasaka nilikuwa nawauliza marafiki zangu kama wataenda kanisani, majority walisema huwa hawapractice dini, na wawili wakaenda mbali zaidi na kusema wanadhani dini zinaleta migogoro zaidi kuliko amani katika jamii.
Hawa wenzangu japo hawapractice dini, huoni wakimisbihave, huoni wakitukana au kugombana, sio wadokozi, n.k... kwa kifupi ni gentlemen...
 
Yes, hata mimi ninafikiri hiyo ndiyo maana ya ustaarabu kwa kiingereza ninaweza nikasema kuishi ndani ya mipaka ya natural justice.
 
Dini pia inatumika kama namna fulani ya kupunguza pressure za umasikini. Inatoa faraja na matumaini hata kama sio tangible, inaweka hofu fulani kwa wale wanaotaka kutenda maovu.

Kwa namna fulani zimesaidia kwa baadhi ya maeneo kupunguza vitendo vya kishenzi kama kufanya mauaji kwa Imani za kishirikina. Ukijaribu kupitia historia za makabila utaona kulikuwa na ukiukwaji mkubwa sana wa haki za Binaadamu hasa mauaji, Wanawake walinyanyaswa sana lakini ujio wa Dini angalau umepunguza hayo, na sababu moja kubwa.........Hofu ya Mungu.

Sikatai kwamba hata walio miongoni mwa Waumini kuna wenye tabia kama hizo lakini angalau wanajua si jambo linalokubalika kwa Mkuu wao kuliko wote - Mungu.

La nyongeza Dini imeziba ombwe la Uongozi hasa kwenye Umasikini. Tunajua kwa nchi masikini kama zetu mlipuko wa Kijamii kutokana na kukosa matumaini unaweza kutokea, lakini kwa mtazamo wangu Dini zimepunguza makali........Kuna matumaini fulani wameyajenga kwenye nyoyo za Watu.
 
Ukifuatilia historia za dini zinaacha maswali mengi sana kuliko majibu, wenye elimu walisha gundua ujanja ujanja ukiopo kwenye dini,maskini hana uwezo wa kupata elimu ya kujitambua kirahisi na anaishi kwa imani ,so lolote atakaloambiwa lenye matumaini atalifuata . Kwa bahati mbaya umaskini na kukosa elimu ni vitu vinavyo ambatana sana .
 
Ng'wamapalala

Ni heri ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuurithi ufalme wa Mungu! Katika hali hii ya umaskini na elimu duni tutaendelea kumwabudu Mungu aliye hai kwani Mungu huangalia moyo uliopondeka na kumtii yeye peke yake.
 
Last edited by a moderator:
Dini pia inatumika kama namna fulani ya kupunguza pressure za umasikini. Inatoa faraja na matumaini hata kama sio
tangible, inaweka hofu fulani kwa wale wanaotaka kutenda maovu.

Kwa namna fulani zimesaidia kwa baadhi ya maeneo kupunguza vitendo vya kishenzi kama kufanya mauaji kwa
Imani za kishirikina. Ukijaribu kupitia historia za makabila utaona kulikuwa na ukiukwaji mkubwa sana wa haki
za Binaadamu hasa mauaji, Wanawake walinyanyaswa sana lakini ujio wa Dini angalau umepunguza hayo, na sababu moja kubwa.........Hofu ya Mungu.

Sikatai kwamba hata walio miongoni mwa Waumini kuna wenye tabia kama hizo lakini angalau wanajua si jambo
linalokubalika kwa Mkuu wao kuliko wote - Mungu.

La nyongeza Dini imeziba ombwe la Uongozi hasa kwenye Umasikini. Tunajua kwa nchi masikini kama zetu
mlipuko wa Kijamii kutokana na kukosa matumaini unaweza kutokea, lakini kwa mtazamo wangu Dini
zimepunguza makali........Kuna matumaini fulani wameyajenga kwenye nyoyo za Watu.
Ninakubaliana na maelezo yako lakini bado pia hukutoa kilicho nyuma ya sababu ya dini za Kikristo na Kiislamu peke yake kushamili katika maeneo ya watu masikini na wasio na elimu ya juu ukilinganisha na imani za dini zingine?
 
Mkuu kwa kiasi kikubwa dini inaendana na Saikoloji ya watu. Mara ningi binadamu akiwa na shida ndipo uhamua kumlilia Mungu. Watu masikini wanapenda kuwa karibu na Mungu ili kujipa Moyo . Mfano Makanisa ya Kilokole wao wanaubiri kuwa ukiomba utajiri Mungu anakupa, ndiyo maana utaona siku hizi Watu wanahama kanisa la Roma na kwenda kwa walokole ili wapate utajiri au hali yao ya kiuchumi iwe sawa.

Cha ajabu ni kwamba binadamu yuleyule alikuwa mcha mungu siku akipata pesa utaona hata kanisa analisahau. Ndiyo Maana hata kwenye bible inaonesha tajiri itakuwa ngumu kuuona ufalme wa mbinguni, kwa hiyo mara nyingi binadamu ujiweka karibu na mungu pale wanapokuwa na shida.

Kwa maelezo hayo ndiyo maana nchi masikini zinakuwa na dini sana kwani kisaikolojia binadamu uwa karibu na dini pale anapokuwa na shida. Hivyo nchi za ulaya kwa kuwa hawana shida sana wao wamehamua kuhasi, hawaoni nini Mungu atawasaidia, lakini ole wao.

Ulaya wanaamini sana sana katika juhudi na technolojia kuliko miujiza
 
Kwa kweli inawezekana. Japokuwa sijui maana halisi ya ustaarabu, lakini naweza kusema ni hali ya mtu kuhakikisha anafuata taratibu zinazokubaliwa na jamii yake, na kutokufanya mambo yanayohusu wengine. Juzi wakati wa pasaka nilikuwa nawauliza marafiki zangu kama wataenda kanisani, majority walisema huwa hawapractice dini, na wawili wakaenda mbali zaidi na kusema wanadhani dini zinaleta migogoro zaidi kuliko amani katika jamii.
Hawa wenzangu japo hawapractice dini, huoni wakimisbihave, huoni wakitukana au kugombana, sio wadokozi, n.k... kwa kifupi ni gentlemen...

Ukumbuke nchi zilizoendelea zilianza kupractice dini miaka mingi iliyopita, huduma za maendeleo ya jamii ni matunda ya usamaria mwema ulionzishwa na mashirika ya dini na baadae serikali iliingilia kuhakikisha kila mtu anapata mahitaji makuu muhimu ya ubinadamu. Nchi masikini hazijaweza kufikia kiwango hicho, mashirika ya dini yanasaidia waumini wao kwa kiasi wawezacho.
 
Nchi zilizoendelea wanaamini sana katika juhudi na technolojia kuliko miujiza, masikini wanaamini katika miujiza. Tajiri ni vigumu kwenda mbinguni (Jesus said)
 
Hao wanaofanya utafiti hawaji kuwa Yesu alishamaliza mchezo hapo?, alisema ni rahisi Ngamia kuingia kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuuona Ufalme wa mbinguni.
 
Ninavyofahamu na kuona S/Korea, China na nchi nyingi za Far East, Ukristu unakua na hii ni kwasababu religion ni natural kwa mwanadamu. Communism ilikufa kwa vile ilikuwa na vacuum.

Hizo nchi hapo juu si masikikini kihivyo,.ukristo wa korea na uchina,hongkong,macau etc upo kwa matajiri,hata west watu wanaorudi ktk ukristu wapo.

North Korea na China wanaangalia ukristu kama tishio kwa tawala za kijamaa kuliko chombo cha mafanikio. Ingawa raia wake wana-fight kuufuata wakiamimini ndio ustaarabu wa mafanikio.

Ukristu korea si majority religion ila impact yake dunia inaona na hata wamisionary wao ni wengi sana dunian.

Tuwe waangalifu, East panakuwa huku wakipokea ukristu, west panaanguka jinsi wanaukataa ukristu. Jamii isiyo na hope ni kama mfu. Yesu ni hope.

Atheism haimpi mtu sababu ya kujenga kitu cha kudumu. Islam inakimbiza watu wafe kuwahi pepo zaidi kuwekeza ktk elimu dunia .
Tuwe waangalifu na tafiti za propaganda km za redet. Hata mashoga wana tafiti zao kuonyesha kuwa hata penguin mashoga wapo,nyani mashoga wapo na wanyama wengine halafu wakahitimisha kuwa ni natural. Lakini nani kawauliza waliwapataje hao wanyama wachache mashoga? Kama si wao waliwaprogram ili potosha dunia.

cc Kiranga
 
Last edited by a moderator:
Imeandikwa...siku za mwisho yatatoka matukio ya kushangaza...
Bado yatakuja mengi..
imeandikwa watu watazikataa imani zao... wakristo wameambiwa waendelee kuamini Injili mpaka mwisho..
 
Dini pia inatumika kama namna fulani ya kupunguza pressure za umasikini. Inatoa faraja na matumaini hata kama sio tangible, inaweka hofu fulani kwa wale wanaotaka kutenda maovu.

...

Mkuu umeeleza mengi mazuri ila nitofautiane ne wewe hapo kwenye red. Sio kila dini inafanya hivyo angalau kwa kuangalia matendo ya tangu waasisi wa dini hizo, viongozi wa dini hizo tulio nao leo, na hata waumini wao. Baadhi ya dini hizi zinahubiri violence na mifano iko hai wala sina haja ya kuitaja hapa.
 
Ng'wamapalala

Data za upande mmoja haziwezi kujenga mahusiano na upande mwingine wa kufikirika. Jedwali lako hapo juu linaonyesha data za imani ya dini lakini sio data za uchumi au elimu.

Je takwimu zinasemaje kuhusu imani ya dini katika nchi kama Marekani? Vipi kuhusu nafasi ya dini kwenye nchi tajiri zaidi duniani za G8?

Vipi kuhusu Uislamu katika mataifa tajiri ya Kiarabu?

Ghana inayoonekana kuongoza kwa Ukristo Afrika inajimudu mno kielimu ukilinganisha na nchi masikini kama Tanzania. Kwanini basi Tanzania isiwe nafasi ya juu zaidi ya Ghana au Nigeria (na haya ni mataifa yenye wasomi wengi zaidi katika nchi za Magaharibi)

Kwa ushauri tu, ili kuweza kuhitimisha kuwa mahusiano kati ya dini na elimu ni vema kupata takwimu za kiuchumi/elimu na hali ya uchumi katika nchi husika.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom