Uwekezaji katika Bond au Hati fungani ni aina ya uwekezaji ambao imekuwepo kwa muda mrefu sana katika nchi mbalimbali,
Hata hivyo hapa nchini kwetu dhana hii ya uwekezaji bado inaonekana kwa ni ngeni miongoni mwa watu wengi
Bondi au Hati fungani ni nini?
Ni uwekezaji ambapo mwekezaji anaikopesha serikali au kampuni, na serikali hiyo au kampuni inaahidi kumlipa mwekezaji huyo baada ya hatifungani hiyo kukomaa,
Kwa kawaida faida inayoambatana na uwekezaji katika bond hugawiwa kila baada ya miezi 6.
Benki ya NMB ambayo ndiyo the most profitable bank, na ndiyo benki iliyo sambaa zaidi nchini Tanzania kwa sasa imetangaza uuzaji wa hatifungani yake, ambapo imeanza kuuzwa kutoka tarehe 10 May na itauzwa hadi tarehe 8 June 2016, kupitia madalali 10 wa soko la Hisa la Dar es salaam Mfano
Arch Financials & Investments Advisory Limited wanaopatikana katika jengo la NIC life house lililopo mtaa wa sokoine posta jijini Dar es salaam, (Tel:+25522732922396,Mob: 0784952814) au Kupitia Tawi lolote la NMB lililo karibu nawe
Kwa Kiasi kidogo tu cha uwekezaji cha shillingi laki tano (500,000) unapata faida ya asilimia 13% kwa mwaka kwa muda wa miaka mitatu ambapo faida hii inakuwa inalipwa mara mbili kwa mwaka, bila kusahau kuwa bondi itakapo komaa "mature" NMB itakulipa pesa yako yote uliyokuwa umewekeza awali
Hati fungani hii ya NMB walengwa wakuu ni wawekezaji wadogo na wakati, japo hata wakubwa hawajazuiwa na ndiyo maana kiwango cha chini cha uwekezaji ni Tsh 500,000/= Tu na kuendelea, tofauti na Bondi nyingine za makampuni zilizo wahi tokea hapa Tanzania
Chukulia kama umewekeza Shillingi 1,000,000 kwa riba ya 13% kwa mwaka, hivi ndivo itakavyokuwa
1.Interest=Principal*Rate* Time
=1,000,000*13/100*1year
=Shillingi 130,000
2.Lakini interest hii inalipwa mara mbili kwa mwaka hivyo malipo ya mkupuo wa kwanza yatakuwa ni TZS130,000/2 =TZS 65,000/=
3.Kila mkupuo wa malipo unatozwa kodi ya zuio ya 10%
=65,000-(65000*10%)
=65,000-6,500
=TZS 58,500
Hivyo kufikia Disemba 2016(baada ya miezi 6) utapokea Shillingi 58,500
4.Baada ya miaka 3, uwekezaji wako katika hatifungani hii utakuwa umekuingizia Shillingi 351,000 (58,500*6) kutoka katika uwekezaji wako wa Shillingi 1000,000. Shullingi 1M yako itakwa imekuwa hadi kufikia shillingi
1,351,000 pasipo wewe kufanya chochote, umeingiza pesa hizi ukiwa umekaa tu nyumbani au upo kwenye shughuli zako nyingine.
Isitoshe endapo utapata dharura, kabla miaka mitatu haija isha,na ukahitaji hizi pesa zako bado una nafasi ya kupata pesa zako ulizo wekeza , ambapo utaweza ku uza hatifungani hii katika soko la Hisa la Dar es salaam, kupitia madalali wake
Source :
TzInsight