evansGREATDeal
JF-Expert Member
- Jan 4, 2016
- 4,013
- 2,333
mkuu come and see,,,.
eden kimario
eden kimario
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ujinga huu,.alafu eti wanasema inanuifaisha watzAisee hii ngumu kumeza....kwahyo kila mwez faida elfu 10!![emoji15] [emoji15]
Imekaa poa sana, somo limeeleweka sanaa...Uwekezaji katika Bond au Hati fungani ni aina ya uwekezaji ambao imekuwepo kwa muda mrefu sana katika nchi mbalimbali,
Hata hivyo hapa nchini kwetu dhana hii ya uwekezaji bado inaonekana kwa ni ngeni miongoni mwa watu wengi
Bondi au Hati fungani ni nini?
Ni uwekezaji ambapo mwekezaji anaikopesha serikali au kampuni, na serikali hiyo au kampuni inaahidi kumlipa mwekezaji huyo baada ya hatifungani hiyo kukomaa,
Kwa kawaida faida inayoambatana na uwekezaji katika bond hugawiwa kila baada ya miezi 6.
Benki ya NMB ambayo ndiyo the most profitable bank, na ndiyo benki iliyo sambaa zaidi nchini Tanzania kwa sasa imetangaza uuzaji wa hatifungani yake, ambapo imeanza kuuzwa kutoka tarehe 10 May na itauzwa hadi tarehe 8 June 2016, kupitia madalali 10 wa soko la Hisa la Dar es salaam Mfano Arch Financials & Investments Advisory Limited wanaopatikana katika jengo la NIC life house lililopo mtaa wa sokoine posta jijini Dar es salaam, (Tel:+25522732922396,Mob: 0784952814) au Kupitia Tawi lolote la NMB lililo karibu nawe
Kwa Kiasi kidogo tu cha uwekezaji cha shillingi laki tano (500,000) unapata faida ya asilimia 13% kwa mwaka kwa muda wa miaka mitatu ambapo faida hii inakuwa inalipwa mara mbili kwa mwaka, bila kusahau kuwa bondi itakapo komaa "mature" NMB itakulipa pesa yako yote uliyokuwa umewekeza awali
Hati fungani hii ya NMB walengwa wakuu ni wawekezaji wadogo na wakati, japo hata wakubwa hawajazuiwa na ndiyo maana kiwango cha chini cha uwekezaji ni Tsh 500,000/= Tu na kuendelea, tofauti na Bondi nyingine za makampuni zilizo wahi tokea hapa Tanzania
Chukulia kama umewekeza Shillingi 1,000,000 kwa riba ya 13% kwa mwaka, hivi ndivo itakavyokuwa
1.Interest=Principal*Rate* Time
=1,000,000*13/100*1year
=Shillingi 130,000
2.Lakini interest hii inalipwa mara mbili kwa mwaka hivyo malipo ya mkupuo wa kwanza yatakuwa ni TZS130,000/2 =TZS 65,000/=
3.Kila mkupuo wa malipo unatozwa kodi ya zuio ya 10%
=65,000-(65000*10%)
=65,000-6,500
=TZS 58,500
Hivyo kufikia Disemba 2016(baada ya miezi 6) utapokea Shillingi 58,500
4.Baada ya miaka 3, uwekezaji wako katika hatifungani hii utakuwa umekuingizia Shillingi 351,000 (58,500*6) kutoka katika uwekezaji wako wa Shillingi 1000,000. Shullingi 1M yako itakwa imekuwa hadi kufikia shillingi 1,351,000 pasipo wewe kufanya chochote, umeingiza pesa hizi ukiwa umekaa tu nyumbani au upo kwenye shughuli zako nyingine.
Isitoshe endapo utapata dharura, kabla miaka mitatu haija isha,na ukahitaji hizi pesa zako bado una nafasi ya kupata pesa zako ulizo wekeza , ambapo utaweza ku uza hatifungani hii katika soko la Hisa la Dar es salaam, kupitia madalali wake
Source : TzInsight
Miaka mitatu unatengeneza laki Tatu. si bora hiyo hela nile minenepe. Hii business ni nzuri kwa watu wenye hela nyingi ukiweka milioni 50 faida yake unaiona sasa uweke mil 1 kwenye miaka mitatu upate laki tatu c utani huo? hata muuza vitumbua anatengeneza zaidi ya laki tatu kwa mwaka na mtaji wake wa elf hamsini.
wamenikiosa.....niliikomalia sana hii deal nilijua inalipaEti 1M kwa miaka mitatu faida laki 3!!!?? Hyo faida muuza supu na chapati anaingiza kwa muda mfupi sio huo wa kwenu
Anyway.....mfumo wa uchumi ulivyo ni kwamba taasisi za kifedha kama benki huwa hazina urafiki na maskini (mwenye kipato kidogo) badala yake ni kumkamua alicho nacho kwa kutumia "lugha tamu inayovutia"
Mmh bopwe sijakupata vrmaKwa ndugu zangu wa mikoa mingine isio kuwa kipenzi wa banki hii na Nbc misishiriki kabisa kununua. Hata kuweka pesa hii benki ni wabaguzi kweli kwenye ajira tena ubaguzi ulokithiri. Hapa zaidi ni ni mkoa mmoja tu wa kaskazini. Wengini wa kuhesabu au wapo kwa address ya wakubwa.
Bank hizi ni nadra kuajiri waislam ...sana utawakuta wawili watatu watoto wa wakubwa au kitengo cha bank ya kiislam.
Hizi bank zilikua mali ya umma..hivyo kutoa ajira kwa misingi ya dini na kabila fulani haikubaliki....na tatasema ili waislam na wamakonde nao wapate kazi ...wacheni ubaguzi...
Mmh sidhani kama hili liko kwa mtazamo huoNaona Sera ya magufuli kuondoka hela za serikali kwenye mabenki imeanza saidia, sasa mabenki hayana hela za kukopesha lazima yakope kwa watu ili wakopeshe wengine!
Safi sana JPM,
Imesaidia nini sasa? Kama ni kweli hawana hela ya kukopesha si ndo wananchi watazidi kuumia au?Naona Sera ya magufuli kuondoka hela za serikali kwenye mabenki imeanza saidia, sasa mabenki hayana hela za kukopesha lazima yakope kwa watu ili wakopeshe wengine!
Safi sana JPM,
Hii inafaa wanaoweka pesa bank hawana cha kuzifanyia lakini si sisi waganga mjaaa...faida ni ndogo sana nikilinganisha nifanya biashara ya uchuuzi nitapata kubwa kuliko hiyo..
Mi nitaweka 500,000 kwanza
Afu baada ya hapo tutaona itakuwaje
Mkuu bond ina tofauti na hisa
usiweke tu kutazama itakuaje
weka na uliza kabisa bond ikiiva utalipwa ngapi
na utalipwa tu....hakuna kupanda wala kushuka kwa thamani
weka hata milioni 500 kama una uwezo
kabla ya kuweka wanakupigia hesabu utalipwa ngapi ikiiva....unajua kabisa
Hivi walisema ukiweka unapata faida ya asilimia ngapi vile?