Kwanini unapaswa kununua bond au Hati fungani ya NMB?

Kwanini unapaswa kununua bond au Hati fungani ya NMB?

Eti 1M kwa miaka mitatu faida laki 3!!!?? Hyo faida muuza supu na chapati anaingiza kwa muda mfupi sio huo wa kwenu

Anyway.....mfumo wa uchumi ulivyo ni kwamba taasisi za kifedha kama benki huwa hazina urafiki na maskini (mwenye kipato kidogo) badala yake ni kumkamua alicho nacho kwa kutumia "lugha tamu inayovutia"
 
Uwekezaji katika Bond au Hati fungani ni aina ya uwekezaji ambao imekuwepo kwa muda mrefu sana katika nchi mbalimbali,

Hata hivyo hapa nchini kwetu dhana hii ya uwekezaji bado inaonekana kwa ni ngeni miongoni mwa watu wengi

Bondi au Hati fungani ni nini?

Ni uwekezaji ambapo mwekezaji anaikopesha serikali au kampuni, na serikali hiyo au kampuni inaahidi kumlipa mwekezaji huyo baada ya hatifungani hiyo kukomaa,

Kwa kawaida faida inayoambatana na uwekezaji katika bond hugawiwa kila baada ya miezi 6.

Benki ya NMB ambayo ndiyo the most profitable bank, na ndiyo benki iliyo sambaa zaidi nchini Tanzania kwa sasa imetangaza uuzaji wa hatifungani yake, ambapo imeanza kuuzwa kutoka tarehe 10 May na itauzwa hadi tarehe 8 June 2016, kupitia madalali 10 wa soko la Hisa la Dar es salaam Mfano Arch Financials & Investments Advisory Limited wanaopatikana katika jengo la NIC life house lililopo mtaa wa sokoine posta jijini Dar es salaam, (Tel:+25522732922396,Mob: 0784952814) au Kupitia Tawi lolote la NMB lililo karibu nawe

Kwa Kiasi kidogo tu cha uwekezaji cha shillingi laki tano (500,000) unapata faida ya asilimia 13% kwa mwaka kwa muda wa miaka mitatu ambapo faida hii inakuwa inalipwa mara mbili kwa mwaka, bila kusahau kuwa bondi itakapo komaa "mature" NMB itakulipa pesa yako yote uliyokuwa umewekeza awali

Hati fungani hii ya NMB walengwa wakuu ni wawekezaji wadogo na wakati, japo hata wakubwa hawajazuiwa na ndiyo maana kiwango cha chini cha uwekezaji ni Tsh 500,000/= Tu na kuendelea, tofauti na Bondi nyingine za makampuni zilizo wahi tokea hapa Tanzania

Chukulia kama umewekeza Shillingi 1,000,000 kwa riba ya 13% kwa mwaka, hivi ndivo itakavyokuwa

1.Interest=Principal*Rate* Time

=1,000,000*13/100*1year

=Shillingi 130,000

2.Lakini interest hii inalipwa mara mbili kwa mwaka hivyo malipo ya mkupuo wa kwanza yatakuwa ni TZS130,000/2 =TZS 65,000/=

3.Kila mkupuo wa malipo unatozwa kodi ya zuio ya 10%

=65,000-(65000*10%)

=65,000-6,500

=TZS 58,500

Hivyo kufikia Disemba 2016(baada ya miezi 6) utapokea Shillingi 58,500

4.Baada ya miaka 3, uwekezaji wako katika hatifungani hii utakuwa umekuingizia Shillingi 351,000 (58,500*6) kutoka katika uwekezaji wako wa Shillingi 1000,000. Shullingi 1M yako itakwa imekuwa hadi kufikia shillingi 1,351,000 pasipo wewe kufanya chochote, umeingiza pesa hizi ukiwa umekaa tu nyumbani au upo kwenye shughuli zako nyingine.

Isitoshe endapo utapata dharura, kabla miaka mitatu haija isha,na ukahitaji hizi pesa zako bado una nafasi ya kupata pesa zako ulizo wekeza , ambapo utaweza ku uza hatifungani hii katika soko la Hisa la Dar es salaam, kupitia madalali wake

Source : TzInsight
Imekaa poa sana, somo limeeleweka sanaa...
Ila tukija kwenye "time value of money" iyo Milion niliyoweka leo siku napewa itakua na dhamani sawa na Milion niliyo invest? maana hapo tayari nishakula "viinterest" vyangu.

pls Mkuu some help hapo
 
Miaka mitatu unatengeneza laki Tatu. si bora hiyo hela nile minenepe. Hii business ni nzuri kwa watu wenye hela nyingi ukiweka milioni 50 faida yake unaiona sasa uweke mil 1 kwenye miaka mitatu upate laki tatu c utani huo? hata muuza vitumbua anatengeneza zaidi ya laki tatu kwa mwaka na mtaji wake wa elf hamsini.

Mawazo kama hayo hapo juu ndio yanafanya maskini kuwa maskini na tajiri kuwa tajiri. Ni fikra. Kutotambua fursa ndio shida, inayofanya wengine wawe maskini na wengine matajiri.

Mtu anapewa fursa, lakini anachoweza kufanya ni kujiondoa na kufikiri hela inaongezeka kwa kuwa na hela nyingi. Wakati kila fursa ni nafasi ya kupata hela.

Yaani hata ukijenga nyumba, hutapata mrejesho wa faida kama kwenye hati fungani.

Watanzania wenye macho , hii ni fursa.
 
Eti 1M kwa miaka mitatu faida laki 3!!!?? Hyo faida muuza supu na chapati anaingiza kwa muda mfupi sio huo wa kwenu

Anyway.....mfumo wa uchumi ulivyo ni kwamba taasisi za kifedha kama benki huwa hazina urafiki na maskini (mwenye kipato kidogo) badala yake ni kumkamua alicho nacho kwa kutumia "lugha tamu inayovutia"
wamenikiosa.....niliikomalia sana hii deal nilijua inalipa
 
Kwa ndugu zangu wa mikoa mingine isio kuwa kipenzi wa banki hii na Nbc misishiriki kabisa kununua. Hata kuweka pesa hii benki ni wabaguzi kweli kwenye ajira tena ubaguzi ulokithiri. Hapa zaidi ni ni mkoa mmoja tu wa kaskazini. Wengini wa kuhesabu au wapo kwa address ya wakubwa.
Bank hizi ni nadra kuajiri waislam ...sana utawakuta wawili watatu watoto wa wakubwa au kitengo cha bank ya kiislam.
Hizi bank zilikua mali ya umma..hivyo kutoa ajira kwa misingi ya dini na kabila fulani haikubaliki....na tatasema ili waislam na wamakonde nao wapate kazi ...wacheni ubaguzi...
 
Naona Sera ya magufuli kuondoka hela za serikali kwenye mabenki imeanza saidia, sasa mabenki hayana hela za kukopesha lazima yakope kwa watu ili wakopeshe wengine!
Safi sana JPM,
 
Mmh bopwe sijakupata vrma
 
Naona Sera ya magufuli kuondoka hela za serikali kwenye mabenki imeanza saidia, sasa mabenki hayana hela za kukopesha lazima yakope kwa watu ili wakopeshe wengine!
Safi sana JPM,
Mmh sidhani kama hili liko kwa mtazamo huo
 
Naona Sera ya magufuli kuondoka hela za serikali kwenye mabenki imeanza saidia, sasa mabenki hayana hela za kukopesha lazima yakope kwa watu ili wakopeshe wengine!
Safi sana JPM,
Imesaidia nini sasa? Kama ni kweli hawana hela ya kukopesha si ndo wananchi watazidi kuumia au?
 
Hii inafaa wanaoweka pesa bank hawana cha kuzifanyia lakini si sisi waganga mjaaa...faida ni ndogo sana nikilinganisha nifanya biashara ya uchuuzi nitapata kubwa kuliko hiyo..

Hati fungani ya NMB ni kwa kila mmoja.
Hati fungani ya NMB inamlenga kila mmoja ambaye anataka kuwekeza na NMB ili kupata malipo ya kuridhisha. Hati fungani ya mauzo inawafaa wale ambao wanapenda malipo ya mara kwa mara au kipato endelevu au walio na upeo wa uwekezaji wa kati na wa muda mrefu. Ofa ya hati fungani ipo kwa ajili ya wale walio na wasio wateja wa NMB.
 
Tarehe 8 mwei huu wa June itakuwa siku ya mwisho kununua Bonds za NMB..
NMB ndio kampuni ya kwanza kuuza Bonds Tanzania kwa public...
Bonds tofauti na hisa huwa hazishuki thamani..ziko fixed
Nchi za wenzetu ni kawaida sana hapa ketu ndo baado tunaanza...

Ushauri wangu wale ambao mnaweza kununua bonds hizi mjitokeze kabla ya deadline
ili angalau zoezi hili liwe la mafanikio kampuni zingine zivutike kuuza bonds pia..

Kwa wale ambao hawajui tu ni kuwa NMB sasa ndo benki kuubwa kuliko zote Tanzania
kwa kila kitu.....(i stand to be corrected)

Kwa idadi ya wateja
ukubwa wa mtaji
thamani ya kampuni na kadhalika....

na sekta ya benki Tanzania bado changa sana...kwani watanzania wanaotumia banks
hawafiki mlioni 3 huku wenye uwezo wa kutumia bank wapo zaidi ya milioni 20

hii ina maana bank zitazidi tu kukua....na thamani ya hizi bank itazidi kuongezeka

mfano mzuri ni hisa tu za NMB....walionunua wakati zinaanza (IPO) leo thamani ya hisa zao
wengi ni mabilioni ya shilingi...na sasa watu kutoka Europe hadi USA wanakuja kununua hisa za NMB

Na hizi Bonds za NMB mwaka huu ndo mwanzo tu .....miaka michache ijayo usishangae zikavuta watu kutoka mbaali sana huku sisi wenyewe tukiwa hapa hapa...

Ningependa hii thread tueleweshane faida za bonds hizi.....na tuhamasishane......
 
Mi nitaweka 500,000 kwanza
Afu baada ya hapo tutaona itakuwaje
Tatizo la sisi Watanzania tunakujaga shitukia vitu muda ummeenda sana
Mfano kwenye hili la Bond mimi na 500,000 yangu siwezi faidi sana
Anaefaidi ni atae weka 1bil na kuendelea
 
Mi nitaweka 500,000 kwanza
Afu baada ya hapo tutaona itakuwaje

Mkuu bond ina tofauti na hisa
usiweke tu kutazama itakuaje
weka na uliza kabisa bond ikiiva utalipwa ngapi
na utalipwa tu....hakuna kupanda wala kushuka kwa thamani
weka hata milioni 500 kama una uwezo
kabla ya kuweka wanakupigia hesabu utalipwa ngapi ikiiva....unajua kabisa
 
Asante kwa ushauri
Kwa awamu hii mi nawashauri wanaojenga magorofa kariakoo bora wakanunue hizo bond wana uhakika wa kupata hela nyingi kwa mwaka kuliko kodi wanyoingiza kwa mwaka
 
Hivi walisema ukiweka unapata faida ya asilimia ngapi vile?
 
Back
Top Bottom