Hati fungani za NMB zimekuja kwa ajili ya watu wenye kipato cha chini ile wenye kuweka hela (saving) kiasi na hawaitumii mpaka muda waliojipangia au dharula inapotokea.
Hizi za NMB zimegawanywa katika 500,000/- kwa bond, ni watu wengi sana wenye kipato cha wastani huwa wanakuwa na balance ya namna hii au zaidi kwenye acc tena inakuwepo kwa zaidi ya mwaka inakatwa tu monthly charges nk, badala ya kuongezeka inapungua.
Hii 500,000 haiwezi kununua fixed deposit (FDR) kwa sababu mara nyingi FDR zinakuwa na min limit ya zaidi hata mili 5 na kuendelea, na rate zake ni 12-16. Ili upate rate ya 15 au 16 ni lazima uweke hela nyingi kuanzia hata mil 100. Kwa mil 10 unaishia kupata 12 au 13, so kama unaweza kupata 13% kwa sh 500,000 ni faida sana.
Hati fungani za serikali ni kwa wenye hela nyingi zaidi, maana unakuta moja inauzwa kwa sh mil 500 na kuendelea na ni kwa miaka 5 au zaidi, rate zake mara nyingi ni 14-16.5%. Hizi sisi hatuwezi.
Kuna watu wanasema kuliko kupata hiyo faida ya 130,000 kwa mwaka akiweka mil 1 ni bora akafanyie biashara gani apate faida zaidi, sasa watu hawa hawa unakuta anaongea hivyo ana hela benki ambazo zipo tu na hata hizo biashara hawafanyi na hela inakatwa charges.
Pole pole watu wakielimishwa wataelewa. Uzuri hii ukiwa na dharula inauzika haraka, na kwenye kuuza utapata faida ila siyo kama ambayo ungepata ukisubiri muda uishe, kuna gharama ya kutoa hati mapema itaathiri faida ila hela yako yote utaipata.