Kwanini usijengwe ukuta katikati ya barabara za mikoani kupunguza ajali?

Kwanini usijengwe ukuta katikati ya barabara za mikoani kupunguza ajali?

Shida kubwa na chanzo Kikuu cha ajali ndani ya nchi yetu ni Kama zifuatazo;

1. Uchovu wa Madereva wakiwa barabarani.
2. Magari mengi Ni mabovu hasa malori hivyo ni Kama majeneza yanayotembea
3. Ulevi kwa madereva, Tanzania tunajifanya Sheria haziruhusu kuendesha ukiwa tayari umeshakunywa pombe wakati tunaona bar Nyingi walevi wanakuwa wamepaki magari wakiwa bar wanakunywa na wakitoka wanaenda kuendesha magari huku Polisi wakiangalia tu kisubiri ajali itokee wapige pesa ndefu.
4. Kutokufuata Sheria za barabara, huu ni ugonjwa wa Madereva wengi wa Tanzania hasa wakati wa ku overtake ,tunatake risk sana, ajali nyingi zinatokana na kuovertake sehemu isiyoruhusiwa.

Turudi kwenye mada kuu, ajali nyingi za siku hizi ni kwamba roli linahama upande wake linaenda upande wa pili halafu chuma zinagongana uso kwa uso, na ni nyingi sana ajali za namna hii kwaKuwa malori ni mengi mno nchi hii wameua reli, sasa sijui reli ije tu ili waondoe haya malori kwa road.

Sasa kwanini serikali isijenge ukuta katikati ya barabara Ili Lori likitaka kuhamia upande wa pili lishindwe hivyo kuepusha Ajali.

Wanaweza wakaweka ukuta hata mita moja, ukuta mgumu na mrefu, kwakuwa ajali zimezidi sana na wewe unaesoma muda wowote utapata ajali ya kugongana uso kwa uso na roli.
🙈 Hongera kwa kuwaza mbali Ila kwa ile nchi ya kusadikika ya Hawa wadanganyika ni mambo yasiowezekana hata Kama ingekuwa rahisi kiasi gani
 
Shida kubwa na chanzo Kikuu cha ajali ndani ya nchi yetu ni Kama zifuatazo;

1. Uchovu wa Madereva wakiwa barabarani.
2. Magari mengi Ni mabovu hasa malori hivyo ni Kama majeneza yanayotembea
3. Ulevi kwa madereva, Tanzania tunajifanya Sheria haziruhusu kuendesha ukiwa tayari umeshakunywa pombe wakati tunaona bar Nyingi walevi wanakuwa wamepaki magari wakiwa bar wanakunywa na wakitoka wanaenda kuendesha magari huku Polisi wakiangalia tu kisubiri ajali itokee wapige pesa ndefu.
4. Kutokufuata Sheria za barabara, huu ni ugonjwa wa Madereva wengi wa Tanzania hasa wakati wa ku overtake ,tunatake risk sana, ajali nyingi zinatokana na kuovertake sehemu isiyoruhusiwa.

Turudi kwenye mada kuu, ajali nyingi za siku hizi ni kwamba roli linahama upande wake linaenda upande wa pili halafu chuma zinagongana uso kwa uso, na ni nyingi sana ajali za namna hii kwaKuwa malori ni mengi mno nchi hii wameua reli, sasa sijui reli ije tu ili waondoe haya malori kwa road.

Sasa kwanini serikali isijenge ukuta katikati ya barabara Ili Lori likitaka kuhamia upande wa pili lishindwe hivyo kuepusha Ajali.

Wanaweza wakaweka ukuta hata mita moja, ukuta mgumu na mrefu, kwakuwa ajali zimezidi sana na wewe unaesoma muda wowote utapata ajali ya kugongana uso kwa uso na roli.
Umezingua hapo mwisho ulivyomalizia kuwa sie tunaosoma tutapata ajali ya kugongana uso kwa uso na lori.
 
Dawa ni kuweka fine KUBWA kwa madereva wazembe wote. Hapo lazima watatia adabu. Kama nchi za wenzetu ughaibuni. Speed ikiwa kubwa tofauti na iliyowekwa barabarani, Ukipiga hata UTURN au uvuke mstari usiokuhusu au ujipitie service road kiboya boya fine kama zote.
 
Safi sana kwa kufikiri vyema mtoa mada. Usifadhaishwe na wapumbavu wanaoamini wanatunza familia kwa mawazo yao bora ilhali hawana uwezo wa kufikiri.

Naamini ulilenga kuwasilisha kitu kama Concrete Barriers, yes inawezakana concrete ni urefu 2 to 4 feat na inaweza kuzuiza magari kuintervene. Mamlaka zifanyie kazi wazo lako.

View attachment 2196430

Kama picha inavyoenesha ukianza kwenda hadi tamati au eneo rasmi la kuingia njia nyingine hii imesaidia sana mataifa mbalimbali kupunguza ajali.
Kwahiyo unaunga mkono kuwekwe kitu kama hicho kwenye upana wa barabara hizi hizi tulizo nazo?.Hao wenzako wanaweka kutenganisha barabara pana kuanzia two,four way nakuendelea nasio kama hizi zetu.Barabara zetu ni nyembamba kiasi ambacho hata ule mstari mweupe wa katikati unakanyagwa na tairi.sasa ndo tuweke hayo makitu si itakua kichekesho.
 
Unachekesha sana aise

Jibu ni haiwezekani kujenga ukuta
Nadhani hujaelewa hoja yake, ambayo kimsingi ina mashiko sana.. Angalia hii hapa chini... Sema tatizo lililopo ni wembamba wa barabara zetu...
Screenshot_20220424-104102.jpg
 
Safi sana kwa kufikiri vyema mtoa mada. Usifadhaishwe na wapumbavu wanaoamini wanatunza familia kwa mawazo yao bora ilhali hawana uwezo wa kufikiri.

Naamini ulilenga kuwasilisha kitu kama Concrete Barriers, yes inawezakana concrete ni urefu 2 to 4 feat na inaweza kuzuiza magari kuintervene. Mamlaka zifanyie kazi wazo lako.

View attachment 2196430

Kama picha inavyoenesha ukianza kwenda hadi tamati au eneo rasmi la kuingia njia nyingine hii imesaidia sana mataifa mbalimbali kupunguza ajali.

Hakika
 
Watu wanamdhihaki! bila kutoa altenative ya suluhu ya ajali!

Innovation huanza na mawazo finyu sana, lakini kadri watu wanavyoboresha ndipo mafanikio hupatikana.

Watanzania tubadilike, unamdhihaki mtoa mada, wewe umechangia jambo gani katika taifa lako likawa na tija!?

Mfano, alivyosema ukuta, mwingine akaja na idea ya barabara mbili,
1. Maalumu kwa ajili ya gari za mizigo
2. Maalumu kwa ajili ya gari za abiria.

Lakini mwingine akaja na Idea ya kudhibiti wanedesha magari makubwa na mabasi, kwamba wawe na umri kuanzia miaka 45 na kuendelea!

Au, ni marufuku kufika maeneo ya bar na gari binafsi, gari zote ziendaazo maeneo ya bar ziwe za biashara eg Ubber, or tax.

Hayo yote hapo ni mawazo ambayo mtu anafikiria kutokana na agenda iliyoletwa! maana yake bila agenda hiyo watu wasingewaza hayo.

Hivyo, wazo linanavyozidi kuboreshwa ndivyo mafanikio yake hupatikana na sio kumkashifu mtoa mada
Una mawazo kama sukuma gang
 
Barabara zetu zimejengwa kwa kiwango cha SERIKALI YA UCHOCHORONI. Hazina hadhi ya kimataifa. Barabara ya mkoa eti ni single lane. Yaani ili nikuovertake inabidi nichukue tahadhari halafu niongeze kasi.

Sasa nitafanya mara ngapi huo mchezo kwa kilometers zote hadi nifike ninapokwenda.

Na shida ni watu kuwa na shuguli za kibinadamu pembezoni mwa barabara. Yaani gari ikiwa kasi ikafeli break then utasikia imeingia kwenye maduka au nyumba ya mtu.

Ili kurekebisha, barabara ya mkoa at least iwe na lane tatu tatu kila upande yaani njia sita. Katikati ya barabara kunawekwa zile partition / Barriers za zege ambazo hata gari kutoka upande m'moja ikileta ufala inakwenda kugonga na kutulia hapo kati bila kuleta madhara kwa upande wa pili.

Jambo lingine. Kutoka hapo ilipo block yaani center ya barabara inatakiwa zihesabiwe mita 70 (Futi 210) kila upande yaani kutoka ile chaki inayotenganisha upande wa kwenda na upande wa kurudi kila upande uhesabiwe upana wa mita 70.

Kusiwe na shughuli yoyote ya kibinadamu ndani ya hizo mita 70 zaidi ya miundo mbinu ya barabara na ishara za usalama na kadhalika.

Hii ikifanyika itapunguza tu sio ajali kwa asilimia 90% but pia itapunguza masaa ya kusafili ambayo husababishwa na sheria mbovu za kichovu kama za kutembea speed 50km/h kwenye vipande vingi lakini pia, watu wataweza kunyoosha mguu bila kuhofia overtaking au tahadhari za mara kwa mara kutazama kama kuna gari inakuja mbele yako.

Ni hayo tu. Kumbukeni kuweka hii hoja kwenye katiba iwe ya kudumu mtakuja kunishukuru.
 
Inawezekana mkuu sema jamaa ameshindwa kuelezea ni ukuta wa aina gani huo!.

Huyu jamaa alitaka kusema kingo ngumu za zege ambazo kuna nchi kadhaa hata hapo Kenya zimejengwa kwenye ile High Way ya kuelekea kasikazini, hata mtu wa kutembea kwa miguu huwezi kuruka kwa haraka.

Hii kitu ni nzuri sana tatizo ni mfumo na serikali kuamua kuwekeza kwenye eneo hilo.

View attachment 2196546View attachment 2196547
Nafikiri hatakiwi kubezwa, kwan ana mawazo, chukulia barabara ya mabasi ya mwendokasi pia kuna hizo kingo japo si ndefu lkn kwa asilimia kubwa zinasidia kupunguza ajal na hata gari linapopata ajali upande mwingine ni salama kabisa.
 
Labda ungeshauri ONE WAY.
Yaani njia ya kwenda IPO peke yake na kurudi ipo peke yake
 
Sasa hii imeingiaje kwenye mada iliyoletwa?
Kuna mtu alisema yeye sio msukuma hivyo nikawa namfafanulia kuhusu Sukuma gang ni watu wa aina gani. Sukuma gang siyo wasukuma kama kabila ila ni watu kama wewe, Bashite, Saambaya, bushiru, Ndogoguy na the like
 
Back
Top Bottom