Kwanini usijengwe ukuta katikati ya barabara za mikoani kupunguza ajali?

🙈 Hongera kwa kuwaza mbali Ila kwa ile nchi ya kusadikika ya Hawa wadanganyika ni mambo yasiowezekana hata Kama ingekuwa rahisi kiasi gani
 
Umezingua hapo mwisho ulivyomalizia kuwa sie tunaosoma tutapata ajali ya kugongana uso kwa uso na lori.
 
Dawa ni kuweka fine KUBWA kwa madereva wazembe wote. Hapo lazima watatia adabu. Kama nchi za wenzetu ughaibuni. Speed ikiwa kubwa tofauti na iliyowekwa barabarani, Ukipiga hata UTURN au uvuke mstari usiokuhusu au ujipitie service road kiboya boya fine kama zote.
 
Kwahiyo unaunga mkono kuwekwe kitu kama hicho kwenye upana wa barabara hizi hizi tulizo nazo?.Hao wenzako wanaweka kutenganisha barabara pana kuanzia two,four way nakuendelea nasio kama hizi zetu.Barabara zetu ni nyembamba kiasi ambacho hata ule mstari mweupe wa katikati unakanyagwa na tairi.sasa ndo tuweke hayo makitu si itakua kichekesho.
 
Unachekesha sana aise

Jibu ni haiwezekani kujenga ukuta
Nadhani hujaelewa hoja yake, ambayo kimsingi ina mashiko sana.. Angalia hii hapa chini... Sema tatizo lililopo ni wembamba wa barabara zetu...
 

Hakika
 
Una mawazo kama sukuma gang
 
Barabara zetu zimejengwa kwa kiwango cha SERIKALI YA UCHOCHORONI. Hazina hadhi ya kimataifa. Barabara ya mkoa eti ni single lane. Yaani ili nikuovertake inabidi nichukue tahadhari halafu niongeze kasi.

Sasa nitafanya mara ngapi huo mchezo kwa kilometers zote hadi nifike ninapokwenda.

Na shida ni watu kuwa na shuguli za kibinadamu pembezoni mwa barabara. Yaani gari ikiwa kasi ikafeli break then utasikia imeingia kwenye maduka au nyumba ya mtu.

Ili kurekebisha, barabara ya mkoa at least iwe na lane tatu tatu kila upande yaani njia sita. Katikati ya barabara kunawekwa zile partition / Barriers za zege ambazo hata gari kutoka upande m'moja ikileta ufala inakwenda kugonga na kutulia hapo kati bila kuleta madhara kwa upande wa pili.

Jambo lingine. Kutoka hapo ilipo block yaani center ya barabara inatakiwa zihesabiwe mita 70 (Futi 210) kila upande yaani kutoka ile chaki inayotenganisha upande wa kwenda na upande wa kurudi kila upande uhesabiwe upana wa mita 70.

Kusiwe na shughuli yoyote ya kibinadamu ndani ya hizo mita 70 zaidi ya miundo mbinu ya barabara na ishara za usalama na kadhalika.

Hii ikifanyika itapunguza tu sio ajali kwa asilimia 90% but pia itapunguza masaa ya kusafili ambayo husababishwa na sheria mbovu za kichovu kama za kutembea speed 50km/h kwenye vipande vingi lakini pia, watu wataweza kunyoosha mguu bila kuhofia overtaking au tahadhari za mara kwa mara kutazama kama kuna gari inakuja mbele yako.

Ni hayo tu. Kumbukeni kuweka hii hoja kwenye katiba iwe ya kudumu mtakuja kunishukuru.
 
Nafikiri hatakiwi kubezwa, kwan ana mawazo, chukulia barabara ya mabasi ya mwendokasi pia kuna hizo kingo japo si ndefu lkn kwa asilimia kubwa zinasidia kupunguza ajal na hata gari linapopata ajali upande mwingine ni salama kabisa.
 
Labda ungeshauri ONE WAY.
Yaani njia ya kwenda IPO peke yake na kurudi ipo peke yake
 
Sasa hii imeingiaje kwenye mada iliyoletwa?
Kuna mtu alisema yeye sio msukuma hivyo nikawa namfafanulia kuhusu Sukuma gang ni watu wa aina gani. Sukuma gang siyo wasukuma kama kabila ila ni watu kama wewe, Bashite, Saambaya, bushiru, Ndogoguy na the like
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…