Nawaza kuna ambao kwa sababu ya kuchelewa kupewa mrejesho, imebidi waendelee kuomba nafasi mpya zinazotoka. Shida ni kumbe kwenye maombi au taarifa walizopandisha kwenye mfumo, kukawa na dosari bila ya wao kujua chochote. Pengine makosa ya uandishi wa barua, vyeti kitopitiwa na wanasheria, au hata kutoonekana vizuri kwenye pdf.
Majibu yanakuja kutoka, wanagundua kinachosababisha wasiitwe ni hayo makosa yaliyopo wakati anafanya maombi yote na kwa hivyo hawana vigezo vya kuitwa kwenye kazi zote walizoomba.