Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Wanajamvi nilitaka kujua kwanini utumishi hutumia takriban miez miwili kuita watu kazini baada ya kufanya Oral, kuna nn kinacho endeleea.
Kwa ninavyoona mimi, tatizo Tanzania ajira chache. Watu wengi wanafukuza kazi chache. Uchumi mdogo.

Waajiri wana nafasi ya kuringa.

Nchi yenye kazi nyingi na watu wachache, waajiri wanakuwa wanaajiri haraka sana, wanaogopa wakichelewa kuajiri tu watu wenye vipaji watakwenda kuajiriwa sehemu nyingine.

Bila kurekebisha tatizo hili la msingi la uchumi na ajira, waajiri watakuwa na nguvu sana na kufanya ajira kwa ratiba wanazotaka wao.

Kuna mambo mengine ya kiutendaji, mambo ya serikali kuwa na urasimu na ukiritimba mwingi, lakini hili la uchumi ndilo la msingi.
 
uliomba kazi gani mkuu..?
Mtakwimu
Screenshot_20220720_230359~2.jpg
 
Utumishi wameitwa watu wa PPRA kwenda kwenye Usahili Dodoma.. naona mida ya Mikeka kutema imewadiiia.
Hapa kama ulipata nafasi ya Sensa na umekuwa Shortlisted linakuwa pigo nalo hilo[emoji2][emoji2]
Sensa ni miyeyusho tu, wakapambanie tonge la muda mrefu huku, hata hivyo usahili mwisho tarehe 20 watawahi kwenye sensa tarehe 23
 
Nawaza kuna ambao kwa sababu ya kuchelewa kupewa mrejesho, imebidi waendelee kuomba nafasi mpya zinazotoka. Shida ni kumbe kwenye maombi au taarifa walizopandisha kwenye mfumo, kukawa na dosari bila ya wao kujua chochote. Pengine makosa ya uandishi wa barua, vyeti kitopitiwa na wanasheria, au hata kutoonekana vizuri kwenye pdf.

Majibu yanakuja kutoka, wanagundua kinachosababisha wasiitwe ni hayo makosa yaliyopo wakati anafanya maombi yote na kwa hivyo hawana vigezo vya kuitwa kwenye kazi zote walizoomba.
 
Back
Top Bottom