Vijana hasa kutoka familia za kimasikini tunalalamika hatuna connection. Hakuna kitu kinaleta amani kama unahitaji ufafanuzi wa inshu fulani, halafu unakumbuka kuna jamaa yako yupo TRA, NAOT, ORCI, IAE, TPDF etc.
Huu uzi ni kama stendi (kituo cha mabasi), watu wako hapa ili kuelekea Ofisi mbali mbali za kila aina.
Kuna watu tunawakubali na kuna watu wanatukubali, kizuri zaidi utu wa mtu au ubaya wake, ukituliza akili unaweza kujidhihirisha hata kwa ID feki.
Sasa swali ni tutafanyaje kutoka kwenye huu uzi, tutengeneze connection za kwenye maisha ya uhalisia?
Tusiishie tu kusaidiana kupata kazi, kuna maisha baada ya wote kuwa kazini.