Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Wakati mnalilia kupangiwa kazi, basi mkumbuke kuwa katika kupangiwa huko kazi mnaweza kupelekwa Vijiji ambavyo kutoka Halmashauri husika ni zaidi ya 60KM

Kwahiyo sio mnafika huku mnaanza kuhaha kuanza kujutia na kulazimisha kuhama, vile unaitaka placement kwa hamu na shahuku basi ni hivo hivo uwe na shahuku ya kutaka kuhudumia Wananchi

Sio mnawaza kuondoa changamoto zenu tu za vipato bali mkumbuke mnatakiwa kwenda kutatua changamoto za Wanachi pia ndomana ukaenda shule hivo muwe na Passion na Taaluma zenu

Nimetoka kutembelea kituo changu cha kazi muda huu, na hizi mvua unaweza kutema bungu. [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Story za Maisha zinatofautiana Kabisa kuna watu wapo tayari kufanya Kazi Eneo Lolote lile hapa nchini Lengo lao ni kuweza kuyakabilia Majukumu ya kusaidia familia zao ambazo Yeye pekee yake ndy amefanywa Tumaini la Familia nzima.

Tukumbuke kuna watu tumebeba matumaini ya familia nzima na kuna watu wamebeba matumaini ya nafsi zao pekee Yao so hapa Level za Uvumilivu katika kuishi kwenye mazingira Magumu tunatofautiana sn.
 
Wakati mnalilia kupangiwa kazi, basi mkumbuke kuwa katika kupangiwa huko kazi mnaweza kupelekwa Vijiji ambavyo kutoka Halmashauri husika ni zaidi ya 60KM

Kwahiyo sio mnafika huku mnaanza kuhaha kuanza kujutia na kulazimisha kuhama, vile unaitaka placement kwa hamu na shahuku basi ni hivo hivo uwe na shahuku ya kutaka kuhudumia Wananchi

Sio mnawaza kuondoa changamoto zenu tu za vipato bali mkumbuke mnatakiwa kwenda kutatua changamoto za Wanachi pia ndomana ukaenda shule hivo muwe na Passion na Taaluma zenu

Nimetoka kutembelea kituo changu cha kazi muda huu, na hizi mvua unaweza kutema bungu. [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Umeongea vyema sana kiongozi binafsi naumiaga sana ninapoona wadau wanapangiwa kazi halaf wanataka kuhama.. Wakati sisi ma jobles tunatamani sana hizo fursa ili tuwatumikie wananchi kikamilifu.
 
Kwenu PSRS tunaomba tena mtangaze nafasi za CDO'S au Community Development Officers uhitaji ni mkubwa sana kwenye nchi hii kila sehemu inabidi kuwepo CDO'S au utumike utaratibu kama ule wa Tamisemi kutangaza nafasi kisha mtu anaomba wao ndio wanapanga majina moja kwa moja.

Mtaani kugumu jamani, na muda wa kustafu unasogea kwa kasi mno ikiwa bado hatujalamba asali hata ya nyuki wakubwa.
Sekretarieti ya Ajira FANYIENI KAZI HILI.
 
Au PSRS inahujumiwa ili wanaopinga Taasisi kurudishiwa mamlaka ya kuajiri zenyewe wakose chakuongea!?

Sina uhakika na nilichowaza lakini bila ya wao kujitokeza hadharani na kutoa sababu zinazoeleweka za kuchelewesha placements, itafanya ndugu zetu wanaosaka ajira kuwaza mengi zaidi ambayo yapo au hayapo. Sekretarieti ya Ajira
Mkuu, Mimi nadhani psrs ni kama wakala tu ambaye anapata oda kutoka taasisi hushika, akiambiwa leta watu analeta, vipi kama taasisi haziombi watu kwa wakati huo psrs atatoaje placements?

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, mpaka unaona tangazo la watu kuitwa kwenye usaili na PSRS ni taasisi husika iliomba kibali cha ajira kwa Serikali na kupewa, ndipo hutumia PSRS kuuendesha mchakato wa ajira na hatimaye kuwapelekea taasisi husika idadi waliyoitaka kulingana na kibali.

Hatutakiwi kuwajibia kwa tunayodhani sisi ni sababu, bali ni tuwe na uhakika au ni wao waseme rasmi kiofisi ni nini hasa kinawakwamisha kutoa placements mapema?

Lengo ni waweze kulinda imani zao kwa waomba ajira.
 
Kwanini Tusiandike barua ya wazi kwa Raisi.
 
Back
Top Bottom