Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Story za Maisha zinatofautiana Kabisa kuna watu wapo tayari kufanya Kazi Eneo Lolote lile hapa nchini Lengo lao ni kuweza kuyakabilia Majukumu ya kusaidia familia zao ambazo Yeye pekee yake ndy amefanywa Tumaini la Familia nzima.

Tukumbuke kuna watu tumebeba matumaini ya familia nzima na kuna watu wamebeba matumaini ya nafsi zao pekee Yao so hapa Level za Uvumilivu katika kuishi kwenye mazingira Magumu tunatofautiana sn.
 
Umeongea vyema sana kiongozi binafsi naumiaga sana ninapoona wadau wanapangiwa kazi halaf wanataka kuhama.. Wakati sisi ma jobles tunatamani sana hizo fursa ili tuwatumikie wananchi kikamilifu.
 
Sekretarieti ya Ajira FANYIENI KAZI HILI.
 
Mkuu, Mimi nadhani psrs ni kama wakala tu ambaye anapata oda kutoka taasisi hushika, akiambiwa leta watu analeta, vipi kama taasisi haziombi watu kwa wakati huo psrs atatoaje placements?

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, Mimi nadhani psrs ni kama wakala tu ambaye anapata oda kutoka taasisi hushika, akiambiwa leta watu analeta, vipi kama taasisi haziombi watu kwa wakati huo psrs atatoaje placements?

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app

Mkuu, mpaka unaona tangazo la watu kuitwa kwenye usaili na PSRS ni taasisi husika iliomba kibali cha ajira kwa Serikali na kupewa, ndipo hutumia PSRS kuuendesha mchakato wa ajira na hatimaye kuwapelekea taasisi husika idadi waliyoitaka kulingana na kibali.

Hatutakiwi kuwajibia kwa tunayodhani sisi ni sababu, bali ni tuwe na uhakika au ni wao waseme rasmi kiofisi ni nini hasa kinawakwamisha kutoa placements mapema?

Lengo ni waweze kulinda imani zao kwa waomba ajira.
 
Kwanini Tusiandike barua ya wazi kwa Raisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…