Through back! Hii ndio ilikuwa comment yangu bora kabisa kwa mwaka huu hapa JF na pia ndio comment maridadi kabisa tangu nijiunge na JF miaka 7 iliyopita.
Ukiniambia kwa mwaka huu umepiga hatua gani katika ndoto zako, basi sina budi kukuonesha hii comment!
Tunapoelekea kuumaliza huu mwaka hatuna budi kumshukuru anayetupatia Pumzi ya bure na kutujalia riziki ya kila siku kwa njia mbalimbali. Endapo hii pumzi ingekuwa tunailipia Bill kama ilivyo bill za umeme, maji, vifurushi vya internet, wachache sana wangemudu hii huduma, ni raha iliyoje kupewa pumzivya bure then ukaanza kuhangaikia mengine.
Uzi huu sprit yake ni KUTOKATA TAMAA, USIACHE KUJARIBU KILA UNAPOPATA NAFASI. tuishi humu.
Wale wote ambao bado wanasubiri placement, kuitwa kwenye interview msiache hii sprit ishini nayo.
Nafasi yoyote ikitokea halafu ukawa na vigezo usiache kuongeza received hata kama unasubiri placement, hivyo hivyo ukiitwa kwenye Interview nenda kafanye hata kama unasubiri placement. Siku ukiona jina lako kwenye placement basi utakuwa na uhalali wa kuacha kufanya usaili(Si huwa unawaona wazee wa mjengoni wakishashinda uchaguzi na kampeni wanaacha moja kwa moja, wengine wanaenda mbali kabisa kwa kutoonekana Jimboni hadi msimu mwingine tena[emoji2][emoji2]...!).
Kwa wale ambao wamefanikiwa kuchomoka tusiache kuwapa miongozi wanaoendelea kupambana(yaani mfundishe kuvua samaki, badala ya kumpa samaki), pia tupunguze kejeli kwa kuwaona si lolote wengine ambao hawajaweza kuchomoka kisa muda wao bado haujafika.
Ahmet meck pro mazaga one na wengineo mumepotea sana humu bila shaka mpo salama huko mlipo na mnaendelea kusukuma gurudumu vizuri