Tangu mwezi wa nane ulipoanza.
Nimejikuta moyo wangu una amani sana nilichokisubiri kwa muda mrefu sijakipata.
Nadhani sasa ni muda wa kupambana na received yangu moja.
Hii database niiweke pembeni sitaki kunipa stress kila kuchungulia mkeka jina lako haulioni na mwaka ushaisha hivyo japo naona wanachukua zaidi ya mwaka na miezi mm naassume sina changu.
Nimeshaomba sana.
Nimefunga sana.
Nadhani nafasi yangu iko.
Nawaaga jamani.
Nitarudi baadae kidogo.
Haupaswi kukata tamaa, bali unapaswa kuendelea na subira uliyokuwa nayo.
Kuchelewa kutopata ingali ushawahi kufanya Oral kuna maana yake.
Siku ukipata ndipo utaelewa, ila kwa sasa ni vigumu kuelewa kwa sababu unaona kama vile umesahaulika.
Unajua kuwa database inadumu kwa mwaka 1, kama muda huo ushapita tangu placement uliyoifanyia, focus kwenye received na kuendelea kuongeza received endapo nafasi ikitangazwa.
Ukifika Oral tena, weka max ya miezi 3 ya kusubiri placement, halafu muda wa mwaka 1 kusubiri placement ya database.
Ukifanya hivyo hautapata tabu ya kuona kama unachelewa sababu utakuwa ndani ya muda uliojipangia.
Hili suala la ajira inapaswa tulifanye kwa malengo kama yalivyo malengo ya mambo mengine, yaani ulipe muda wa kulifanya na kusubiri matokeo yake kama yatazaa matunda au la.
Ukiona umefeli/kwama unarudi kukaa chini na kuboresha mbinu ili uweze kulifanya tena kwa ubora zaidi.
Japo inafikia hatua unaona kama hauna bahati kulinganisha na mwingine, hiyo ni sehemu ya hustle na kila mmoja atafanikiwa kwa namna yake, mwingine anawahi kufanikiwa, mwingine anachelewa.