Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Ukifika eleza tatizo lako hawatashindwa kukufanyia usahili.

Tatizo kama lako njia pekee ni wao kukuandikia maswali then ukisoma swali utawajibu kwa kuongea kwa sauti.
Shukrani sana kwaushauri.... ni sahihi njia yako ni itanifaa zaidi....japo nikiwa karibu nasikia vizuri tu...ni kutojua umbali toka kwa wasahili hadi kwangu...

Ubarikiwe sana.
 
Naona Electrical degree Tushakuwa garbage ,Hadi bwawa la asali TAA nao wanatutema tu .
Wamesomba diploma tu hii pdf ya leo
Dah mkuu hata mimi naona wametutupa sana.. maana toka mwaka jana mwezi wa tano watoe nafasi 1 ile ya bunge hawajawahi toa tena nafasi mpaka leo..
Inasikitisha sana
 

Kwanza kwenye Profile yako umeonyesha ulemavu wako.

Panelist inakuwaga na watu wengi zaidi ya watano.


Kada gani kwani kiongozi maana wenye ulemavu wanapewaga kipaumbele
Kada ni Elimu ..tutorial assistant ...
 
Chapati 2 swali kada gani naona halipendi ,maana kuna mkuu hapo juu kampa ufafanuzi na yeye kaja kajibu ila hilo swali kali skip,so ukiona halijibu unaacha kumuulizaπŸ˜€
Nashukuru kwa ukumbusho mkuu...umenitag nimeona kumbe ni muhimu ili kupata taarifa zaidi.. sikutoa uzito...nashukuru
 
Elimu mkuu ....naomba Tutorial assistance, sema nakata tamaa kama naweza pita... Nimekaa muda mrefu nikiruka nafasi hizi japo confidence na material Mungu mwema najiweza.
Utapata tuu zamu yako itakuja kikubwa ufike oral na ufanye vzr na hali yako itaku feva utapochuana marks na mtu ambaye hana ulemavu wowote utapewa wewe kipaumbele ,jitahidi ufike oral
 
Wakuu..
Hivi hizi international certificates zinafanya kazi serikalini?
Zinaweza kukupandisha cheo au kukuongezea daraja la mshahara kama ilivyo private?
CCNP, ACCA n.k
 
Tangu mwezi wa nane ulipoanza.

Nimejikuta moyo wangu una amani sana nilichokisubiri kwa muda mrefu sijakipata.

Nadhani sasa ni muda wa kupambana na received yangu moja.

Hii database niiweke pembeni sitaki kunipa stress kila kuchungulia mkeka jina lako haulioni na mwaka ushaisha hivyo japo naona wanachukua zaidi ya mwaka na miezi mm naassume sina changu.

Nimeshaomba sana.

Nimefunga sana.


Nadhani nafasi yangu iko.

Nawaaga jamani.

Nitarudi baadae kidogo.
 
Nenda katambikie mizimu ya kwenu, halafu uje unishukuru.
 
Haupaswi kukata tamaa, bali unapaswa kuendelea na subira uliyokuwa nayo.

Kuchelewa kutopata ingali ushawahi kufanya Oral kuna maana yake.

Siku ukipata ndipo utaelewa, ila kwa sasa ni vigumu kuelewa kwa sababu unaona kama vile umesahaulika.

Unajua kuwa database inadumu kwa mwaka 1, kama muda huo ushapita tangu placement uliyoifanyia, focus kwenye received na kuendelea kuongeza received endapo nafasi ikitangazwa.

Ukifika Oral tena, weka max ya miezi 3 ya kusubiri placement, halafu muda wa mwaka 1 kusubiri placement ya database.

Ukifanya hivyo hautapata tabu ya kuona kama unachelewa sababu utakuwa ndani ya muda uliojipangia.

Hili suala la ajira inapaswa tulifanye kwa malengo kama yalivyo malengo ya mambo mengine, yaani ulipe muda wa kulifanya na kusubiri matokeo yake kama yatazaa matunda au la.

Ukiona umefeli/kwama unarudi kukaa chini na kuboresha mbinu ili uweze kulifanya tena kwa ubora zaidi.

Japo inafikia hatua unaona kama hauna bahati kulinganisha na mwingine, hiyo ni sehemu ya hustle na kila mmoja atafanikiwa kwa namna yake, mwingine anawahi kufanikiwa, mwingine anachelewa.
 
Dah mkuu hata mimi naona wametutupa sana.. maana toka mwaka jana mwezi wa tano watoe nafasi 1 ile ya bunge hawajawahi toa tena nafasi mpaka leo..
Inasikitisha sana
Noma sana mkuu .
Na wewe ni Electrical au Mechanical ?
Kuna moja ile walibeba jamaa kadhaa wa REA mwezi wa kwanza , tokea hapo imekuwa mtafutano , utaona wizara ya nishati Placement moja kila baada ya pdf kumi .
Dah ! πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…