Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Hivi wanavyotangaza ajira mpya na database haijaisha uwa wanamaanisha kwamba watu wote wamefeli oral au ni maamuzi yao
Kuna taasisi wanataka kushiriki kupata candidate wanayemtaka wao, hawapokei mtu kutoka kwenye database. Hivyo huwa wanataka watu wao washiriki mchakato wa kupata watumishi wanaowataka wao. Ukiona umepangiwa taasisi nzuri kutoka database ujue walikuwa na uharaka.

Ndio maana wengi kwenye database wanapelekwa LGAs a.k.a halmashauri
 
Hivi wanavyotangaza ajira mpya na database haijaisha uwa wanamaanisha kwamba watu wote wamefeli oral au ni maamuzi yao
yaani hawa jamaa hawaeleweki wengine vyeti vya bodi mpaka vinaexpire tumerenew mpaka tumechoka.watu wamechanical wamewafanyisha usaili wamewaita watatu sjui kati ya 20 alafu wanawaita usaili tena.
 
dah kama ndo ivo tunasafari ndefu
 
Hii ipo sahihi, na kwa sasa ukikosa LGA unashukuru
 
Mkuu una maanisha usaili huo ko wanakuwa na watu tayari ila wanataka tu kukamilisha taratibu za kiserikali
 
Best wishes. Kawakande kisawasawa. Huu ndio mwaka wa ku-force mpambanaji mwenzangu
Mkuu japo umenikatishaa tamaa na comment yako apo juu nimeunganisha matukio sana any way ngoja lkn nikatest mitambo interview yangu ya kwanza
 

Ingawa sio kweli hapo kwenye bold, MNH wanazidi kiasi hasa kwenye allowances ila kwa mshahara, gap ni around 300k only
 
Ingawa sio kweli hapo kwenye bold, MNH wanazidi kiasi hasa kwenye allowances ila kwa mshahara, gap ni around 300k only
Sasa laki 3 ni ndogo? Huo ni mshahra wa mtu
Pia anaweza kulipa pango la nyumba tena nyumba nzima ambayo ni fenced😀
Kwa dar au dom ni pango la nyumba nzima unakaa mwenyewe na familia yako
Hilo gep kubwa sana aisee
 
Inshallah kesho pia kazi zitaendelea kutangazwa mana safari hii naona mambo n 🔥
 

MSD, PURA, TBS, TFNC, TANROADS, GCLA, BRELA, NHC nishaona placements zao sana.

MSD mwaka jana hadi mwaka huu mwanzoni wameita watu wengi sana kazini, tena wengi wao walitokea Database.

GCLA hawa mwaka 2022 walimwaga nyingi sana na watu walizifanyia usahili, na baadae wakawa wanachukua wengine database.

TBS washatangaza mara kibao na watu washafanya sahili zao

PURA mwaka 2022 washatangaza na watu washafanya sahili zao

BRELA washatangaza nyingi tu na watu washazifanyia usahili

TFNC, TANROADS, washachukua watu database

NHC mwaka 2022 march, walifanyisha sahili kupitia PSRS, kuna jamaa aliwahi kufanya sahili hizo ila baadae akaja kupata nafasi RUWASA kupitia database.

NHIF mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2021 walifanyisha sahili za Quality Assurance Officer II kupitia PSRS, baada ya hapo sijaona tena badala yake niliona tangazo la nafasi za Management ambalo ilikuwa mwaka 2023 lakini sikuona waitwe Kwenye Interview hadi sasa.

OSHA mara chache sana nishaona placement yao wakichukua kutoka database
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…