Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Ninavyoelewa mimi ni ngumu kupewa ruhusa ukiwa mwajiri mpya ukamalize masomo then urudi kibaruani rasmi,but inawezekana kupewa ruhusa iwapo mkoa uliopata kazi na chuo unachosoma vipo sehemu moja unaweza kumuomba HR wako ukawa unaingia jioni mbali na hvyo inabidi u postpone chuo utaendelea baadaye.Pia kwa maelezo zaidi unaweza muuliza HR kwa maelezo zaidi.
 

Mkuu una utani, yani ndo kwanza wamekuajiri, wanakusubiri kwa hamu, kazi zinakusubiri za kutosha na wakupe ruhusa umalize kusoma full time?
 
Asante sana nimekuelewa vizuri kabisa
 
Akuna ugumu shida roho mbaya watu wengi wanapenda watu wasote kama wao walivyosoma Kwa kuungaunga
 
Mkuu una utani, yani ndo kwanza wamekuajiri, wanakusubiri kwa hamu, kazi zinakusubiri za kutosha na wakupe ruhusa umalize kusoma full time?
Niko tayari bila ukakasi wowote ule mkuu, ila si unajua kuuliza sio ujinga huwezi jua kumbe ningetulia kisingetokea chochote, ila kwa kuuliza labda lolote linaweza kutokea si umeona wadau baadhi wameonyesha kuna uwezekano
 
Upo kada gani mkuu, kama ni afya kwa huo mwaka mmoja uliobakisha kuhitimu hawawezi kukukatalia, ukifika ongea na Mkuu wa Idara atakuelekeza cha kufanya.

Usiwe na uoga, watu wengi wameweza kuruhusiwa kurudi shule hata wale waliokua wanaanza kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…