Wakubwa namshukuru Mungu nami nimebahatika kulamba asali naamini Mungu ni mwema kwetu sote na kila mmoja kwa wakati wake naye atailamba asali
Sambamba na hilo nahitaji sana msaada wenu wakubwa kwani katika hizi harakati za kuendelea kusikilizia asali mimi niliona nichukue muda huo kuendelea na masomo kwa ngazi ya shahada ila hilo halikunizuia kujaribu bahati yangu nilipoona nafasi zimetangazwa na kwa bahati Mungu akajalia
Sasa mwaka huu ndio nimeingia mwaka wa mwisho wa masomo kwa ngazi hiyo ya shahada, nimesikia sikia story nyingi nyingi kuhusu uwezekano wa kuomba nafasi ya kumaliza masomo kisha kuingia kibaruani rasmi, ila sijaweza kupata maelezo yaliyonyooka kuhusu hilo ndipo nikaona ni vema niwaulize wataalamu humu ili mnisaidie mwongozo juu ya hilo au ufafanuzi zaidi ili nipate kuelewa, Natanguliza shukrani wakubwa