Wakuu nina swali moja hivi kuna anayejua vigezo wanavyotumia utumishi kumpa placement mtu aliyeingia oral.
Je aliyewahi kuingia database ndio ataanza kupata placements au laa?
Mfano mwezi september nilifanya interview za MDA & LGA sikupenya oral nikalambwa NOT SELECTED zile za kada ya afya.
Baadae nikaja kufanya interview ya taasisi moja ya chuo mwezi december kwa kada yangu ambapo walitaka mtu mmoja tu oral tukaingia 12 hivi.
Mkeka wa placement ukatoka mwezi february akachukuliwa huyo mmoja nikabaki na Selected For Oral kwa akaunti yangu.
SASA IKO HIVI KILA SIKU KWENYE HIZI PDF ZA PLACEMENTS ZA WALIMU NAONA NA WATU WA KADA YANGU WAKICHUKULIWA
Ila ni wale waliofanya interview mwezi september sasa najiuliza na mimi nawez bebwa au kwa kuwa mimi interview ya oral haikuwa ya MDA & LGA ndio maana siwezi pata placement