Tuweni serious, 2018 na sasa 2022. Kama unaapply kwa mara ya kwanza kwa sasa hakikisha kila kitu kiko sawa. Mfano mimi niliapply ustate attorney na Parliamenrary draftman kwa wakati mmoja, hiyo ni mwaka huu, lakin cha kushangaza nlikuta nmekuwa shortlisted parliamentary draftman lkn state attorney sikuwa shortlisted sababu ikiwa sijaattach birth certificate, na kwel nlikuwa sijaatach, same applies pia BRELA na SELF microfinance, brela nliitwa registration officer, licencing officer nkatemwa kisa ikiwa sijaattach birth certificate, self nkaitwa, ila nlishindwa fanya interview pia kisa siku na birth certificate original na nlikuwa nshaanza kushughulikia ila RITA.
Nmefanya interview yangu ya kwanza ya land officer na ndo nlifika oral ila mpaka sasa placement bado. Ila ni baada ya kuweka kila kitu sawa. Na issue ni kwamba mpaka oral kila kitu kinakaguliwa, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kitambulisho na vitu vyote walivyosema tena wanataka original, ukipita written labda huna kimojawapo utakuja kamatwa oral, maana secretary atawacheck na bado kila kitu kitacheckiwa na hao wanaokuinterview.
Kila kitu kinawezekana, rekebisha mapema kabla hujafika huko.
Ntaandika uzi wa kila kitu kinachotakiwa itawasaidia wengine.
Ahsanteni