Aisee, kuna watu wana nyota sana, ukifikiria unashindwa kujua kikwazo kinachokusibu nini..
Mimi kama wana wameingia kwenye mirija kilaini sana.
Kuna mwamba tulipomaliza mafunzo kwa Vitendo kabla tunasubiri makibu ya pepa la leseni, tayari kapata kazi ya Tutor kwenye college fulani inayotoa kozi ngazi za certificate hadi Diploma.
Majibu yalipokuja akawa amefaulu akapata leseni kiulaini, hapo kaacha halaiki wana viporo vya kuclear sup ili wakidhi vigezo vya kupata leseni.
Zilipokuja kazi za Tamisemi, akaapply na akapata. Halaiki wengine wanaopiga miayo kitaa/kwenye vijiwe nao waliaapply ila wakakosa. Hapo sasa ule usemi wa MWENYE NACHO HUONGEZEWA tukaukumbuka.
Sasa wengine wenye nyota za kukandwa, kila tukijaribu tunakandwa tena kila sehemu[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]