Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Pale HESLB nafasi ya LOAN OFFICER II wameita watu elfu 5 na usheee hivyo wamepanga watu kwa mafungu kutokana na series namba . Ila kwa bahati mbaya SN 3901 - 4300 kwenye pdf ya kuitwa kwa usaili majina yao hayapo sana sana baadhi ya majina ya herufi M yale ya mwisho mwisho na herufi P yale ya mwanzo kama paulo n.k pia n aherufi N na O wote mfano Omari, Nasibu nk . Hivyo kama una mtu hajaona jina kwa mkeka aingie kwa akaunt yake ataona huko

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Sasa ambao hawapo kwenye Pdf watajuaje kuwa wamepangiwa room gn kwaajili ya interview?

Maana naona zimepangwa kulingana na serial number, na serial number zipo kwenye pdf
 
Umeangalia kwenye account yako hujaona chchote?
Kwenye Account ni shortlisted. Halafu kwa chini yake kuna view timetable, of which haifunguki kwa simu.Nataka enda Internet cafe kuangalia ratiba maana kwa simu haifunguki.Maana sijui ni room ipi natakiwa ingia ni jina la herufi P huko ambao hawapo ktk serials kwenye pdf
 
Kwenye Account ni shortlisted. Halafu kwa chini yake kuna view timetable, of which haifunguki kwa simu.Nataka enda Internet cafe kuangalia ratiba maana kwa simu haifunguki.Maana sijui ni room ipi natakiwa ingia ni jina la herufi P huko ambao hawapo ktk serials kwenye pdf
Download app yao itafunguka
 
Nimeitwa aisee, ngoja nikakamilishe ratiba ya mwaka huu, mikando non stop.

Hadi sasa PSRS wana clean sheet dhidi yangu halafu huu wa NAOT sina muongozo wowote, itakuwa vituko huko

Mkuu, nilikuwa nasubiri sana kuona hili jibu lako.
Kila la kheri Mkuu.
 
Upo sawa kabisa mkuu ya kufundishia ni nyepesi sana kuliko hizi zingine utapigwa maswali mpka ushangae useme jamani na hili swali linaruhusiwa [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Hahaha, maswali yanashushwa mpaka unaweza kuhisi wamepanga njama wakukoseshe kazi kwa nguvu.
 
Kawaida mie oral nimekutana na maswali mawili yamejirudia la presentation vile vile na advantage ya technology kwenye elimu au kwenye kufundishia so mpka hapo nakua nimebaki na kujieleza education background ambayo najua ni lazima so hapo kwa mahesabu nakua nimepata maswali matatu yote oral so nabaki na maswali mawili moja Toka kwenye nilichopresent ambalo ni asilimia 80 ya kulipata na jingine kuhusu kazi so hata wakiniuliza job description najibu tu so kwa mahesabu nakua nimejibu maswali yote kwa uhakika Sasa hapo no wao wanipe kazi au waninyime kazi [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hv kujieleza na education background ni swali ambalo unapata marks au Lipo tu kwa ajili ya kukutambua?then unagongwa maswali husika
 
Ahsante mkuu, tuombeane japo nionje hata oral ya kwanza

Unaionja Mkuu, tunakuombea kheri.

Kuna dogo mmoja amenichekesha sana, ameniambia hii vita ya NAOT peke yake hatoiweza, kwa hiyo atatembea kukusanya miujiza ya manabii wote aende nayo bila kukosa Mwamposa.

Nikamwambia awe makini manabii wengine hawamtegemei Mungu wanatumia shortcuts, akajibu kwenye hili tutasameheana yeye anachoangalia ni kupata kazi hata kama wanamtegemea shetani, atatubu mbele ya safari.
 
Back
Top Bottom