Dah hatari sana jamaa inaonekana wanawanyooshea sana hakuna ch3nga chenga alf taasisi zinapelekewa watumishi wasio wataka hii nchi ngumu snaa kuna watu wanaona kama yao vile
Hii ipo mzee, kuna taasisi tumelamba asali lakini unaona wazi kabisa hawakufurahishwa sio tuliokuwa nje ya mfumo wao kutoboa ilhali kuna raia wamejitolea kwa muda mrefu wamedunda, lakini ndio hivyo tena Mungu ni mwema alitupigania na tukapenya
Na hii ilinipa funzo moja, hizi taasisi au mamlaka zenyewe zingeendesha usaili hakuna hata mmoja ambae angetoboa
Na hii ni funzo kwetu, hii PSRS pamoja na vipengele vyake ila imekuwa msaada mkubwa kwa ambao hatukuwa na connection kabisa, tuiombee iendelee kuwepo
Hili suala likirudi kwenye taasisi husika, aisee watakaotoboa ni wachache sana, kuna ubinafsi mkubwa sana na kujuana
NB: Taasisi niliyotoboa (nilipost huko nyuma kwenye uzi huu shukrani zangu nisingependa kurudia) niliomba field miaka miwili nikakosa, baada ya kuhitimu nikaomba intern mara 2 niliambatanisha kila kitu mavyeti yote ila hata ujumbe wa kuitwa tu kwenye usaili sikuitwa😂😂💔
Hatimae, Utumishi wakatangaza nafasi nikajilipua. . .nilimtanguliza Mungu mbele sikuwa na uzoefu kivileee ila nikapiga moyo konde, nikapenya Written, baada ya Oral nikasubiri sana (miezi 7 kitaa, hapa katikati nilipiga interview nyingi tu ila sikupenya. . .) mpaka nikahisi ndio basi tena, ila baadae mkeka ukatoka na jina langu tena la kwanza!🙏🏿
So kuwa mvumilivu ipo siku utatoboa na usikate tamaa, apply tu ukiitwa Dodoma nenda, ukikosa nauli piga moyo konde, subiria inayofuata ila usisite kujaribu wala usione hatari kutumia hela yako kwenye usaili.