Sasa wenye TGS B wasemeje jamani mnapo jadiri haya,Maisha hayajawahi kuwa fair,chochote unachopata ndo sitahiki yako,kuna watu hawana kabisa hata hizo TGS wanazisikia tu.
Ni kibaya ukiwa nacho,ila usipo kuwa nacho macho yatakutoka kama mjusi kabanwa na mlango,
turidhike na tunavyo vipata,
Halimashauri hakupo kuzuri kivile ila hii hali ya ujobless kitaa ni heli uende huko harimashauri ya ndani ndani huko utaweza hata kulima
Kuliko kubaki town huna mbele wala nyuma,mwili una nuka shida ,kila mtu anakukwepa ,hata simu za wana hupati.
PATA KAZI HATA YA MSHAHARA MDOGO
WATU WATAKUHEASHIMU,HATA KUKOPESHEKA UTAKOPESHEKA KWA MANGI.
Siku zote mshahara haujawahi kutosha,unapopata ajira usiache kutafuta vyanzo vingine vya kukuingizia kipato,mana kama mtaji unaweza kujichnaga mwenyewe japo kwa mda mrefu ukaanzisha chochote hata cha kukuingiza mia mbili .
UJOBLESS NI MBAYA MNO ,USIKIE KWA JIRANI TU,UNATWEZA UTU,HESHIMA INAPOTEA,UNALETA UTENGANO KWA NDUGU,UNALETA MAFARAKANO NA JAMII UNAYO ISHI NAYO .
NGUO HUWA ZINAPAUKA,SIMU NAYO INATAFUTA SABABU ZA KUTENGANA NA WEWE MARA INAKUFA SYSTEM CHARGER,AU UNASHANGAA INAIBIWA KABISA KATIKA MAZINGIRA TATANISHI,NA UKIELEZA WATU WANAKWAMBIA UMEIUZA.
HATA WAREMBO UTAWASIKI TU ,HATA UKIKUTANA NAO UWAPE SALAM HAWAITIKII.