Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Acha tu mzungu anajua kucare hawana longo longo za kikuda wala majivuno kama ma Hr wakibongo.Mbongo akiona mtu anataabika ndio roho yake inafurahi.

Sijawahi kufanya interview hata moja ila hii ya bomba la mafuta la east africa ndio imekuwa ya kwanza aloo mzungu mzungu tu.

Tulikuwa wengi tulioitwa kwenye interview almost 300 ila hata kama uko kijiji gani utalipiwa nauli hadi ufike dar kwenda na kurudi usafiri wowote utakaopenda ila usipande ndege tu[emoji3][emoji3].Hii ni kwa both oral and written.

Ukilala hotelini hata kama ni guest ya 5000 ,watakulipa 70,000 per night. Hotel tuliokuwa tukifanyia interview sasa ni seacliff [emoji3][emoji3]. Pesa ya kula 30,000

Na hapo Hotelin unakuta wamekuandalia Chai nzito vitafunwa vya kila aina, maji, chocolate,pipi yaani watakulazimisha ule hata kama hutaki utakula tu.

Hoteli ile ni kubwa ila kuanzia getini utakaribishwa kama mfalme. Kuna wale ambao kwa namna moja ama nyingine walikuwa wanashindwa kufika kwenye interview yaani utapigiwa simu wanakuuliza kama utaweza wakupangie siku nyingine. Kuna jamaa alisema siwezi kuja sababu sijajiandaa wakawa wanambebeleza njoo hivyo hivyo ujaribu bahati yako.

Maswala sijui ya kubeba mavyeti hawataki ni wewe na I'd yako yoyote. Ukimaliza interview unaenda kwa cashier anakulipa pesa zako zote ndio unasepa.

Kwenye oral interview kila mtu alikuwa amepewa saa moja kwenye venue uliopangiwa mfano ukachelewa wanam interview mwenzako aliewahi halafu wew watakuinterview baadae sio kama wabongo eti ukichelewa hata kwa bahati mbaya ndio imekula kwako na mabango juu.

Wakati wa interview sasa nilikuwa najiuliza nitaongea kizungu gani mimi na wazungu kwenye lisaa lizima wakati kizungu chenyewe sijui aloo wale jamaa wanajua kucare [emoji3][emoji3][emoji3]interview zote zingekuwa hivyo daa wakiona kuna swali unatapa tapa kujibu wanapredict unachojaribu kujibu wanakuolezea mpaka mwenyewe unasema yes yes yes ndio hiyo.

Au wakiona umechoka kidogo wanakwambia pumzika dakika tano kunywa maji Kisha tuendelee. Ambao tumepita oral interview last month tumeambiwa tutafute best private hospital yoyote iliyo kwenye mkoa uliopo Kisha tuwatumie ndio tunasubiri majibu yao twende kwenye medicals.

Sent from my SM-A025U using JamiiForums mobile app
Sasa kwa kuyajua haya yote watu bado wanahangaika na interview za Serikali za nini?. Mimi huko Serikalini nimewahi hudhururia interview Moja tu, tena nilizuiliwa kuingia kisa Sina NIDA, nikiwa na namba tu wakagoma. Tangu siku hiyo sintokuja kuhudhuria interview za utumishi, nawala sijutii kutopata kazi Serikalini. Kwanza wanalipa mishahara midogo halafu masimango wakati wa interview kama yote. Wanaona wao ndio wameshikiria maisha ya watu.
 
Mkuu atafutae hachoki, akichoka ujue kapata
 
Mkuu atafutae hachoki, akichoka ujue kapata
Polen sana waku, lakini private sector nyingi wako fair kuliko Serikalini ndio maana taasisi nyingi za Serikali ni magumashi. Nimefanya interview nyingi sana na private sector wengi wao wako very positive hata kama hutopata kazi lkn utapata experience yakutosha. Mtu anaetafuta kazi Private sector probability yakupata kazi nzuri nikubwa kuliko huko Serikalini.
 
Hivi hao waliokua wako siriously salary inaanza na ngapi?.
Itakuwa wanalipwa parefu mwaka mmoja tu walikuwa wamenunua magari makali balaa. Na kuanzia mwaka huo huo wakaanza kupelekwa vyuo vya njee kuchukua masters kwa awamu wengi uingereza, India na japan .Yaani ilikuwa tu ufikishe hiyo GPA hakuna baba kanituma wala nn

Sent from my SM-A025U using JamiiForums mobile app
 
Sasa kwa kuyajua haya yote watu bado wanahangaika na interview za Serikali za nini?. Mimi huko Serikalini nimewahi hudhururia interview Moja tu, tena nilizuiliwa kuingia kisa Sina NIDA, nikiwa na namba tu wakagoma. Tangu siku hiyo sintokuja kuhudhuria interview za utumishi, nawala sijutii kutopata kazi Serikalini. Kwanza wanalipa mishahara midogo halafu masimango wakati wa interview kama yote. Wanaona wao ndio wameshikiria maisha ya watu.
Hata hii interview tuliyofanya government ana hisa zake nasikia ewura alitaka yeye ndio awe anasimamia maswala ya kuajiri pamoja na tpdc Mzungu akakataa wenyewe wanatumia hizi agencies kutafuta watu. Hawaangalii sijui wewe ni mtoto wa nani au status ya mtu maana jamaa kuhusu maokoto kwao sio tatizo hawana njaa

Sent from my SM-A025U using JamiiForums mobile app
 
Kuna ile kuwa ushawahi kuwa na check namba halaf kazi ukaacha mwenyewe au hata wakakuachisha wenyewe sasa ukataka kurudi tena serikalini (Hata kama sababu za kuacha ni genuine)

Mziki wake unaweza tumia hata miaka 3 bado wapo wanashughulikia🥲🥲🥲🥲
Jambo unaloona lnaweza malizwa ndani ya mwezi lnavyozungushwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom