Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Si kuna ajira alizosem wazir Simbachawene zitamwagwa almost elfu 44 kunzia mwezi huu mpk wa 7..so tusubir mambo ayo tuone,maana baada ya mwaka 2025 naona ngma itakua ngumu,watu washaingia madarakani apo 2026[emoji50]‍[emoji100]
Ukisubirigi yanayosemwa utakesha saaaana!.
Kwa kuongea na kuaminisha watu viongozi wetu wapo vzr ila njoo kwenye uhalisia.

Mm I wish akisema ajira ni 44k na vibali vishatolewa sasa nione tangazo lenye kuhitaji hao watu hapo ingekuwa magoli saaana na nadhan hata huko kulalama kwa sana kwa sisi vjana kusingekuepo. Ila unastukia mwaaaaaaka huooooooo unakata huelewi elewi 44k inavyoishilia
 
utum.jpg
 
Wote ambao walifaulu oral watapata nafasi kwa muda wao.

PSRS wanapoita watu wengi oral huku nafasi zikiwa chache sio kwamba wanataka kuwapotezea watu muda, hapana.

Hapo inakuwa ni Advantage kwa pande zote mbili(PSRS na Jobless). PSRS wataokoa muda wa kusaili mara kwa mara kwa nafasi zile zile kwa kuweka hao akiba ili waje kuwapangia nafasi baadae. Jobless wanakuwa wanaokolewa pia kwenye ishu ya muda na gharama za kwenda kufanya usaili tena.

Kwahiyo pindi ukiitwa kwenye usaili, kuwa na malengo 2 hata kama nafasi ni 1.

Lengo la kwanza, kafanye usaili ili upatw hiyo nafasi kwa muda huo.

Lengo la pili, kafanye usaili ili ubaki database endapo lengo la kwanza likikwama. Kukaa database ni ushindi kulinganisha na yule aliyeogopa kwenda kufanya kisa nafasi ni 1 na akaamua kutoenda ili asipoteze muda na pesa.

Mimi nilijiwekea hayo malengo 2 hasa lengo la pili baada ya kukandwa saili za mwanzo(saili 3). Bahati nzuri nikaangukia kwenye lengo la kwanza, pia hata kama ningekwama kwenye lengo la kwanza ningekuwa nishatimiza lengo la pili hadi sasa maana tayari kundi letu lote tushapangiwa kazi
Nawatakieni maandalizi mema ya mikando iliyopo mbeleni.
 
Back
Top Bottom