Habarini Ndugu zangu wapambanaji.
Naomba kwa yeyote aliepata kazi au alieshikwa mkono akalamba asali, Sifa na Utukufu ampe Bwana, maana hata kama umeshikwa mkono ni Bwana katengeneza njia kwa huyo mtu alifanikishe.
pia tafadhalini msinitumie msg Pm, sijahusika kwenye Asali ya Pinaco, ila tu niliguswa sana na namna alivyokua aki appear humu kila siku na karibia kila page lazima awepo, mkumbuke humu ndani kuna watu mbali mbali wanapitia, wapo wanaochangia moja kwa moja, na wapo wasiochangia ila wanazipitia conversations zenu kwa uzuri.
Ni sawa na ule uzi wa bwana mdogo Rick Boy kuna siku nilistaajabu kusikia mtu akiuzungumzia nikiwa sehemu ambayo si rahisi kuamini kama yipo mtu wa jamii Forum.
I am just a normal guy, ilaa... kuna uwezekano kulingana na watu wa hapa na pale naowajua naweza washirikisha sikitiko la mtu flani sio mfano mtu mmoja au wawili na kama Mungu akijaalia mambo yanatiki.
Hivyo kwasasa nisitumiwe msg imetokea bahati tu kwamba nilimtaja Peanacco na kumbe Mungu alikua amekwisha achilia Baraka juu yake.
Nitoe wito kwa watu wenye nafasi na network wanaopitia uzi huu najaua wapo wengi na huwa hawasemi neno, basi ukiona kuna kijana umevutiwa au kuguswa na masikitiko yake emu mtext umsaidie, ANGALIZO, MSAIDIAJI AU MSAIDIWA USIOMBWE PESA AU KUTUMA PESA ILI USHIKWE MKONO HASA KWA MTU USIEMFAHAMU, NA KAMA ITAKUJA SWALA LA SODA UWE UMEJIHAKIKISHIA KWA UKARIBU NA UHALISIA WA ASILIMIA 70-80% KWAMBA KUNA HARUFU YA ASALI YA KWELI.
Nitoe hongera kwa wote wanaotoa shuhuda za kula asali, pia wazid kuelezea hatua za kupigiwa simu ilikuaje..kufata barua ilikuaje na kureport ilikuaje, ili kuwapa moyo na kuwaburudisha walio katika lindi la kucboka.
Sifa na Utukufu kwa Bwana Yesu atupae kufikia malengo yetu na kufungua njia zetu.