Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Naombeni kuuliza swali?

Nilifanya oral moja ya hospital kubwa nchini tulikuwa watu 150+ mwezi wa nane.

Wakaitwa watu mwezi wa 11 kazini idadi walizotangaza ni 50 ila waliita watu 20 tu kazini.

Baada ya hapo hawakuita tena database mpaka mwezi uliopita ndo wakaanza kuchukua watu kwa database yetu maana muda wote walikuwa wanaita wale waliotutangulia.

Swali langu .

Je mwezi wa nane ikifika database yetu itakuwa ina expire ilhali hawajafika idadi hata ya watu 100+?
Ili usijipe pressure, assume tu itakua ime expired
 
Habari ya asubuhi. Wakuu nina GPA ya 2.7 ya public Administration inaweza nisaidia kupata kazi kupitia UTUMISHI au nilime viazi tu huku njombe.
GPA haina shida mkuu kwa post nyingi lakini kuna baadhi ya post zinahitsji GPA kubwa kama zile za Tutorial assistant na Research assistant na zinginezo inategemea uhitaji wa eneo husika lakini zilizo nyingi haziangalii GPA
 
Kwani waziri anahusika vipi na pdf ukiachana na katibu mkuu
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete kuhakikisha anafanya uratibu wa kuhakikisha Vijana wanapata ajira zinazozalishwa na Sekta mbalimbali hapa Nchini.


Akiongea Ikulu Dar es salaam leo July 26,2024 baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali, Rais Samia amesema “Mh. Ridhiwani Kikwete umekuwa Naibu Waziri Mtiifu na Bora, umefanya kazi vizuri na kutokana na kazi hiyo tumeona tukupandishe, umekuwa Waziri sasa katika Wizara hiyo ya Vijana na ajira zao na kazi lakini pia una kundi la Watu wenye ulemavu ambapo Viongozi waliokuwepo wamefanya kazi nzuri kiasi na nataka ukasimamie kazi hiyo”

“Kazi yako kubwa kwenye ile Wizara ni uratibu wa kuhakikisha Vijana wanapata ajira zao, kunakuwa na uzalishaji wa kazi katika Sekta nyingine, kilimo, madini, uvuvi kote kuna ajira kwa Vijana, nataka ukawe mratibu na ukahakikishe kila Sekta inatoa ajira kwa Vijana na tukikuuliza Ridhiwani mpaka kufikia December mwaka huu kama tupo January mwakani, tumetengeneza ajira ngapi uniambie kwenye finger tips kisekta, kilimo hizi wapo hizi, ndio kazi yako, kazi yako sio wewe kutengeneza ajira kwa Vijana, kazi yako ni kuhakikisha Sekta zinatengeneza ajira kwa Vijana nawe unaratibu kazi lakini na haki zao”
 
GPA haina shida mkuu kwa post nyingi lakini kuna baadhi ya post zinahitsji GPA kubwa kama zile za Tutorial assistant na Research assistant na zinginezo inategemea uhitaji wa eneo husika lakini zilizo nyingi haziangalii GPA
Nimekusoma kaka asante dogo kagonga GPA ndogo kinouma sana
 
Wakuu habari za asubuhi.? Samahani kwa wale mliopiga Aptitude test za utumishi mlikua mnapitia site gani zenye maswali ya aptitude test course mbalimbali. Asanteni
 
😀 sawa mkuu japo JF hapa watu hawataki kusema ni wao kila jambo akileta hapa anasingizia mdogo wangu,mwanangu,dada,kaka n.k kumbe ni yeye muhusika😀
Sasa mkuu mm rejea post angu ya juu ya kuomba huo ushauri 😂😂🤣🤣 japo na mimi nina GPA ndogo kwa michepuo ya sciance na sio arts
 
Mwezi wa Saba Unaenda kuisha


Nipende kuwapongeza.
Civil engineering.
Madaktari.
Nurses.
Famasia.
Maendeleo ya jamii.
Madaktari wanyama.
Mifugo na kilimo.

Hizi ni kada zilizoongoza kulamba asali kwa mwezi huu.

Tusubiri wa nane sijui zamu ya nani itakuwa?
 
Mwezi wa Saba Unaenda kuisha


Nipende kuwapongeza.
Civil engineering.
Madaktari.
Nurses.
Famasia.
Maendeleo ya jamii.
Madaktari wanyama.
Mifugo na kilimo.

Hizi ni kada zilizoongoza kulamba asali kwa mwezi huu.

Tusubiri wa nane sijui zamu ya nani itakuwa?
Na madereva
 
Wakuu habari za jioni.? Samahani kwa wale mliopiga Aptitude test za utumishi mlikua mnapitia site gani zenye maswali ya aptitude test course mbalimbali. Asanteni
 
Wakuu habari za jioni.? Samahani kwa wale mliopiga Aptitude test za utumishi mlikua mnapitia site gani zenye maswali ya aptitude test course mbalimbali. Asanteni
Maswali yanayotolewa ni kulingana na Kada uliyosomea hamna tofaut sana kama tulivyokua tunafanya written mwanzo except sasa hv maswali ni ya kuchagua
 
Back
Top Bottom