Kwanini viongozi wa kitaifa hupenda kula Sikukuu DSM badala ya Dodoma yalipo makazi yao?

Kwanini viongozi wa kitaifa hupenda kula Sikukuu DSM badala ya Dodoma yalipo makazi yao?

Sikukuu unakula ukiwa Nyumban sio Kazini

Dodoma ni Kazini na Dar ni Nyumban

Kambarage alikuwa sikukuu anaila akiwa kwao Butiama

Mzee Mwinyi alikuwa anailia 'kwao' Msasani

Mkapa akiwa Kwao Lupaso

Jakaya alikuwa anailia kwao Msoga

Samia anailia kwao Znz japo sina hakika kama ni Makunduchi maana Makunduchi kule ni Platform iliyomleta kwny Bunge la Jamhuri ni asili ya Baba yake

Labda kwake ni Kijitoupele au Jia la Uzi (njia kuu ya kupitishia Nyaya za Umeme) au Kiembe samaki ( Seaview ya Znz)



Baada ya Mwendazake kumaliza Mwendo sasa hivi ofisi za Wizara za Dar es salaam zimeanza kufufuliwa mdogo mdogo wenyewe wamesibatiza jina 'Ofisi ndogo ya Wizara' wameanza ku beep kuja kufanyia visemina Uchwara Dar vya wiki mbili mbili ili angalau wawe karibu na Familia zao

Mzee alikuwa anapenda sana kushadadia yale mambo ya kukomoa komoa tu
Mama ana hekalu Mbweni hapo jirani na chuo cha wavaa suti na miwani meusi
 
Nauliza tu maana Dodoma wamebakia akina mzee Mgaya na mzee Ndugai wengine wote wametimkia Dar es salaam kula sikukuu ya Eid El Fitr.

Ni kwamba Dodoma ni padogo au bado ni mashambani hakufai kusherehekea sikukuu zenye amsha amsha?!!

Eid Mubarak!
Kama sasha saa zote yupo dar tusijeona anafuta sheria ya dodoma kua mji mkuu. Kupokea hati mabalozi kaja dar kuhutubia wazee kaja dar utafikiri dodoma hakuna wazee😂😂. Ikiwa mabalozi wanafuatwa dar je wataona haja ya kuhamia dodoma? Au tufanye dar zaidi ya biashara ni mji wa mabalozi? ..sijui kama huo utaratibu upo 😂😂
 
Ni kwa sababu ya sheria iliyopitishwa lakini hakuna mfantakazi wa umma anapenda kuishi dodoma - tuwe wakweli kwenye hili.
 
Mkapa alikuwa na utaratibu huo kila mwisho wa Mwaka,
Hadi leo Mwinyi yupo Msasani, bora JK hata akitaka kurusha picha mtandaoni anasogeaga Msoga kupata picha za shamban anakwanyua Hindi kwny Mti huku ana mawani yake ya kibishoo na Travolta mguuni
Kumbe mwinyi kwao ni Msasani,halafu Hugo mkapa kweli alikuwa anenda huko kijijini Lupaso
 
Narudia tena na tena. Kuhamia Dodoma ni kosa la kinkakati. Na Dodoma ni moja ya yale Mwl JK Nyerere hata kama hakukiri hadharani, aliyo sema," Hatukuwa malaika sie yako tuliyo kosea." Na aliwashangaa viongozi walio muenzi kwa kuchukua mambo waliyo fanya makosa awamu ya kwanza na kuyaendeleza, eti kumuenzi, kaa!

DSM ndio roho ya uchumi wa Tanzania ilipo, khalafu unaitelekeza. Uache majumba yaliyo tayari yakiishi mijuzi ukuta na popo. Uchukue kodi ukazitupe Dodoma kujenga majumba na miuondo msingi mingine huku ukiacha iliyo kuwa tayari na ikitumika ya DSM.

Angalau kuapishwa kwa wateuliwa hawa wa mikoa kutafanyika DSM pengine Mama Rais SSH atajiongeza na kuachana na zimwi Idodomiya.
 
Sio viongozi tu, hata wasaidizi wa viongozi wanalalamika sana kuishi Dodoma.
Kama hawataki waache kazi dom mbona pako poa pametulia sio Kama dar vurugu daily saa kumi upo Barabarani kuwai folen kwenda ofisin , unatoka Saa 9 kazi nyumbani unafika saa tatu usiku,
 
Nauliza tu maana Dodoma wamebakia akina mzee Mgaya na mzee Ndugai wengine wote wametimkia Dar es salaam kula sikukuu ya Eid El Fitr.

Ni kwamba Dodoma ni padogo au bado ni mashambani hakufai kusherehekea sikukuu zenye amsha amsha?!!

Eid Mubarak!
Kwani sikukuu wanakula kuofisi au kifamilia?
 
Ili waendelee kutubebesha walipa kodi mzigo usiotuhusu. Gharama za kusafiria kutoka Dodoma kuja Dar na kurudi Dom zinabebwa na walipa kodi
Nauliza tu maana Dodoma wamebakia akina mzee Mgaya na mzee Ndugai wengine wote wametimkia Dar es salaam kula sikukuu ya Eid El Fitr.

Ni kwamba Dodoma ni padogo au bado ni mashambani hakufai kusherehekea sikukuu zenye amsha amsha?!!

Eid Mubarak!
 
Back
Top Bottom