Kwanini vitabu vya dini havijataja sayari zingine zaidi ya Dunia?

Kwanini vitabu vya dini havijataja sayari zingine zaidi ya Dunia?

Uko sahihi sana.

Dini ni tool ya kucontrol masses.
Period.

Ni mtu mjinga tu ndiye ana miaka 18+ na anaamini nyoka aliongea, mvua inaweza kunyesha dunia nzima na kuleta mafuriko dunia nzima kwa wakati mmoja au kwamba Kuna sehemu hewani inaitwa mbingu ambapo watu wataenda kunywa pombe mitoni na kuzagamua mabikira 70+ .

Hebu tuwe na akili kidogo, tuache kuact utoto wakati tumeshakuwa watu wazima.
Great mind zinawaza streight bila woga wala wasiwasi kwa vitu vya kuambiwa, tatizo tunaambiwa vitu vingi mno vya kututisha ili tukubali
 
Yawezekana hujasoma

Biblia imetaja dunia inaelea angani miaka mingi mno kabla hata ya sayansi

Biblia imetaja mzunguko wa maji kabla hata sayansi haijaelewa na kutaja

Biblia itaja umbo la dunia kabla ya sayansi

N.k.
 
Great mind zinawaza streight bila woga wala wasiwasi kwa vitu vya kuambiwa, tatizo tunaambiwa vitu vingi mno vya kututisha ili tukubali
Hakika.
Ni muda wa watu kuachana na hofu walizopandikizwa na wahubiri, mapadre, walezi na waimba injili toka utotoni.
Mara ohh.. utachomwa moto, utapata mabalaa, kulia na kusaga meno ..
Aiseeh ..
 
Quran sijui Ila Biblia inahusu Dunia maana ndio ilizingua. Kuna sayari nyingi tena zrnye viumbe wema zaidi ya decilion mara decilion
Wewe ili useme jambo hili ni jema au baya unaangalia nini? Ulijuaje? Ndo maana neno **** kwa kiswahili ni tusi ila
Kuna mahali halina
Maana yyte. Hao waliokuambia mema na mabaya ndo mastermind wa dunia sasa ili waweze kukucontrol
 
Na wewe unauhakika gani hizo sayari zipo km sayansi inadanganya?

Km tu umbo la dunia ni debate mpaka leo

Baharini binadamu hajaifikia kuijua hata theruthi moja?

Mabara tu hajamaliza uchunguzi kagoogle bara la aktic

Vya hewani sayansi itaviweza?
Nimerudia kuangalia ID yako mara mbili mbili, umeandika kama FaizaFoxy
 
Dini zimekuwa sehemu muhimu ya maisha ya binadamu kwa maelfu ya miaka, zikitoa mwongozo wa kimaadili na kiroho. Hata hivyo, kuna hoja mbalimbali zinazotumiwa kuonyesha kwamba dini ni utapeli. Moja ya hoja hizi ni kwanini vitabu vya dini havijataja sayari nyingine zaidi ya Dunia.

Vitabu vya dini, kama vile Biblia, Quran, na vingine, vimeandikwa na watu wa zamani ambao walikuwa na uelewa mdogo sana wa sayansi na anga za mbali. Wakati wa kuandikwa kwa vitabu hivi, sayari nyingine hazikujulikana na hazikuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya watu. Hii inaonyesha kwamba vitabu hivi vilikuwa ni tafakuri ya maarifa na imani za watu wa wakati huo, badala ya kuwa na ufunuo wa kweli kutoka kwa nguvu za juu zinazodaiwa kuwa na maarifa yote.

Zaidi ya hayo, ukweli kwamba vitabu vya dini havijataja sayari nyingine unazua maswali kuhusu uhalali wa madai yao ya kiroho na kiufunuo. Kama kweli vitabu hivi vilikuwa vimeandikwa kwa mwongozo wa nguvu za juu, ni kwa nini hazikuweka maarifa ya msingi kuhusu ulimwengu unaotuzunguka? Hii inaongeza wasiwasi kwamba dini zinaweza kuwa zimeundwa ili kudhibiti na kuongoza jamii, badala ya kutoa maarifa ya kweli na sahihi.

Kwa mtazamo wa kisayansi, maendeleo mengi yamefanywa tangu wakati wa kuandikwa kwa vitabu vya dini. Sayari kama Mars, Jupiter, na Saturn zimegunduliwa, na tumeweza hata kutuma vyombo vya anga kwenye baadhi ya sayari hizi. Hii inaonyesha kwamba maarifa ya kisayansi yanabadilika na kupanuka, wakati maarifa ya kidini yamebaki kuwa yale yale kwa maelfu ya miaka.

Hitimisho ni kwamba, hoja ya kwanini vitabu vya dini havijataja sayari nyingine zaidi ya Dunia inaweza kuonekana kama ushahidi kwamba dini ni utapeli. Inaonyesha kwamba vitabu hivi ni bidhaa za maarifa ya wakati wao, na si ufunuo wa kweli kutoka kwa nguvu za juu zinazodaiwa kuwa na maarifa yote.
Kwa kujua juu ya sayari nyingine, kumekufanya ukaishi huko? Sayansi imezigundua, mbona hatuoni faida zake?
 
Wewe ili useme jambo hili ni jema au baya unaangalia nini? Ulijuaje? Ndo maana neno **** kwa kiswahili ni tusi ila
Kuna mahali halina
Maana yyte. Hao waliokuambia mema na mabaya ndo mastermind wa dunia sasa ili waweze kukucontrol
Maneno yako hayana uhusiano na mchango wangu.
 
Hakuna mtu anaweza kukujibu hilo, Ulimwengu wote unakadiriwa kuwa na galaxies zaidi ya bilioni 200, galaxy yetu pekee ya Milk way inakadiriwa kuwa na sayari zaidi ya bilioni 100.
Kuna msemo Mmoja huwa naupenda sana kuutolea Mfano...

The Eyes can not see What the Mind is Not!

kama Ubongo wako Haujui kitu hata ukuonyeshwa huwezi kujua Ni nini hicho...

Katika Karne hizo hakuna mtu aliyekuwa anajua kuwa Kuna sayari nyingine na ndo maana maandiko yote yalideal na Dunia peke yake..

Hakuna mtu atakuonyesha Any proof kutoka katika Biblia Uwepo wa sayari zingine..

Kuna sayari zaidi ya 1Mil + na galaxy zaidi ya 500 na kila galaxy ina Star system yake..

So Unafikiri kwanini Galileo aliuliwa na Kanisa na kupewa Adhabu??

Baada ya kusema Dunia Inazunguka Jua Kinyume cha Biblia..
 
Na wewe unauhakika gani hizo sayari zipo km sayansi inadanganya?

Km tu umbo la dunia ni debate mpaka leo

Baharini binadamu hajaifikia kuijua hata theruthi moja?

Mabara tu hajamaliza uchunguzi kagoogle bara la aktic

Vya hewani sayansi itaviweza?
Really ?

Unajua kitu kinaitwa Telescope ? Au maana ya Sayari ?
 
Back
Top Bottom