Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Ni wazi kuwa Rais wa awamu ya 6, Dkt Samia Suluhu Hassan, ameondoa zuio haramu za kufanyika shughuli za kisiasa za vyama vya upinzani na hivyo kurejesha ukuaji wa kidemokrasia Kwa vyama vya upinzan hapa nchini, ambao ulikuwa umeminywa Kwa kiasi kikubwa Kwa zaidi ya miaka 6 ya utawala wa awamu ya 5 ya Mwendazake.
Lakini jambo la ajabu ninaloliona ni Kwa vyombo vya habari nchini, kuendelea kutoa taarifa za vyama vya kisiasa vya upinzani Kwa "machale" makubwa.
Inafahamika pia kuwa vyombo vya habari ni Mhimili wa 4 wa Dola, usio rasmi.
Tunajua pia kuwa vyombo vya habari kama vile luninga ya TBC na gazeti la Habari Leo, ni vyombo vya umma, vinavyoendeshwa kwa kodi zetu wananchi wa vyama vyote vya siasa, iwe ni CCM au CHADEMA, kwa hiyo vinapaswa vilipiti Kwa usawa habari za vyama vya siasa, bila kufanya upendeleo.
Vinapaswa vyombo vya habari hapa nchini visiwe "biased" wakati wa kuripoti taarifa zao,ziwe za CCM au Chadema, viripoti sawa.
Lakini sivyo vinavyofanya hivi Sasa, kwani mfano TBC inaendeleza mapambio yake ya "kumsifu na kumwabudu" Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan.
Vinapaswa vyombo vya habari hapa nchini, viige mfano wa nchi jirani ya Kenya, namna vinavyoripoti taarifa ya vyama vya kisiasa nchini mwao bila upendeleo.
Tulijionea wakati wa uchaguzi Mkuu uliopita wa Kenya namna vyombo vya habari vya nchi hiyo vilivyokuwa huru, wakiripoti mubashara, shughuli za kisiasa, ziwe za chama tawala au vyama vya upinzani.
Utashangas hapa nchini kwetu, Kwa tukio dogo kabisa linalofanywa na Mwenyekiti wa CCM, Samia Suluhu Hassan inarushwa mubashara na luninga ya Taifa, wakati hotuba ya viongozi wa kitaifa wakihitubia, hawaonyeshi mubashara!
Kama kweli Taifa letu linataka kukuza Demokrasia nchini, basi vyombo vya habari nchini, vinapaswa vibadilike katika utendaji wake.
Kwani LAZIMA vifahamu kuwa enzi zile za kutishiwa kufungiwa, kama vilivyokuwa vikifanyiwa na utawala wa awamu ya 5, hadi kutishwa kuwa "you don't have that freedom to that extent" umeshapitwa na wakati.
Mungu ibariki Tanzania