Kuripoti kwa weledi kutoka kwa hawa wanahabari wetu, usahau.
Mara nne kampuni yetu imewahi kutembelewa na viongozi wa Serikali. Wanapokuja wanatanguzana na waandishi wa habari waliowalipa. Baada ya kikao, mara zote, nikaja kuambiwa na maofisa wangu kuwa waandishi wa habari wamesema wanaomba milioni 1 wakati mwingine milioni mbili, eti ili waka-report huo mkutano wa viongpzi wa Serikali walipotembelea kampuni.
Mara zote mimi nilikataa, lakini wenzangu waliniambia kuwa ndiyo utaratibu ulipzoeleka. Ndiyo maana utakuta Waziri au mkuu wa mmoa, hata akifanya tukio dogo saa 8 usiku, lazima mwanahabari atakuwepo, na hasa kama tukio hilo litampandisha kuobekana ni mchapa kazi. Wanadai kuwa hata marehemu akuwa Waziri wa Ujenzi alitumia sana technique hiyo. Anaenda kwenye mradi wa ujenzi wa daraja saa 7 usiku, lakini mwanahabari yupo. Anatoa karipio kali huo usiku, na ilimpandisha sana mbele ya wananchi. Na aluzidisha zaidi baada ya kuwa Rais.
Hivyo kama vyama vya upinzani vinataka habari zake zitangazwe sawa na zile za CCM, labda wafanye yale ambayo CCM huwa wanafanya. Hata ndani ya Serikali au CCM, wale ambao hawatoi chochote kwa wanahabari, hata kama wanachapa kazi kiasi gani, habari zao hazitangazwi sana.
Huko Kanda ya Ziwa mpaka kuna kampuni ya habari za Waziri iliyojificha kwa jina la mtu mwingine lakini lengo la kampuni hiyo binafsi ya habari, ni kum-promote na kumpamba huyo Waziri ili aonekane ni mchapa kazi kwelikweli.