Mleta mada umepotosha pakubwa na kuna kitu huenda huelewi.
Mimi nimefika Moshi na kuzunguka maeneo tofauti ya mkoa wa Kilimanjaro ili kuona hali ya maendeleo, mapungufu nk.
Binafsi sio mchaga na siwakubali kabisa wachaga (kwa sababu ya majigambo yao na sifa zao za kijinga) lakini kuna vitu jamii zingine inabidi zikajifunze kwa wachaga. Haya ni kwa uchache niliyoyakuta Moshi na Kilimanjaro.
1. Moshi ni mji mdogo lakini wenye ustaarabu mkubwa wa kimaendeleo katika mazingira ya miji ya jamii za kiafrika. Huduma zote muhimu za kijamii na miundo mbinu yote muhimu imekuwepo kwa miaka mingi. Hawa jamaa ama walipendelewa au walijipendelea.
2. Population yake ni ndogo, shughuli zake ni chache za hapa na pale, hivyo ningeshangaa kukuta utiriri wa majengo mengi makubwa, marefu na kisasa katikati ya mji. Ya kazi gani? Urembo? Kwa mfano jengo kubwa pale la NSSF, tangu lijengwe zaidi ya miaka kumi, nilielezwa halijawahi kupata wapangaji hata nusu.
3. Kiwango cha maisha ya wakazi wa Moshi na ubora wa makazi wa wananchi wa kawaida wa Moshi na Kilimanjaro uko juu zaidi ikiwa utawalinganisha na watanzania wengi wa mikoa mingine.
4. Idadi ya wachaga ni ndogo mnoo ukilinganisha na idadi ya watanzania wote. Hao jamaa nadhani hawafikii hata 2% ya watanzania wote, lakini ndio jamii iliyotapakaa maeneo mengi zaidi ndani na nje ya Tanzania huku ikiwa na maendeleo bora ya mfano.