kwanini Waethiopia wanaongoza kwa kukimbia nchi yao ili kuishi ukimbizini?

kwanini Waethiopia wanaongoza kwa kukimbia nchi yao ili kuishi ukimbizini?

Kenya nimeishi na ninaenda mara kwa mara maisha ya Kenya ni magumu kupata pesa ni kugumu na matumizi muhimu hasa ya chakula ni gharama sana usidanganywe

Sio kweli mzee maisha ya watu binafsi ni magumu na pia kazi kupeana ni kwa ukabila
Kupata Pesa Kenya ni rahisi kuliko Tanzania.
Kila nchi duniani ina kundi la watu wanaopitia maisha magumu utofauti huwa ni katika asilimia, watu wenye maisha magumu zaidi Kenye ni 16%, watu wenye maisha magumu zaidi Tanzania ni 26%.
Chakula kuwa rahisi haimaanishi maisha ni rahisi. Watanzania wengi masikini wanakula makande yenye maharage ya kuhesabu, makande ya masikini Kenya yana maharage au karanga za kutosha.
 
Hivi ulishawahi kufika huko Kasulu vijijini, Vijiji vya Kondoa,Kongwa, Mpwawa, Manyovu, Singida? Au wewe unaangalia tu TV?
Kenya sehemu ambayo kuna shida na maisha magumu ni Turkana pekee...sehemu zingine maisha yao yameboreka kuliko Tanzania kwasababu upatikani wa pesa ni rahisi sana lakini pia dhamani ya pesa yao bado inawabeba.
Fikiria bado unaweza kupata chakula kwa ksh 10
Hawa wanaosema hivyo huenda hata hawajawahi kufika mkuu Yani kiufupi tz kuna raha sio tu afadhali
 
Wanakimbilia nchi za nje sababu wanapenda maisha yale expensive kama anavyo sema Mwijaku expensive life 😄
 
Kenya nimeishi na ninaenda mara kwa mara maisha ya Kenya ni magumu kupata pesa ni kugumu na matumizi muhimu hasa ya chakula ni gharama sana usidanganywe

Sio kweli mzee maisha ya watu binafsi ni magumu na pia kazi kupeana ni kwa ukabila
Hata World Bank walitupa pesa za TASAF za kusaidia kaya masikini kwa sababu ya Ufukara uliotopea.
 
Hii ni ETHIOPIA, wanaongoza kwa kupata treni ya kisasa mapema, ndege nyingi, barabara za juu kwa juu, nk ktk Africa Mashariki.

Lakini najiuliza kwanini Waethiopia wanaongoza kwa kukimbia nchi yao ili kuishi Ukimbizini Ilhali Ethiopia hakuna VITA? naomba majibu?

View attachment 3054635
View attachment 3054640
View attachment 3054643
View attachment 3054644
View attachment 3054645
Pamoja na kwamba maisha magumu yanachangia ila kuna mataifa raia wake hawaridhiki haraka kama bongo. Wanapambana kwenda nje kwa lengo la kupata maisha bora zaidi na ikiwezekana wapate uraia wa huko.
Shida ya waethiopia wanapenda kupitia njia za panya ndo maana wanaonekana kama wanakimbia nchi yao.

Kuna nchi kama Nigeria, Kenya, SA na nchi nyingi za Kaskazini mwa Afrika wanaongoza kwenda nje na wengi wamefanikiwa kupata uraia huko. Ndo maana wasanii wa Nigeria wakienda Ulaya na USA shows zao wanapata watu wengi kutokana na kwamba kuna raia wengi huko kutoka nchi zao.

Watanzania nahisi na kutokufahamu sana Lugha za kigeni kunachangia watu kutoenda nje tunabaki tunajifariji kwamba tuna maisha mazuri kushinda wenzetu ndo maana hatipambanii kwenda nje ya nchi. Kitu ambacho ni uongo mtupu hata hao tunaowaita wakimbizi wa Ethiopia unakuta maisha wanayoishi kwenye nchi zao ni mazuri zaidi ya watanzania wengi tunaojidai tuna maisha mazuri
 
Hivi ulishawahi kufika huko Kasulu vijijini, Vijiji vya Kondoa,Kongwa, Mpwawa, Manyovu, Singida? Au wewe unaangalia tu TV?
Kenya sehemu ambayo kuna shida na maisha magumu ni Turkana pekee...sehemu zingine maisha yao yameboreka kuliko Tanzania kwasababu upatikani wa pesa ni rahisi sana lakini pia dhamani ya pesa yao bado inawabeba.
Fikiria bado unaweza kupata chakula kwa ksh 10
Hapo Dodoma tu makao makuu kuna sehemu za vijijini zinatisha kwa umaskini
 
Pamoja na kwamba maisha magumu yanachangia ila kuna mataifa raia wake hawaridhiki haraka kama bongo. Wanapambana kwenda nje kwa lengo la kupata maisha bora zaidi na ikiwezekana wapate uraia wa huko.
Shida ya waethiopia wanapenda kupitia njia za panya ndo maana wanaonekana kama wanakimbia nchi yao.

Kuna nchi kama Nigeria, Kenya, SA na nchi nyingi za Kaskazini mwa Afrika wanaongoza kwenda nje na wengi wamefanikiwa kupata uraia huko. Ndo maana wasanii wa Nigeria wakienda Ulaya na USA shows zao wanapata watu wengi kutokana na kwamba kuna raia wengi huko kutoka nchi zao.

Watanzania nahisi na kutokufahamu sana Lugha za kigeni kunachangia watu kutoenda nje tunabaki tunajifariji kwamba tuna maisha mazuri kushinda wenzetu ndo maana hatipambanii kwenda nje ya nchi. Kitu ambacho ni uongo mtupu hata hao tunaowaita wakimbizi wa Ethiopia unakuta maisha wanayoishi kwenye nchi zao ni mazuri zaidi ya watanzania wengi tunaojidai tuna maisha mazuri
Sahihi
 
Ethiopia hakuna vita mkuu hata vyombo vya habari husikilizi Kuna ukanda huko wanakinukisha Kila siku na Kuna njaa hatari
 
Hawa wanaosema hivyo huenda hata hawajawahi kufika mkuu Yani kiufupi tz kuna raha sio tu afadhali
Kwa upande wangu huu huwa nauona kama upuuzi. Watanzania tunapenda kujifariji kwenye upuuzi ambao umeendelea kutudumaza. Ukweli ni kwamba Tanzania hatuna maisha ya kusema tunawazidi Kenya on average huo ni uongo na upuuzi uliopitiliza.
Mfano mzuri angalia bajeti ya kenya na bajeti ya Tanzania mwaka huu na ulinganishe na Idadi wa watu.

Watanzania tuache upuuzi wa kuwa tunajifariji kwenye ujinga, sisi ni maskini wa kutupwa bado.
 
Biggest slums kubwa katika hii dunia ziko India, Mexico na South Africa. Slums za India na Mexico ni kubwa zaidi duniani lakini hiyo haimaanishi tumeendelea kuzidi hizo nchi.

Kaunti nyingi za Kenya zina maendeleo kuliko Tanzania, majiji ya Kenya ya Nairobi, Mombasa, Kisumu ni makubwa kuliko yote ya Tanzania kwa pamoja. Kuna kaunti nyingi Kenya ambazo hata hawaiti majiji ili ni kubwa kuliko Mbeya na Tanga.
Mzee hebu acha kutufananisha na wakenya. Unatuaibisha watanzania.
Huwezi kukuta watanzania wanaishi hivi: 👇 👇 👇 🤣 🤣 🤣 Uwe na Adabu na Tanzania Labda wewe ni Mkenya na tabia zenu za bragging 🤣🤣🤣🤣

1722156243692.png

1722156287301.png

1722156332639.png
 
Back
Top Bottom