Kwanini wafanyabiashara wakubwa wakutane na Rais Ikulu badala ya Waziri husika Wizarani?

Kwanini wafanyabiashara wakubwa wakutane na Rais Ikulu badala ya Waziri husika Wizarani?

Acheni chuki zenu kwa mama. Mbona Magufuli alipokutana na Dangote ikulu hamkutia neno?
Inatakiwa kuwa ni kwenye dharura tu, ndio Raisi inakuwa vizuri kukutana na wafanya biashara au moja kwenye suala muhimu.
 
Wakati ikulu ilikuwa inatumika kwa ajili ya vikao vya chama mlikuwa wapi. Tunaomba msitupangie. Mpo wengi sana lakini juhudi zenu ongezeni kiduchu angalau hata msikike kitaa maana mmechoka hamjaanza hata kazi mliyotumwa
 
Walichofanywa wafanyabiashara wa tz hii miaka 5 ya muovu hata wana hamu tena? Wanahitaji muda wajipange upya, maana muovu aliwafanya kitu mbaya sana, wengi iliwapasa hata kuuza assets zao na kukimbia nchi yao. Yupo wapi Manji leo hii? Mtz aliyeajiri maelfu ya watz, muovu kwa mabifu yake ya kishamba akamsambaratisha
Manji yupi? Unazungumzia ajira zipi? KUna wakati munasema mambo kama kijana wa kijiweni tu! Mtu unatumia maneno ya jumla jumla yasiyopimika. Aliajili maelfu, watu wengi, .... Ajira za kulipwa laki moja yeye akitengeneza mabilioni na kujenga Canada! Hapa wanavuna mitaji na kujiondokea.
 
Ulikuwa na mawazo sawa na haya wakati Magu akikutana na akina Rostam au hata huyo Dangote hapo Ikulu?!

Unaweza kueleza hapa utofauti wa Dangote aliyekuwa amekutana na Magu na Dangote aliyekutana na SSH ili tuamini Dangote huyu anayekutana na SSH ni mwando tu wa kuturudisha kwenye uchuuzi lakini Dangote yule wa Magu alikuwa ni wa kutupeleka kwenye industrial nation!

View attachment 1797748

Hapo juu ni Mwenyekiti wa Bharti Enterrprise!!

Haya sasa... tofauti ya ukutanaji huu wa sasa ni ipi ukilinganisha na ule wa zamani hadi uone huu wa sasa unataka kuturudisha kwenye uchuuzi?!
Mimi nikisoma kilichoandikwa kinawahusu viongozi wote wa CCM. Wewe unaona kama anazungumziwa Samia pekee. Hayo ni mahaba ya aina gani sasa. Hawa ni wote!!!! Hatufiki kokote kwa dili za kupitia ikulu. Akilalamika mmoja rais anaagiza sheria iangaliwe.
 
Manji yupi? Unazungumzia ajira zipi? KUna wakati munasema mambo kama kijana wa kijiweni tu! Mtu unatumia maneno ya jumla jumla yasiyopimika. Aliajili maelfu, watu wengi, .... Ajira za kulipwa laki moja yeye akitengeneza mabilioni na kujenga Canada! Hapa wanavuna mitaji na kujiondokea.

Kwani kuna tofauti gani na aliyejenga uwanja wa ndege huko porini wa 39b, ambao hauna mahitaji?
 
Umenena vema.

Wengi wanaendekeza maneno yenye upuuzi mwingi. Hawapendi kujishughulisha na kufahamu mambo ya msingi.

Mataifa makubwa, yenye pesa na teknolojia, kila siku yanahangaika kutafuta wawekezaji. China inatafuta wawekezaji. Saudia mpaka wana ofisi Marekani kwaajili ya kutafuta wawekezaji, lakini mtu mmoja ambaye amejaza watoto si chini ya watano nyumbani pake, hajiulizi hao watoto wake wakifikia umri wa kufanya kazi, wataajiriwa wapi?

Baadhi ya wanasiasa wetu wanatudanganya kuwa watu wajiajiri lakini utajiajiri kwa mtaji upi, kwa uzoefu upi, kwa teknolojia ipi, kwa kulenga soko lipi? Kijana anahitajika aajiriwe, akusanye mtaji, apate uzoefu, atengeneze connections, ndiyo anaweza kufikiria kuanzisha kitega uchumi chake chenye faida. Kujiajiri kwa kukaanga chips na mihogo, hakuwezi kuibadilisha nchi.
 
Kuna watu wanauelewa mdogo acha nao. Hawajui concept ya followers
 
Manji yupi? Unazungumzia ajira zipi? KUna wakati munasema mambo kama kijana wa kijiweni tu! Mtu unatumia maneno ya jumla jumla yasiyopimika. Aliajili maelfu, watu wengi, .... Ajira za kulipwa laki moja yeye akitengeneza mabilioni na kujenga Canada! Hapa wanavuna mitaji na kujiondokea.
Munasema ndio nini? Sukuma gang detected
 
Hizi hoja nyingine kuhusu Rais Samia ni za ovyo sana! Yaani Rais kuzungumza na wafanyabiashara na kuwahakikishia usalama wa mitaji yao ni kosa? Kwani kuna mkataba kasaini Rais hapo Ikulu? Halafu mleta hoja ujue Rais ni taasisi ana hadi washauri wa masuala ya uchumi. Hebu tujadili mambo kwa kuonyesha hili ni jukwaa la great thinkers.
 
Acha apewe chochote atakacho, kuliko kutawaliwa na yule dhalimu aliyeko ahera.
Maneno ya aina hii huwa yananipa picha kwamba kuna watu munatafuta raha ya maisha ambayo haipo dunia hii. Na munachukia viongozi kwa manufaa binafsi tu! Tunapojadili suala la kitaifa huwezi fikia hatua ya kuruhusu rais awe mwizi wakati jamii ya dunia hii, wizi unakubalika kwa watu wapuuzi tu. Hata kama alimnyonga mzazi wako, ifikie kiwango ujiulize kama mzazi alikuwa mtu wa maana kiasi gani.
 
Msitegemee Rais afanye kila kitu, kama kuna shida kwenye kilimo mbona kuna waziri wa kilimo.
Rais anaingilia tu pale wasaidizi wake wanapopata kigugumizi, Kwa mfano kiwanda cha Dangote kilikuwa na matatizo ndio maana aliingilia kati!
Ukiulizwa matatizo gani hata huyajui, ile unaona alikuwa na matatizo, Yapi???? Taja ni yapi?
Hicho siyo kiwanda cha kwanza nchini. Wapo akina Twiga Cement inayomilikiwa na makampuni makubwa kuliko hata Dangote amabaye ni mtu binafsi tu!
 
Maneno ya aina hii huwa yananipa picha kwamba kuna watu munatafuta raha ya maisha ambayo haipo dunia hii. Na munachukia viongozi kwa manufaa binafsi tu! Tunapojadili suala la kitaifa huwezi fikia hatua ya kuruhusu rais awe mwizi wakati jamii ya dunia hii, wizi unakubalika kwa watu wapuuzi tu. Hata kama alimnyonga mzazi wako, ifikie kiwango ujiulize kama mzazi alikuwa mtu wa maana kiasi gani.

Hao aliowauwa, kuwabambikizia kesi, kuwaacha na vilema, walikuwa ni kikwazo gani cha kutekeleza hayo aliyotaka? Na baada ya kufanya huo udhalimu, what so special ameachive kwa sababu ya kufanya huo udhalimu? Acha akae mwingine mwenye utu atakayekubaliana na changamoto za uongozi, na sio mtu kuongoza kwa kuendekeza mapungufu yake binafsi. Nchi hii ina miaka mingi, na maendeleo ni mchakato ambao hata angeua wote walio kinyume na yeye, bado asingeifanya iwe ya dunia ya kwanza. Nasema hivi, bora rais mwizi anayekubali kukosolewa, kuliko jizi lisilokubali kukosolewa wala kuhojiwa fullstop.
 
Mbona kipindi kile akina Rostam wameenda kuonana na ile maiti ya chato hamkuyasema haya

Mwacheni mama aipeleke nchi mahala salama kutoka kwenye ile diversion aliyokuwa anatupeleka bwana Mayanga/majanga
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]🥱🥱🥱🥱🥱
 
Sisi tunanyamaza maana tukisema tunaitwa sukuma gangkwa sasa praise team wamebaki wa Msoga na ndugu zao Chadema,ndo kutwa na mapambio Daah nchi hii mmmhh
Binafsi nimesha hitimisha kwamba kuna Chaga tribalists wanaoaamini this time watakula raha waliyoanza nayo miaka ya 70.
 
Back
Top Bottom