Kwanini wafanyabiashara wakubwa wakutane na Rais Ikulu badala ya Waziri husika Wizarani?

Kwanini wafanyabiashara wakubwa wakutane na Rais Ikulu badala ya Waziri husika Wizarani?

Watu wengi bado tunaishi maisha ya KIJIMA sana aise; hivi bado kuna mtu hajui faida za wawekezaji katika nchi? Magufuli mwenyewe ali straggle sana kuwapata wawekezaji, sema matendo yake yalikua yanawafukuza; tunajua Dangote alitaka kufunga kiwanda chake, aliitwa na Magufuli Ikulu wakayamaliza but bado ni kama uzalishaji wake ulikua unasua sua, kaongea na watu wa Barrick baada ya yeye mwenyewe kuwachanganya, kina Rostam Aziz hadi waliondoka nao nchini but he called them back, kafanya sana vikao na wafanyabiasha wa ndani na wa nje but huenda wawekezaji/wafanya biashara walikua wanaona maneno yake na matendo yake vilikua vinapingana na waka decide otherwise.
Moja kati ya faida za wawekezaji ni AJIRA kwa Watanzania, tumelalamika ugumu wa ajira kipindi cha mwendazake, unajua sababu kubwa ni nini? Serikali haina uwezo wa kuajiri wataalamu wote, wengine wataajiriwa sekta binafsi, ndio hao wawekezaji au wafanyabiashara.
Faida ya pili ndio hiyo mambo ya kodi na dividends kwenda serikalini, ukiwaondoa wafanyabiashara hayo mengine yatatokea and hence hata hizo kodi tunazo sema zimefikia Tilion zita drop na ujambazi/wizi unaweza kuongeza. Tuache mawazo ya KIJIMA, tufikirie kisasa, duniani kote serikali zinatengeneza mazingira mazuri kwa wafanyabiashara/wawekezaji, halafu sisi na mawazo yetu ya KIJIMA tunawaona kama wanyonyaji, stupid
 
Hao aliowauwa, kuwabambikizia kesi, kuwaacha na vilema, walikuwa ni kikwazo gani cha kutekeleza hayo aliyotaka? Na baada ya kufanya huo udhalimu, what so special ameachive kwa sababu ya kufanya huo udhalimu? Acha akae mwingine mwenye utu atakayekubaliana na changamoto za uongozi, na sio mtu kuongoza kwa kuendekeza mapungufu yake binafsi. Nchi hii ina miaka mingi, na maendeleo ni mchakato ambao hata angeua wote walio kinyume na yeye, bado asingeifanya iwe ya dunia ya kwanza. Nasema hivi, bora rais mwizi anayekubali kukosolewa, kuliko jizi lisilokubali kukosolewa wala kuhojiwa fullstop.
Bado hujaandika kitu. Unaandika mambo ya jumla sana! Hao akina nani? JF ya enzi zetu ilikuwa ya kutoa ushahidi siyo mambo ya kijiweni na majukwaa ya Lissu. Be specific! na huenda utasema Lissu wakati unaelewa Absalom Kibanda alitolewa jicho enzi ya Kikwete, Ulimboka aling'olewa meno enzi ya Kikwete. Tena PM akasema wapigwe tu!

Una matatizo mengi kichwani usiyoweza kuyaeleza kwa ufasaha.
 
Watu wengi bado tunaishi maisha ya KIJIMA sana aise; hivi bado kuna mtu hajui faida za wawekezaji katika nchi? Magufuli mwenyewe ali straggle sana kuwapata wawekezaji, sema matendo yake yalikua yanawafukuza; tunajua Dangote alitaka kufunga kiwanda chake, aliitwa na Magufuli Ikulu wakayamaliza but bado ni kama uzalishaji wake ulikua unasua sua, kaongea na watu wa Barrick baada ya yeye mwenyewe kuwachanganya, kina Rostam Aziz hadi waliondoka nao nchini but he called them back, kafanya sana vikao na wafanyabiasha wa ndani na wa nje but huenda wawekezaji/wafanya biashara walikua wanaona maneno yake na matendo yake vilikua vinapingana na waka decide otherwise.
Moja kati ya faida za wawekezaji ni AJIRA kwa Watanzania, tumelalamika ugumu wa ajira kipindi cha mwendazake, unajua sababu kubwa ni nini? Serikali haina uwezo wa kuajiri wataalamu wote, wengine wataajiriwa sekta binafsi, ndio hao wawekezaji au wafanyabiashara.
Faida ya pili ndio hiyo mambo ya kodi na dividends kwenda serikalini, ukiwaondoa wafanyabiashara hayo mengine yatatokea and hence hata hizo kodi tunazo sema zimefikia Tilion zita drop na ujambazi/wizi unaweza kuongeza. Tuache mawazo ya KIJIMA, tufikirie kisasa, duniani kote serikali zinatengeneza mazingira mazuri kwa wafanyabiashara/wawekezaji, halafu sisi na mawazo yetu ya KIJIMA tunawaona kama wanyonyaji, stupid
Dah! Kwa uandikaji wa aina hii!!! Una elimu gani Boss? Nawe unategemea kufaidika na Dangote?
 
Sisi tunanyamaza maana tukisema tunaitwa sukuma gangkwa sasa praise team wamebaki wa Msoga na ndugu zao Chadema,ndo kutwa na mapambio Daah nchi hii mmmhh
Kwani wewe sio sukuma gang mkuu?
 
Mkuu umeongea. Nililiona hili jambo nalitamani kuliwasilisha in the coming articlea. Me sioni dhana ya Rais kuwa main speaker.. Ila in Africa, Everything is possible
 
Dah! Kwa uandikaji wa aina hii!!! Una elimu gani Boss? Nawe unategemea kufaidika na Dangote?
Nimeishia darasa la hapa na pale but that doesnt mean kwamba sijui faida za uwekezaji. Hivi hujui baada ya Dangote kuanza uzalishaji bei ya cement nchini ilishuka? Dangote aliwapa sana changamoto wazalishaji wengine; ngoja nikupe hi nyingine; Cement ya Tanzania kwa sehemu kubwa iliokua inapatikana sokoni ilikua ile ya class 32.5, Dangote akawa anamwaga mzigo wa class 42.5 kwa bei chee, ndio sasa na kina Simba, Twiga nao ikabidi waji align na soko, zikaanza hizo sijui twiga plus, mara twiga extra nk. Bado utananmbia, Dangote hana faida?
 
Sawa!
Somo la kwanza: Kwani hujui kwamba msimu wa mvua bei ya viazi hupungua? Au, nayo kuna Dangote wa viazi?
 
Hivi wale waliojipanga barabarani na kumlilia Mwenda Zake hata kufikia kuvunja geti ya JKN airoort walikua wanaonyesha picha gani?walikua wanamlikia dikteta,katili,mlafi,mwizi ???NO NO NO tena HAPANA
Walilia wakijua sasa lile JABALI lao limeanguka.
Walilia wakijua sasa ile NGUZO KUU iliyoshikilia nyumba yao Tanzania sasa imeanguka.
Na kilio chao hakitakua bure waka machozi yao hayatakua machozivya samaki.Nitakukumbuka Magufuli Daima maana ulisimama na wanyonge nabkutaka kutuinua.
Ni ajabu sana wapo wanaokubeza na kukushutumu.Waliokua wanatunyonya,waliokua wanapiga dili,wazee wa mikataba feki,walitaka kuona wanyonge wa nchi hii wanatupwa ktk dampo tusahaulike.
Historia itawahukumu.
 
Mfanyabiashara wa chini hukutana na kuzungumza na waliochini, mfanyabiashara mkubwa huzungumza na wakubwa. Hata kanisani muumini maskini akifa huzikwa na mzee wa kanisa au katekista, lakini akifa tajiri huzikwa na askofu au maskofu.
PESA NDO MUNGU WA DUNIA HII, UMASKINI NDIYO DHAMBI KUBWA.
 
Ogopa sana Technolojia, mtoa mada kule juu ana matatizo sana. Ana imani za kishamba kuwa ili kupata uwekezaji, unatakiwa na sera za NGUNGULI, mambo ambayo yamepitwa na wakati. Hizi enzi ni za utandawazi, utajikuta unaogelea peke yako. Dunia hii ni ya uwekezaji(narudia uwekezaji na siyo uchuuzi)!
Falsafa za kichuuzi na kujitenga zimeonesha kushindwa, kifo cha mende!
Ask the Chinese.
 
Tunavutia wawekezaji lakini njia za kuwekeza na Sheria za uwekezaji haziko Ikulu.

Tunazo Wizara na ofisi zinazohusika. Kwa kuwa marais wetu wameamua kuwa ni waalikaji wa wawekezaji, nawaona Mawaziri na wahusika wengine wakikaa pembeni na kufanya kazi za sekretari, kukopi kumbukumbu za mikutano na ahadi za Rais. Hii haifai. Leo Dangote, kesho wawekezaji wa Ulaya, kesho wachina, wahindi, Wakenya, n.k. mpaka lini hali hii?

Sasa Ikulu ni ya wafanyabiashara, wakiitwa wawekezaji. Ni vigumu kwa mkulima mashuhuri kufika Ikulu. Rais hajakutana na kundi lolote la waajiliwa wake; iwe Jeshi, waalimu, idara ya afya, nk.

Imekuwa ni rahisi sana Dangote kufika Ikulu kujadili uwekezaji wa kiwanda kimoja tu. Kuna udhaifu gani unaotafutwa Ikulu? Ni kugawa shares za kiwanda kama tulivyowahi sikia?

Huu sasa umekuwa mtindo wa kudumu kwa marais wetu wa CCM.
Nyie maccm Kama Hamuna akili tuwasaidie vipi?
 
Watanzania wanaamini wafanya biashara ndo watawapeleka uchumi wa kati wa juu ila hawajui mfanyabiashara siku zote anaangalia faida tu si kitu kingine
wafanya biashara ndio injini ya uchumi wao hutoa mazao mashambani na kupeleka sokoni ndani na nje wao ndio wanajenga viwanda vy kusindika mazao ya wakulima,wao ndio huzitoa dola nje na kuzirudisha.Nadhani wewe ni mmoja ya watu wanao wachukia wafanya biashara bila kujua kua mfanyabiashara awe mdogo au mkubwa kitu cha kwanza anaangalia faida.
 
Back
Top Bottom