Tunavutia wawekezaji lakini njia za kuwekeza na Sheria za uwekezaji haziko Ikulu.
Tunazo Wizara na ofisi zinazohusika. Kwa kuwa marais wetu wameamua kuwa ni waalikaji wa wawekezaji, nawaona Mawaziri na wahusika wengine wakikaa pembeni na kufanya kazi za sekretari, kukopi kumbukumbu za mikutano na ahadi za Rais. Hii haifai. Leo Dangote, kesho wawekezaji wa Ulaya, kesho wachina, wahindi, Wakenya, n.k. mpaka lini hali hii?
Sasa Ikulu ni ya wafanyabiashara, wakiitwa wawekezaji. Ni vigumu kwa mkulima mashuhuri kufika Ikulu. Rais hajakutana na kundi lolote la waajiliwa wake; iwe Jeshi, waalimu, idara ya afya, nk.
Imekuwa ni rahisi sana Dangote kufika Ikulu kujadili uwekezaji wa kiwanda kimoja tu. Kuna udhaifu gani unaotafutwa Ikulu? Ni kugawa shares za kiwanda kama tulivyowahi sikia?
Huu sasa umekuwa mtindo wa kudumu kwa marais wetu wa CCM.
Raia wa kawaida angekutana na viunzi 1000 kisha anakata tamaa wakati ndiye mwenye-nchi ambaye biashara yake, kula kwake, kuuguzwa kwake, kusafiri kwake, kununua bidhaa kwake, kulima mazao ya chakula na na biashara ndio KODI endelevu inayoifanya serikali kuwa hai na kutanua misuli huku yenyewe ikijiimarisha kwenye fahamu kuu tano za kimamlaka ili kuendelea kutawala.
1. Kusikia lakini wanaweka pamba masikioni
2. Kuona lakini wanapuuzia kwakuwa wananchi inawezekana ni washamba
3. Kunusa hatari na usalama lakini wakipima hadhi ya mtendewa ambaye ndie mwenye-nchi
4. Kuhisi wanapendwa au kuchukiwa bila ushahidi halisia kutoka kwa wenye-nchi
5. Kugusa kwa uthubutu wa kuhakiki hatari au usalama na pengine kuogopa kugusa kisichogusika kwa hofu ya kupoteza uungwaji mkono na wenye-nchi
Raia akiwa na dukuduku ambalo limesababisha changamoto ya kukata tamaa na maisha baada ya kudhulumiwa au kukutana na viashiria vya rushwa ili tatizo lake litatuliwe anaambiwa aanzie kwa mjumbe, mwenyekiti mtaa/kitongoji/shehia, mtendaji, mkuu wa wilaya, DAS, DED, RAS, DC, RC, WZR nk bila mafanikio yoyote. Akiomba nafasi kuonana na kiongozi mwenye mamlaka ya juu wasaidizi wanampigisha kona za kimizengwe hadi anapoteza imani na kutelekelzaq azma yake.
Tajiri akionekana kwa hisia unanusa pafyumu lakini mlalahoi anahisiwa anawweza kuhatarisha usalama-maajabu sana!!!
*Kwa hiyo ni rahisi sana kwa NGAMIA kupenya kwenye tundu la SINDANO kuliko TAJIRI wa mali (sio tajiri wa akili, hekima, busara na maarifa) na SIFA za KUJIKWEZA.