Kwanini wafanyabiashara wakubwa wakutane na Rais Ikulu badala ya Waziri husika Wizarani?

Kwanini wafanyabiashara wakubwa wakutane na Rais Ikulu badala ya Waziri husika Wizarani?

Wasukuma eeehhh...[emoji16][emoji16][emoji16]ifike kipindi mkubaliane tu na hali kwamba mshapoteza...mlipewa nafasi mkawa mnapika ugali tu IKULU mkasahau raia[emoji440][emoji440]
 
Rais kukutana na Dangote ni inshara nzuri sana na kuna ujumbe ulikuwa unatumwa duniani kote.
 
Tatizo dangote ni mweusi mwenzetu ndio maana maneno yamekuwa mengi angekuwa mhindi au mzungu wala msingepiga hizi kelele za kujifanya mna uchungu sana na nchi.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Naona huna historia na nchi hii na viongozi wetu. Hukumbuki wazungu waliokuwa wanakuja hapa TZ na wengine kutoa hata zawadi ya suti kwa rais? Hukusikia tukipiga kelele? Huwezi kuwa investor unayetegemea support ya rais badala a mifumo ya nchi. Kama ni mifumo, hakuna sababu ya kuingia ikulu kila wakati.

Kama ni kutafuta 'dili' za mdomo basi aendelee na hata hizo ajira unazosema utapata ajira za kishenzi tu kama unavyoona madereva wake wakilalamikia kukosa mikataba kwa miaka na hakuna mtetezi.
 
Fuatilia changamoto anazopitia Dangote kwenye kiwanda chake cha saruji (cement) huko mtwara, kuna somo linaitwa mjasiriamali na yanayomzunguka 'the entrepreneur and his environment ' tumepitia kwenye sera zisizo tabirika (policy uncertainty) huwezi kupanga namna ya kukuza biashara kwa sera ambazo hazina muelekeo 'you can not plan business growth with policy uncertainty' wafanya biashara wengi waliumizwa na hicho kikosi chenu cha 'task force ' kazi ya ziada inahitajika kurudisha imani ya wawekezaji na wafanya biashara na ndicho anakifa fanya Mama
Una tatizo la maono na uelewa. Tangu lini rais akawa na uwezo wa kubadili sera ikulu? Anweza kutoa matamko na mchakato ukaanza. Hiyo inahitaji kutembelewa ikulu?
 
Hebu tuwekee ushahidi mmoja wa hizo enzi zenu mkiwa mnaweka ushahidi, ili nijifunze namna ya kuweka ushahidi kama nyinyi enzi zenu.
Unataka mifano ya darasa la tatu, boss! Hiyo sina! Ila usitumie maneno yasiyopimika. Wengi....bhla! bhla!
 
Wakuu tujiepushe na mtego wa ukabila katika kujenga hoja zetu, siamini Kila anayepinga Ni kabila fulani au anayeunga hoja Ni kabila fulani .
Kwa kiwango kikubwa taifa letu limevuka kwenye ukabila, huwezi kuhukumu kabila zima kwa ajili ya mtu mmoja la sivyo na wewe utakuwa mkabila vile vile.
Kila mtu ana utashi wake katika kutoa hoja Wala hatumwi na kabila lake
Tumpinge kwa hoja au tumuunge mkono kwa hoja
 
Ukiulizwa matatizo gani hata huyajui, ile unaona alikuwa na matatizo, Yapi???? Taja ni yapi?
Hicho siyo kiwanda cha kwanza nchini. Wapo akina Twiga Cement inayomilikiwa na makampuni makubwa kuliko hata Dangote amabaye ni mtu binafsi tu!
Dangote cement walikua na matizo madereva wao waligoma Na RC alishindwa kusuluhisha!!
 
Wasaidizi wake waliweza kuyatatua lni, na umejuaje kwamba matatizo ya Dangote hayawezi kutatuliwa na wasaidizi wake. Ni nani anajitoa ufahamu hapa?

Alitakiwa aje mashambani siku ile alipomaliza kumweka kaburini Magufuli, that's how urgent it was, and remains so, mpaka kesho kutwa.
Matatizo ya kugoma kwa madereva wa Dangote yalidumu Kwa muda mrefu hata kusababisha uhaba wa hiyo bidhaa Na bei yake kupanda nchi nzima!! Hence the urgency to solve the impasse by the President’s intervention. The whole economy was being affected!
 
Matatizo ya kugoma kwa madereva wa Dangote yalidumu Kwa muda mrefu hata kusababisha uhaba wa hiyo bidhaa Na bei yake kupanda nchi nzima!! Hence the urgency to solve the impasse by the President’s intervention. The whole economy was being affected!
So, this was the reason behind their meeting recently, was it! And Dangote came out smiling, promising to bring in more investors whose workers will be marginalized!

Was he reassured by the president that there will be no work stoppage in future, no matter what?

What will happen if our farmers took the same approach in order for their problems be heard by the head of state?

Will this be her way of solving problems in future in other sectors of the economy?
 
Enzi za Mzee Ruksa,Ikulu ilikuwa pango la walanguzi! Sijui kwa Mama ikoje.
 
Ule mgomo wa wafanyakazi wa Dangote labda anautafutia ufumbuzi.
Hivi Dangote ndio Obasanjo undercover?
 
Watanzania wanaamini wafanya biashara ndo watawapeleka uchumi wa kati wa juu ila hawajui mfanyabiashara siku zote anaangalia faida tu si kitu kingine
Yes na hiyo faida ndo inagenerate pesa za kusolve problems ili tufike huo uchumi wa juu
 
Tatizo dangote ni mweusi mwenzetu ndio maana maneno yamekuwa mengi angekuwa mhindi au mzungu wala msingepiga hizi kelele za kujifanya mna uchungu sana na nchi.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Bahati mbaya hunijui na assumptions zako zinabaki kuwa irrelevant na hasa ukianza kuingiza mambo ya racial and colour. That is so low for me to respond to.
 
Back
Top Bottom