Kwanini wafanyabiashara wanakwepa kusajili stoo zao? Taarifa zinasema wamejaza mali za magendo baada ya kuziingiza nchini isivyo halali

Mbona serikali inawaacha mafisadi wanaokwapua mabilioni ya pesa kila mwaka?
 
Jamani mwisho Wa Hawa watunga será na Serikali Yao na Spika wao ni Vema ikawa 2025 .
Hawa watu wameshindwa kusimamia mapato ya nchi. Wanakopa Kila Siku pesa zinaishia mifukoni Mwa Mafisadi
Kuna watu huko bandarini na TRA wanashirikiana na Wahindi kuiibia Serikali Kila sekunde ya pesa zinazoingia kwenye mfuko mkuu. Wanatumia wataalam Wa IT kutoka nje . Nchi ya Tazamia tu maisha Bora inaibiwa sana.
Haiwezekani nchi yenye Wananchi mil. 61 isiweze kujiendesha kupitia Kodi. Hapana ni uwongo Mkubwa unaosimamiwa na Mafisadi kuibia Nchi hili. Nchi hii Ina watumishi Wachache sana ukilinganisha na ukubwa wake na rasilimali zake na wingi Wa watu.
Hii Kila MTU analipa Kodi Kwa Kila bidha anayoinunua iwe ni kumnunulia mtoto wake au vinginevyo. Nchi hii watu wake wengi Wana ajira Binafsi au ya kuajiriwa. Ukienda huko mikoani na vijijini ukaona mageti ya ushuru usiku na mchana kutwa nchi Nzima utashangaa pesa zinakwenda Wapi!
Watu wanaiibia sana Serikali iliyojaa watawala waovu wanaowaogopa Wazungu kuliko MUNGU.
Jiulize Stendi za Mabasi nchi Nzima Kwa Siku wanakusanya Sh. Ngapi . Pesa ya kuokota tu kutoka Kwa wamiliki wa Mabasi Kwa kile kinachoitwa ushuru Wa Halmashauri lakini kiukweli ni pesa za kuwanufaisha walioshika zabuni na pesa kadogo sana Ndio zinaingia Halmashauri.

Watanzania wamelala fofofo hasa vijana wasomi . Halmashauri Badala ya kuajiri Vijana wasomi wakusanye ushuru wao Wanatumia wazabunia ambao ni watu wao wanaoshirikiana kupoteza mapato ya Serikali kupitia ushuru.
Usiku kucha kuna mabilioni ya pesa zinatolewa na wafanyabiashara kupitia mageti ya ushuru lakini zaidi ya asilimia 75 zinaishia mifukoni Mwa watu.

Hiví Kwa Mfano Stendi ya Mabasi kama Chalinze inahitaji Teknolojia Gani kujua KUWA Kwa Siku inaingiza Sh. Ngapi.! Yaani idadi ya magari Kwa Siku inajulikana halafu MTU anaeugusu makusanyo yaingie mifukoni Mwa mzabuni halafu kidogo kiende SERIKALINI. Mzabuni mwenye wafanyakazi wasio na NSSF Wala Bima ya Afya Wala hawalipi Kodi kwenye mishahara . Lakini tuna watu waliotunga SHERIA za ajabu Kwa manufaa Yao ya Kila mbunge kushirikiana na madiwani na Mkurugenzi kuhujumu mapato ya nchi. Wanaoumizwa ni wafanyabiashara Kwa manufaa ya majizi . Mipaka 61 ya uhuru Bado nchi unategemea misaada na kuwaacha watawala kujilimbikizia Mali za Wizi .
Hakuna muujiza zaidi ya kuwatoa wahuni madarakani.

Lakini wakati huo huo Kuna MTU mmoja Ana Miliki Malori mia nane na anabeba madini usiku kucha na Hana ushuru Barabarani Kila wilaya kama MTU aliyebeba mahindi au matikiti ambao linahesabiwa moja moja na Kila moja litolewe pesa .

Kuna MTU anaagiza Malori mia tatu Kwa pamoja lakini anapitisha bandarini kijanja kijanja lakini maskini akiagiza kiaIST analipa makodi na maushuru na matozo zaidi ya 70 % ya Bei aliyonunulia.
Kwa haraka haraka Lori mia tatu kuingizwa bandarini Kama zinalipiwa Kodi kama wanavyolipa wananchi wanyonge wanaoagiza Bajaji basi Hapo pangekua kuna mabilion ya pesa zinaishia SERIKALINI? Lakini Hapo ni rushwa na pesa zinatoroshwa na kuhamishwa huku nchi ikiwa inabaki kuendeshwa Kwa Mikopo.

Kuna MAHALI fedha za umma zinavuja sana.

Bahati Mbaya sana viongozi Wa upinzani nao wameshajionyesha mapema KUWA kumbe wanajali maslahi Yao na Sio umma Ndio Maana walipopewa stahiki zao za kisheria kabisa wamekaa kimya kama vile wamepewa hisani.
CCM irudi kwenye misingi yake ya kupambana na rushwa na ubadhirifu Wa Mali za wanyonge.
 
Kwa maelezo yako mazuri, neno
GSM halikupaswa kukosekana.
Lakin pia serkali na Tra wafungue mfumo wa uwepo wahasibu na tax consultants kwa wafanyabiashara wa ngaz zote kwa premium rafiki. Inapanua ajira pia.
Ni kama tunavyopigania utambuz wa paralegals kusaidia raia ngaz za chini.
Mf Uganda katika biashara ya magari walishinikiza uwepo wa dalali na commission yake kimfumo na kisheria.
Hapa kuna tatizo na changamoto.
Tatizo: sheria za kodi hasa asilimia au double taxation.
Changamoto: watendaji kama maafisa na task force kutumia mbinu za kibabe au nginjanginja na kwa nia ovu ya rushwa.
Bottomline: sheria zetu ni za kufirisiana si rafiki.
 
Daaaa!!wafrika tuna shida sanaa!!yaani umeona hilo la ukwepaji kodi halikuhusu?!!kama mwananchi wa kawaida
Nadhani malalamiko yao umeyasikiliza vizuri..
Issue siyo kulipa Kodi ni taratibu wanazotimia kukusanya/kupata hizo kodi...

Kulipa si wanalipa miaka yote...Tena kwa Wafanyabiashara wa Kariakoo siyo Issue..
 
Kodi za tz ukitekeleza kwa asilimia Mia moja unafunga duka
 
Umeongea ukweli mtupu. Na hatufungui maduka sasa , potelea mbali, paka kama huyo mtoa mada aje yeye afungue biashara yake halafu tuone
 
Umenena yote kitu kimoja tu kama ulivyosema wateja kukamatwa waache mara moja ila hili la store nadhani lina mantiki kubwa labda ni njia ya kufuatilia hili kwa maana kwa ushirikiano ili isiwe linaleta kukimbizana. Nimewahi kwenda kununua bidhaa sehemu la alifungua simu tu nakuangalia kama iko kwenye stock yao mbona hakuna shida na mambo ya kodi ni rahisi kuwasilisha report stock ni hii ni tupate utaratibu lakini lazima tukubali kuna ujanja mwingi kwenye hizi store sana tu.
 
Sasa kwani nani kasema kinachofanyika ni kinyume cha sheria? Tunachosema ni kwamba hizo sheria kandamizi zibadilishwe
 
Sasa kwani nani kasema kinachofanyika ni kinyume cha sheria? Tunachosema ni kwamba hizo sheria kandamizi zibadilishwe
Sheria kama hiyo yetu ya tax administration; Kenya yao wanaita ‘tax procedure act’


Mambo hayo hayo yaliyopo kwetu na kwao yapo.



Na kwenyewe unatakiwa utunze record kwa miaka 5 kama Tanzania (huo ndio muda ambao nchi nyingi tax authorities hurudi nyuma kwenye uchunguzi).

It must be said hadi wafanye uchunguzi wakurudi nyuma kwa miaka 5 ni kwa sababu wamebaini ubadhirifu mkubwa ambao unawapa mashaka ata miaka ya nyuma ulikuwa ulipi sahihi.

Sasa wao TRA wana abuse aspect ya hiyo dhana kwa kuwasumbua watu unnecessary, kutaka kuona record za nyuma wakijisikia tu; huo ni unyanyasaji na sio dhumuni lake.



Ndio hayo tunayozungumza mambo ya kutaka kufika mpaka store ata Kenya yapo.




Power to search and seize; mambo tunayo lalamikia TRA kuingilia bank na kutaka kupewa bank statement na Kenya yapo.

Hizo sheria zetu hazina shida kabisa zinafanana duniani, issue ni uelewa walipa kodi. Otherwise ukitimiza wajibu wako afisa wa TRA ni fala tu ambae awezi kukuzingua kabisa, mipaka yake ipo kisheria awezi toka nje ya hapo.
 

Hatuwezi kuishi kwa mazoea, Kenya walipofunga Lockdown Corona ulitaka na sisi tuwaige?
 
Utaratibu wa Uganda na sheria yao 👇




Na kwenyewe hayo hayo weka record kwa miaka 5



Mamlaka ya mapato inataka access ya information including physical assets (maana yake storage).



Uwezo wa kuomba details zako za bank.

Nikienda nchi za ulaya sheria zao zitakuwa na mambo hayo hayo; this is why you learn those principle in taxation modules and financial accounting; uwezi kwanza ata kuandaa financial statement yako bila ya hizo info.

Mfanyabiashara anaeshangaa ni clueless kabisa kwenye maswala ya uhasibu.
 
Hatuwezi kuishi kwa mazoea, kisa Uganda wameamua kuwa masikini na sisi tukubali kuemdelea na umasikini? Dawa hii hapo chini. Jibu hiyo hapo chini kama una hata akili mbili kichwani, maana umekuwa kama kasuku tu.

 
Mkuu vitabu tumecopy na kupaste kwenye advanced country kwa mazingira yetu Bado serikali na vyombo vyake inahotaji kuilea sekta binafsi.Mtu kauza shamba lake la miti hapo Njombe anaamua kufungua biashara hajui chochote juu ya hizo stori za vitabu.Ni jukumu la TRA kuwalea kidogo kidogo.Lakini kwa kuwa tunao vijana wanapenda maisha maxuri fasta.Akifika pale ni kuchapa offence na kumwita huyu mgeni wa biashara mezani.Anapewa option ya kutoa mlungura wa 1M au kulipa 4M serikalini.Unadhani Kuna mjinga ataopt 4M?
 
Kwenye hili serikali msikubali. Asiyetaka afunge duka lake. Wafanyabiashara wengi Ni majizi yanakwepa Kodi.
Huo ni mtazamo wako na ni mtazamo hatari.Wangekua wezi bidhaa ungepataje?
 
Mayor Quimby Mkuu wewe ni corporate attorney?
Wala just basic accountancy knowledge in taxation (ata watu wa finance baadhi ya vyuo wanafundishwa tax) lazima ujue madhara ya kukwepa kodi, what evidence you need to keep, nini kitafanyika jamaa wakiweka kambi na kuchunguza kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wa mfanyabiashara pia ata ukijifanyia auditing wewe mwenyewe kuona kama mali zako aziibiwi kishamba utapita njia hiyo hiyo ya TRA. Ata kutengeneza trial balance na financial statement utatumia info hizo hizo.

Ni basic accountancy knowledge. Ndio maana ata kwenye hili sakata baada ya kumsikiliza waziri ni kuona kuna mchezo wa kukwepa kodi particularly kwa watu wanaoleta na kuhifadhi hiyo mizigo in bulk kwa wafanyabiashara wa kariakoo na ndio walio nyuma ya huo mgomo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…