Kwanini wafanyabiashara wanakwepa kusajili stoo zao? Taarifa zinasema wamejaza mali za magendo baada ya kuziingiza nchini isivyo halali

bossi ukiambiwa ukatoe ushahidi utaweza?!, we unafanya biashara gani mkuu?!, kama unasubiri notification ya bank mwisho wa wezi huwezi elewa kero na karaha. wanazopitia. itoshe kusema kuwa mazingira ya kodi yanatakiwa kuwa rafiki kwa mlipaji.
Kwani mizigo inaingia na meli au Manuari!? Kama ni meli si bandari ndio mzigo inapokelewa!? Sasa huu uzushi unautoa wapi!?
 
Nadhani malalamiko yao umeyasikiliza vizuri..
Issue siyo kulipa Kodi ni taratibu wanazotimia kukusanya/kupata hizo kodi...

Kulipa si wanalipa miaka yote...Tena kwa Wafanyabiashara wa Kariakoo siyo Issue..
Kwani wao ulipaji wa kodi ni tofauti na wafanyabiashara wengine?inshu sio utaratibu hawataki kutumia EFD,kwani wengi hawapendi kuandika thamani halisi ya mauzo,na ndio maana kariakoo kuna watumishi wa TRA wao ni kufuatilia wateja,wanaokuwa wamenunua bidhaa,na unakuta mtu ana tv ya thamani ya laki 6,ila risiti aliyonayo imeandikwa laki 2!
Na usajiri wa store ndio umewavuluga mnooo!!
 
Ukweli ni kwamba kuna tatizo, fuatilia rapid open interview aliyoifanya Mkuu mpya mteule wa Mkoa alipokuwa akiongea na sampuli ya wafanyabiashara.
 
Hospital za nje ukienda kutibiwa wanakutibu lakini wanenda mbali kuangalia nini imeleta hali hiyo ili watibu kule pia sasa badala ya ku deal na matokeo kwanini wasiende na kuangalia inapitaje kwenye mfumo wote huo bila kulipa kodi, je wana bypass system, je kuna bandari bubu, je kuna airport bubu, je mipaka haiko salama kuna maswali mengi sana na kwanini wafanya biashara wanafanya wanayofanya je wanahisi wanaonewa kodi kubwa hazilipiki ni lazima jambo hili liangaliwe katika package ya kukuza uchumi kwa miaka mingi haya mambo hayawezi kuamuliwa kwenye kikao kimoja tu leo, ni lazima tuje na package ya kuchochea ukuaji wa uchumi na kufanya Tz kuwa kitovu cha biashara EA na haya yanawezekana.
 
Wabongo hasa wachaga wanapenda mtelezo

USSR

Sent using Jamii Forums mobile
Dah! Unaonesha ulivyojaa chuki dhidi ya kabila ulilolionesha hapo juu.
Najiuliza hivi ni kweli hususani ulipoandika hasa wachaga?. Kwa nini umewachukulia kama case study?.Tafsiri yangu juu ya mstari uliouandika ni kwamba wabongo wengi wanapenda njia rahisi lakini Wachaga wao wanapenda zaidi. This is more than a fallacy of hasty generalizations.
..................................................................................................
 
Kwanin hawako faithful unadhan the only reason ni roho ya kutaka kingi ?

Sio mfanyabiashara niliesimama ila nipo kweny huo ulimwengu nahakika 90% wapo tayar kulipa kodi shida ni hio serikali.

Kaka unaongelea inshu ya kuclaim,em niambie kuhusu input na output taxes na jinsi ya kuclaim labda sijui.
 
Tuna Utaratibu mbovu sana wa ulipaji Kodi nchini infact ukifuatiia hata ukadiriaji wa kodi unaofanywa na watu wa TRA kwenye maduka matatu tu yaliyopo hata mtaani unapoishi utabaini magumashi.
Makadirio magumashi, ulipaji magumashi..
 
Jamaa una akili wewe. Ningekua kwenye mamlaka za uteuzi ungeongoza kitengo. Kuna vijamaa vimekariri madesa vinaona wafanyabiashara hawana akiliiii
 
Reactions: Tsh
.Jamaa una akili wewe. Ningekua kwenye mamlaka za uteuzi ungeongoza kitengo. Kuna vijamaa vimekariri madesa vinaona wafanyabiashara hawana akiliiii
😀 😀 shukran sana mkuu kwa hilo.
 
Hii ni sababu ya msingi
 
Mmekalia ofisi ma mishahara makubwa siku za kustaaf zikifika mtaani mnapashindwa.Mnabakia kufuga kuku.Acheni viburi tengenezeni mazingira mazuri ya Biashara hata nyinyi yatakuja kuwasadia
 
Nataman nikutukane pumbavu zako. Wew unadhan watu hawapendi kulipa kodi?

Unadhan watu wanapenda kuingiza mizigo kimagendo?
Kwani kuingiza mizigo ya magendo inalazimishwa? Watu wanataka utajiri wa harakaharaka. Siamimi kama wafanyabiashara pamoja na malalamiko yao yooote wao hawana sehemu ya kulaumiwa.
 
Nilitamani sana TRA, TPA, POLISI nao wapewe platform wajibu tuhuma zao publically ili ku balance story. Siamini kama Wafanyabiashara ni wasafi kivile, ila mtu ana upande wake wa pili wa shillingi
 
wana vitu vingi vya magendo hupitisha baharini na kuna vitu kama vipodozi vilivyopigwa marufuku wao wanazo stoo
 
Yaani nipewe makadirio ya stoo na y dukani?
 
Kwani kuingiza mizigo ya magendo inalazimishwa? Watu wanataka utajiri wa harakaharaka. Siamimi kama wafanyabiashara pamoja na malalamiko yao yooote wao hawana sehemu ya kulaumiwa.
Kaka hizi biashara kama kamishna wa TRA na wasaidizi wake wakiazimia kila bidhaa ilipe kodi watu watalipa bila shida. Mim naingiza bidhaa × ila kodi nayolipa hailingani na mtu mwingine alieingiza alike products ,unafikir margin yetu itakua sawa. Unafikir next time nkitak kuingiza mzigo nini ntafanya?

Mfano naingiza IST kodi nayotakiwa kulipa ni 3M fine nalipa yote.Mwingne anaingiza IST lakini kodi analipa kimagumashi unafikir huko sokoni nan atauza hio IST haraka
 
Walipe kodi, hutaki kulipa Kodi funga biashara basiiiii...
 
Sawa Nchemba. Tatizo hata kodi zikilipwa Mnaishia kuzipiga.. Makodi makubwa af yanaishia kusikojulikana.
 
Hivi haya yote yanafanyika ulinzi na usalama unakuwa umelala.Na kwanini ukuwai kituo cha usalama cha karibu waende kukamata hayo magendo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…