Kwanini wagonjwa wa Kisukari hukatwa miguu na si mikono au kiungo kingine?

 
Kwa comments nilizopitia hapa kisukari ni hatari sana kwa kweli!
 
UMETISHA. kuongeza, hata kidole cha mkono pia hukatwa kwenye ncha ya nerve ndio kunawahi kuharibika. Mwili ni mfumo hivyo sehemu moja ikiumia mwilimzima huko hatarini.
 
je kuna dalili za mbali kwa mtu asiye na ugonjwa anaweza zimonitor?
 

Kwa kuongezea ni kwamba mfumo mzima wa kinga wa mwili pia huathiriwa kuweza kupambana na magonjwa hasa vidonda. Ukiacha mabadiliko yanayotokea kwenye eneo husika. Mfano: ukipata kidonda, mwitikio wa mwili kupambana huwa hafifu na hivyo basi maambukizi kuweza kusafiri toka sehemu moja kwenda nyingine kwa kufuata msuli/compartment kirahisi.

Hii hupelekea mtu kuwa anaona kidonda kiko sehemu moja kumbe athari yake imeshasafiri umbali mrefu kufuata msuri au bando zima la misuli.

Ila kwa ujumla kila kiungo mwilini kinaathiriwa na sukari kuanzia ukucha wa mguu mpaka nywele kichwani endapo hautazingatia namna ya kuishi vyema kwa dawa na ushauri wa wataalamu.
 
Nianze kwa kusema kwamba Kila kundi la chakula Lina kazi take mwilini.. sugar ama carbohydrate no kuupa mwili nguvu baada ya kuwa imeshameng'enywa mwilini.. Sasa mtu mwenye kisukari mwili wake unajua hauna uwezo wa kutumia sukari kama chanzo cha nishati hivyo wingi wa sukari utaongezeka tu kwenye damu, na ikishaaongezeka inaanza kuziba mirija ya damu hivyo supply ya damu ikianza kupungua kwenye seli za mwili zinaanza kufa kama mdau alivyosema Hapo juu....

Pia mtu mwenye kisukari hua hayuko vizuri kwenye mechi hii pia kwa sababu ya mwili unakua hauna nguvu kwa sababu sugar n chanzo kizuri cha nguvu kwa kua hakitumiki mtu huyu mwili wake unakua zaifu kidgo.


Ndio maana mtu mwenye kisukari hashauriwi kula wanga maana hauna matumizi kwake.

Mwisho tujari afya zetu kwa marndeleo yetu, nchi na dunia kwa ujumla
Kwa nini yapandishe sukari wakati kwa mtu asiye na sukari ni mazuri mkuu ?

Naomba nipate faida kuna mechanism gani inatokea ukila matunda yenye sukari kwa mgongwa wa diabete ?
 
Kwa nini yapandishe sukari wakati kwa mtu asiye na sukari ni mazuri mkuu ?

Naomba nipate faida kuna mechanism gani inatokea ukila matunda yenye sukari kwa mgongwa wa diabete ?

Ili kuelewa haya ni vyema kuelewa kisukari ni nini hasa?(nitatoa maelezo saidifu kwa kifupi yasiyo rasmi ili tuweze kuelewa).

Kisukari ni pale ambapo seli za mwili hushindwa kuitumia vyema sukari iliyopelekwa mwilini/kwenye damu ili kutengeneza nguvu. Hii hutokana na sukari kutokuingia kwenye seli ambayo ni tanuru ya kuunguza sukari ili kutoa nguvu. Hivyo, sukari hubaki ikiwa inaelea kwa wingi kwenye damu.

Kuelea kwa wingi kwa sukari ndio huleta madhara yote ya sukari.

Msingi mkuu ni kutokufanya vyema kazi kwa insulini ambayo ni ufunguo wa njia ya sukari kuingia kwenye seli. Hivyo, hili linaweza kusababishwa na kiasi kidogo cha insulin, insulini mbovu au tatizo la kufuri/mlango wa njia ya sukari kuingia kwenye seli.

Kuna sababu nyingi zinazohusishwa na kusababisha kisukari kimsingi:
1: Kurithi
2: Maambukizi kwenye kongosho/tatizo la kongosho
3: Wakati mwingine sababu kutojulikana
4: Na tatizo la kufuri/receptor kama ilivyoelezwa hapo juu.
5: Nk....

Hivyo basi, chakula chochote chenye asili ya kuleta sukari mwilini huitajika kupelekwa kwa kiasi kidogokidogo ili kutokufurika sukari mwilini. Hii hufanyika kwa kutambua uhitaji wa mwili wa muhusika kwa kujua aina ya kazi anayofanya na kiasi cha ukubwa wa mwili wake. Hapa madaktari bingwa wa ugonjwa wa sukari, wale wa magonjwa ya ndani/physicians na dietician husaidia sana katika hili.

Cha muhimu ni kujua kuwa mgonjwa wa kisukari ataendelea kuhitaji makundi yote ya vyakula kwaajili ya mwili wake. Uzingatiaji wa KIASI CHA CHAKULA na matumizi sahihi ya dawa na masharti yake ya mwenendo wa kimaisha ni muhimu sana.
 
NAONA WATU WANAANDIKA KONGOSHO INAFELI!
Note
kongosho ikifeli unakufa ndani ya saa 48 haijalishi nini, hivyo kongosho sio inafeli bali 2 husababishwa na inflamation either kwenye mfereji unapitisha insulin au kwenye utumbo mdogo or both. Hivyo kiasi kidogo kinaweza kupita na inflamation lazima inaanzia kwenye damu.
 
Niulize tu sasa kwa wale wanaopata ulabu- ni basi wasipate ulabu kabisa katika maisha yao yote au kuna aina ya ulabu utawafaa? Au kuna aina ya ulabu hauna sukari? Au hata glasi ya red wine basi? Yaani kazi kweli kweli!

Shukrani nyingi Mkuu!
Kula vyombo mzee maisha ndio haya haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…