Kwanini wahandisi wazuri sana duniani (Magari, Mitambo) wanapatikana nchini Ujerumani? Siri yao ni ipi hasa?

Wajerumani wachawi tu, we hushangai mpaka leo chemli na pasi ya mjerumani haijapatikana na watu bado wanaitafuta mpaka kesho. (masihara)

Germany's prowess in engineering is indisputable πŸ™ŒπŸ™Œ
 
Sio Israel tena mlamu!
Nami nilitaka niseme hivyo hivyo.Naona wameiweka akiba wataijaza baadae.
Ukisoma physics ndio utajua wajerumani ni akina nani.
Hawa wazungu ndio wanaamini kuwa ndio binadamu bora tangu kuumbwa kwa dunia,ukiwachunguza unaweza kuwaamini.Walipigwa vita ww2 na kushindwa,wakajipanga wakarudi na kuwa taifa bora kiuchumi na kiteknolojia ulaya.
Luna mahala nilisoma ktk physics kuwa wao somo la quantum physics walilipa kipaumbele wakawekeza facility na sasa matunda yanaonekana.
 
duuuh ina maana watu wengi walikuwa wanakimbilia kwenye kazi za mikono (ufundi)?
Wamewekeza ktk kujenga akili sio kazi za mikono.Babu zetu walijua sana kazi za mikono,walisuka kila aina ya ususi lakini walisahau kuwekeza ktk ubongo.
wajerumani wamewekeza ktk kuujenga ubongo.
Sidi waafrika tunawekeza ktk music and sports.Watu wanatumia muda mwingi ktk ngoma,muziki Mpira hawana muda na teknolojia.Sisi tunakuza vipaji vya muziki na Mpira sio sayansi na teknolojia.Tumeamua kuchagua entertainment.
 
Unajua hawa jamaa babu zao ndio waliogundua aina zote mbili za engine (petrol na dezeli).Kwa wale waliopitia"Thermodynamics" mtakuwa mnakumbuka "Otto cycle" na "Diesel cycle", Hawa mababu Nikolaus Otto na Rudolf Diesel walikuwa Wajerumani hivyo vizazi vilivyo kuja baada ya hapo vimeendelea kuboresha hiyo teknolojia toka wakati huo (karne ya 19) ndio maana magari na mitambo yao ina ubora wa hali ya juu
 
Kwa nini hao maengineers wa bongo wasiumize kichwa kuwe na standby ili chanzo kimoja kikiungua kingine kiwake?Bado tunarudi kulekule kwamba engineers wa bongo wana uwezo mdogo.
 

C and p From Quora
 

Maneno chungu nzima, wewe fani yako ni hipi,labda tuanzie hapo.
 


Nani kawambieni Quantum physics unahusika katika uundaji wa magari?
 
Gauss Markov ni nyoko aisee.....pia kuna Gottfried Liebniz.

Kama ulivyosema Ujerumani ina historia ndefu sana ya sayansi. Maendeleo makubwa sana ya kiteknolojia yanatokana na maendeleo ya sayansi ambayo kwa Wajerumani yameanza karne nyingi sana zamani.
 
Kwa nini viwe vichache?tuanzie hapo kwanza
Mkuu, huwezi tu ukaamua kujenga HydroPower Station Buguruni kwa Kimbengere; lazima upate eneo linalokidhi kuwa na kituo kama hicho; hayo maeneo ndio mtihani sasa kuyapata. Ndio maana Stiegler's Gorge zinajengwa huko kwenye maeneo sahihi, yanayokidhi mahitaji yote ya kuwa na kituo kama hicho.
 
Kwa hiyo unataka kusema Tanzania ina uhaba wa maeneo?Kama mapori yamejaa tele,mito imejaa tele,mabwawa yako tele.
Nini kinakosekana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…