Inferiority complex ndio inakusumbua hapa, watu wanazungumza nini, wewe umekazania ku-derail mada just to get even, kwani hatuwajui hulka zenu za kukwamisha maendeleo ya Mikoa ambayo ilikuwa mbali kielimu, kimaendeleo kabla na baada ya uhuru mpaka mid 1970s - badala ya mikoa iliyokuwa nyuma kimaendeleo na elimu kwenda kujifunza mbinu zinazo tumiwa na Mikoa iliyo fanikiwa nyinyi mkabuni mbinu za kukwamisha Mikoa endelevu mnapo pewa madaraka Serikalini.
Nani ambae hajui kwamba mikakati hii ya siri ya kudidimiza kimakusudi baadhi ya Mikoa hapa Tanzania inatekelezwa mpaka leo, mkavunja vyama vyetu vya Ushirika bila sababu yoyote ya maana, bila aibu wanavunja vyama vya ushirika vilivyo anzishwa kwenye miaka ya 1930s, mkataifisha mali zake pamoja na fedha zilizokuwa benki, fedha hizo hazijarudishwa mpaka leo, fedha hizo ndizo zilikuwa zinatumika kujenga shule, kulipa ada za watoto wa wakulima nchini mpaka Ulaya, kujenga viwanda, Mahoteli, Mashamba ya kisasa nk.
Mnajifanya kusahau ukatiri huo wa kushangaza, badala yake mnaleta ngojera zenu eti "Mikoa ya kanda ya ziwa ndio hiko nyuma sana kimaendeleo,elimu na umaskini!"