Siku tqjiri wa kanisa alipoudhuria ibada za katikati ya wiki, akaudhuria na mkesha wa maombi makali japo masaa matatu mchungaji alipagawa. Akawa anamtambulisha mara kumikumi.
Hii inaonekana matajiri wa kikristo hawategemewi kuwa siriasi na ibada kihivyo. Ndio maana hata mimi nikashangaa kuona mchungaji anashangaa ingawa hashangai kupokea sadaka zake.
Bila kujali ipi dini ya kweli, niwe mkweli matajiri wengi wa kiislam wanapenda ibada sana. Kuna wengine huko saudia wanaishi misikitini tu huku mambo yanaenda. Wetu wa kikristo wako shalo kiroho, wanakuja wamechelewa na kuwahi kuondoka. Wengine hawaji kabisa wanasubiri kuombwa kichango tu japo wengu hutoa sio bahiri.
Sababu ni nini?
Siwasimangi watumishi wa Mungu mbona mabilionea wa kibibilia walikuwa watu wa ibada kupitiliza hadi ibirisi anawaonea wivu?
Mfano: Ibrahim, Isaka, Yakobo, Ayubu, Suleiman, Daudi, Yusuph wa Armathaya, etc
Hawa jamaa wasaidiwe aisee. Wanatakiwa kuwa mfano mzuri kiroho kwa waumini masikini ambao ndio rundo makanisani.
Ni hayo tu
Mtumishi
Matunduizi.
Hoja yako nimeipata vizuri mtu aliye tajili au mtu mwenye pesa zake
Neno ibada ni nzuri ulilolitumia
Sipo hapa kuchambua na kukupa tafsili ya neno ibada lakini kifupi tu ni makanisa machache sana ya kikisto yanafanya ibada
Mengi yanafanya mafundisho na sio ibada
Na ndio maana utaona taratibu nyingi zinaanza
Nyimbo
Kwaya
Sadaka
Matangazo ni mengi hata kuliko mafundisho
Then mafundisho
Vikao mbalimbali nk
Ukiangia mambo yote hao huita ibada lakini sio kweli
Nachelea kusema makanisa mengi kama ilivyo kuwa matendo ya mitume ni jumiia ya waamini ukusanyika pamoja kujifunza ile imani yao
So kama ungetaka kuwa sahihi ungesema kwa nini matajili wa kikristo hawahdhuriii makusanyiko ya katikayi ya wiki na sio kutumia neno ibada
Matendo ya Mitume 2:41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.
Matendo ya Mitume 2:42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.
Nimalizie tu nikusii tafuta kufahamu neno ibada
Kwa ujmla nasikitika kuona kuona tunaudhuria kanisani lakini ibada haifanyiki
Walau kwa kiasi kidogo wakatoliki wanafanya ibada
Je ukienda kwa mwambosi utasema pale kuna ibada??
Bila kutaja wanamwabudu nani waisalamu wanafanya ibada,