Loading failed
JF-Expert Member
- Sep 14, 2023
- 2,603
- 7,501
- Thread starter
-
- #61
Mkuu moyo uko wapi mpaka iwe tofauti..? ukiwa ndani ya moyo fukara na nje ya mwili wewe ni fukara pia maana moyo upo ndani ya mwili na ndivyo ilivyo imani.. huwezi ukawa fukara moyoni alafu ukafanya matendo ya kimwili katika utajiri.Ufukara wa moyo ni katika imani, na ni tofauti na ufukara wa mwili.
Napia ili uweze kuwa mtu mwema unatakiwa uwe kiroho na siyo kuwa na moyo wa kifukara..Imani hii inamjenga mkatoloki kuwa tayari kupokea hali yoyote katika imani, kutokuwa m-binafsi na kuwa tayari kumshukuru Mungu katika kila jambo na kila hali. Usipokuwa na moyo thabiti wa ufukara, ukitetereka kidogo hata katika biashara au kazi, unaweza kumkufuru Mungu.
Hapo msamiati 'Heri' ulitumika vibayaBiblia ni falsafa ngumu:
Rejea swali lako, utasemaje kuhusu Yesu kuwaambia watu,
Mt 5:3-12
Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika. Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.
Je, Mungu anataka tuwe wenye huzuni? Mbona andiko jingine linasema, "furahini katika Bwana"?
Katika falsafa ya kiimani ufukara au umaskini unaozungumziwa ni ule wa Roho, siyo mali. Na ufukara wa Roho, ni ile hali ya kujiona wakati wote umepungukiwa, na hivyo kuishi kwa kumtegemea Mungu. Utajiri wa Roho humaanisha kuwa umejitosheleza kila kitu, na hivyo Mungu hana nafasi katika maisha yako.
Sasa kuhusu hiyo michango iliyokithiri hayo ni mambo ya kibinadamu zaidi. Sadaka ni unatoa chochote kulingana na uwezo wako, so ni jukumu lako wewe kuamua kama uwaridhishe bonadamu au umridhishe Mungu. Akili kichwani mwako.Kunatofauti ya ufukara , unyenyekevu na huruma..
Utatimizaje matendo ya huruma kwa muhitaji ilihali wewe ni fukara.. na kama moyo wa ufukara ni wa huruma kama wao wanavyo maanisha kwanini basi viongozi na makasisi wa kikatolik wasiwe na huruma kwa waumini wao na wawatake watoe kiduchu kadiri ya mapato yao , pia wasifute harambee na michango lukuki..
Yesu alizaliwa ukoo wa kifalme! Chumba alichozaliwa yesu walipachagua kwa kuwa palikuwa mahali pa utulivu. Kumbuka wakati huo kilikuwa kipindi cha mwisho wa mwaka wakati wa sensa ya watu na makazi kati ya mwezi 9-11 na kila mtu alikuwa anaenda kuhesabiwa hivyo nyumba hiyo ya mbari ya daudi ilijaa wageni mama mariam angepata wapi utulivu ili aweze kujifungua ?. Sisi wakatoliki hatuamishi mtu yeyote kuhusu masuala ya dini, bali yeye mwenyewe inabidi aamini kwa moyo wake mkunjufu,
. Ingawa nyinyi waislam suala la kuaminisha mtu dini ndo mmeweka kipaumbele zaidi na kufikia hatua ya kutukana matusi dini za upande wa pili.
Yesu alizaliwa katika mazingira duni huko Bethlehemu, akionyesha unyenyekevu na ufukara( hakuwa na kitu bali kilichopatikana walikula kwa pamoja) , jambo ambalo Wakristo wanaalikwa kuliiga. Ndiyo maana katika sala hii, waumini tunaomba "moyo wa ufukara," roho ya unyenyekevu, ukarimu, na kutokufanya mali kuwa kipaumbele cha maisha..
Haimaanishi hivyo Muombe Mungu akupe akili ya kulitafakar na kulijua neno laMunguNdugu..
Ufukara tunajua ni laana na hakuna mtu anayetaka wala kutamani kuwafukara, Mungu mwenyewe alisema atatubariki na utajiri unatoka kwake na tukimuomba atatupatia na kutujazilishia vya kutosha.
Pia Yesu alisema ukiomba jambo lolote kwa jina lake atalifanya hali kadhalika tukaambiwa sadaka yako ilipo ndipo na moyo wako utakapo kua.
Sasa unapo wasikia na kuwaona wakatoliki wakisali rozari .
KWENYE MATENDO YA FURAHA,. utaona wanamuomba Mungu awajalie moyo wa ufukara ambao ni moyo wa kimasikini kupita kiasi huku wakisahau kwamba Yesu akisema mtu awazavyo moyoni mwake ndivyo alivyo na pia alituambia tuulinde moyo maana ndipo zitokapo chemchem za uzima ,
1: Kwanini hawa wakatoliki basi wanaomba Mungu awajalie Moyo wa ufukara kwanini hawautaki utajiri kutoka kwa Mungu ila wao wanataka wawe mafukara?
2: Je, wana sali na kuamini kitu wasicho kijua?
3: Je, huko Roma- vatican ni kwamba wameweka maombi ya mtego kwa waumini wa kikatoliki ili kuwafunga maisha yao wabakie kua mafukara huku wao wakijitajirisha na kuneemeka na sadaka zao pamoja na harambee za kila kukicha?
Naomba kuwasilisha