Kwanini wakatoliki wanamuomba Mungu awajalie moyo wa ufukara na siyo ya utajiri kama vile Mungu alivyosema atatubariki?

Kwanini wakatoliki wanamuomba Mungu awajalie moyo wa ufukara na siyo ya utajiri kama vile Mungu alivyosema atatubariki?

Ufukara wa moyo ni katika imani, na ni tofauti na ufukara wa mwili.
Mkuu moyo uko wapi mpaka iwe tofauti..? ukiwa ndani ya moyo fukara na nje ya mwili wewe ni fukara pia maana moyo upo ndani ya mwili na ndivyo ilivyo imani.. huwezi ukawa fukara moyoni alafu ukafanya matendo ya kimwili katika utajiri.

Mfano. Moyo ukihuzunika hata nje ya mwili inajifunua kwamba una hudhuni na wakati mwingine kuugua na kulia kwa uchungu.. na hivyo hivyo ukiwa fukara moyoni hata kimwili utakua fukara na ndiyo itakua umejifunga kiimani
 
Imani hii inamjenga mkatoloki kuwa tayari kupokea hali yoyote katika imani, kutokuwa m-binafsi na kuwa tayari kumshukuru Mungu katika kila jambo na kila hali. Usipokuwa na moyo thabiti wa ufukara, ukitetereka kidogo hata katika biashara au kazi, unaweza kumkufuru Mungu.
Napia ili uweze kuwa mtu mwema unatakiwa uwe kiroho na siyo kuwa na moyo wa kifukara..

rejea matendo ya rohoni.

Wagalatia 5:22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,

23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.

Sasa kwanini wao wakatoliki wautake ufukara na siyo kutaka matendo mema kama ilivyowazi kwenye maandiko kama kweli wanachomaanisha ni kizuri. Kwanini wasiende direct wanazunguka mbuyu..
 
Biblia ni falsafa ngumu:

Rejea swali lako, utasemaje kuhusu Yesu kuwaambia watu,
Mt 5:3-12
Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika. Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.

Je, Mungu anataka tuwe wenye huzuni? Mbona andiko jingine linasema, "furahini katika Bwana"?

Katika falsafa ya kiimani ufukara au umaskini unaozungumziwa ni ule wa Roho, siyo mali. Na ufukara wa Roho, ni ile hali ya kujiona wakati wote umepungukiwa, na hivyo kuishi kwa kumtegemea Mungu. Utajiri wa Roho humaanisha kuwa umejitosheleza kila kitu, na hivyo Mungu hana nafasi katika maisha yako.
Hapo msamiati 'Heri' ulitumika vibaya
Kiuhalisia badala ya Heri ilitakiwa iwe
'Wamebarikiwa'
Ikiwa Maana Wamebarikiwa maskini,webarikiwa wanyonge
Ukiwa maskini ukibarikiwa ina maana wewe ni tajiri,
Ukiwa mnyonge utapewa moyo wa ushujaa,

Na Sio Heri,Heri,Heri ambayo inasound ki lay man ukisoma. Hata Bible ya kingereza
Inasema Blessed all........
 
Nipo mkoa unaosifika Kwa kuwa na makanisa mengi uchwara ya kikristo.
Ninachokiona na kukishuhudia kwa hawa watu. Aisee! nitadumu mno kwny ukatoliki nikishindwa kabisa bora niwe mpagani.PERIOD.
 
Moyo wa ufukara...
1. Kuona mali si kitu mbeke ya uzima wa milele.

2. Kugawa ulichobarikiwa kwa maskini.

3. Majivuno kupitia mali si kitu, maana tulivikuta na tutaviacha.

4. Mali za dunia hazina msaada kwenye ukimbozi wa roho yako.
 
Kunatofauti ya ufukara , unyenyekevu na huruma..
Utatimizaje matendo ya huruma kwa muhitaji ilihali wewe ni fukara.. na kama moyo wa ufukara ni wa huruma kama wao wanavyo maanisha kwanini basi viongozi na makasisi wa kikatolik wasiwe na huruma kwa waumini wao na wawatake watoe kiduchu kadiri ya mapato yao , pia wasifute harambee na michango lukuki..
Sasa kuhusu hiyo michango iliyokithiri hayo ni mambo ya kibinadamu zaidi. Sadaka ni unatoa chochote kulingana na uwezo wako, so ni jukumu lako wewe kuamua kama uwaridhishe bonadamu au umridhishe Mungu. Akili kichwani mwako.
 
. Sisi wakatoliki hatuamishi mtu yeyote kuhusu masuala ya dini, bali yeye mwenyewe inabidi aamini kwa moyo wake mkunjufu,

. Ingawa nyinyi waislam suala la kuaminisha mtu dini ndo mmeweka kipaumbele zaidi na kufikia hatua ya kutukana matusi dini za upande wa pili.


Yesu alizaliwa katika mazingira duni huko Bethlehemu, akionyesha unyenyekevu na ufukara( hakuwa na kitu bali kilichopatikana walikula kwa pamoja) , jambo ambalo Wakristo wanaalikwa kuliiga. Ndiyo maana katika sala hii, waumini tunaomba "moyo wa ufukara," roho ya unyenyekevu, ukarimu, na kutokufanya mali kuwa kipaumbele cha maisha..
Yesu alizaliwa ukoo wa kifalme! Chumba alichozaliwa yesu walipachagua kwa kuwa palikuwa mahali pa utulivu. Kumbuka wakati huo kilikuwa kipindi cha mwisho wa mwaka wakati wa sensa ya watu na makazi kati ya mwezi 9-11 na kila mtu alikuwa anaenda kuhesabiwa hivyo nyumba hiyo ya mbari ya daudi ilijaa wageni mama mariam angepata wapi utulivu ili aweze kujifungua ?
 
Ndugu..

Ufukara tunajua ni laana na hakuna mtu anayetaka wala kutamani kuwafukara, Mungu mwenyewe alisema atatubariki na utajiri unatoka kwake na tukimuomba atatupatia na kutujazilishia vya kutosha.

Pia Yesu alisema ukiomba jambo lolote kwa jina lake atalifanya hali kadhalika tukaambiwa sadaka yako ilipo ndipo na moyo wako utakapo kua.

Sasa unapo wasikia na kuwaona wakatoliki wakisali rozari .

KWENYE MATENDO YA FURAHA,. utaona wanamuomba Mungu awajalie moyo wa ufukara ambao ni moyo wa kimasikini kupita kiasi huku wakisahau kwamba Yesu akisema mtu awazavyo moyoni mwake ndivyo alivyo na pia alituambia tuulinde moyo maana ndipo zitokapo chemchem za uzima ,

1: Kwanini hawa wakatoliki basi wanaomba Mungu awajalie Moyo wa ufukara kwanini hawautaki utajiri kutoka kwa Mungu ila wao wanataka wawe mafukara?

2: Je, wana sali na kuamini kitu wasicho kijua?

3: Je, huko Roma- vatican ni kwamba wameweka maombi ya mtego kwa waumini wa kikatoliki ili kuwafunga maisha yao wabakie kua mafukara huku wao wakijitajirisha na kuneemeka na sadaka zao pamoja na harambee za kila kukicha?


Naomba kuwasilisha
Haimaanishi hivyo Muombe Mungu akupe akili ya kulitafakar na kulijua neno laMungu
( Moyo wa ufukara, moyo usio na tamaa, moyo wa kuwapenda wengine, moyo usio na ubinafsi, moyo wa kujitolea kwa ajili ya wengne)
 
Back
Top Bottom