Kwanini wakazi wengi wa Dar es Salaaam mna roho mbaya?

Nikija bara nimeenda kwetu nitafikia kwetu. Nikienda mkoa mwngne nitafikia lodge au hotelini.
Mimi uwa sipendi kufikia kwa watu ili niwe huru na nisiingilie mfumo wao wa maisha.
Hujui maisha we dogo.
 
Unaniita mimi dogo huenda ninakuzidi. By the way mimi msafiri nasafiri mikoani kila mara lakini uwa ninajitahidi nisiwe mzigo kwa watu niwapo kwenye harakati zangu.
Dogo kujumuika na ndugu na jamaa ndio unakuwa mzigo?
 
Dogo kujumuika na ndugu na jamaa ndio unakuwa mzigo?
Ukiingia kwenye familia ya watu kuna namna flan unawaaharibia mfumo wao wa maisha yao waliouzoea.

Huwezi kuelewa kwakuwa wewe bado ni dogo umezoea kufikia kwa shemeji yako au unaishi kwa shemeji yako.

Jitahidi ufikie kwa watu pale inapokuwa na ulazima, kama unaweza kuafford fikia hotelini au lodge.

Hii haimaanishi watu wasitembeleane wala kulala kwa watu, lakini isiwe ni tabia yako unatoka unatoka eti kisa unamfahamu flani yuko dar basi ushapanga tu kuwa utafikia kwake tena wafanya kumpa taarifa tu.
 
Hii kasumba ya kusema mnaharibiana mifumo ya maisha ndio roho mbaya yenyewe.

Jifunze kuwa maisha huwa yanabadilika, leo utapokea wageni na wewe ipo siku utakuwa mgeni. Ubonadamu ni kuwa na hali ya kujumuika na watu.

Watoto wapuuzi kama wewe mmekulia kwa wazazi hamjawahi kupata tabu ndio maana mna roho mbaya.
 
Nikija bara nimeenda kwetu nitafikia kwetu. Nikienda mkoa mwngne nitafikia lodge au hotelini.
Mimi uwa sipendi kufikia kwa watu ili niwe huru na nisiingilie mfumo wao wa maisha.
Sasa hapo kwenu ndugu wakija Dar huwataki, utathaminiwa vipi ?
 
Unaishi kwa shemeji gharama za maisha utazijua wapi wewe?

Njoo kwangu ukiwa na ulazima, siyo unakuja kupumzika eti.

Ndiyo unaharibu utaratibu wa familiaz lazima watu wajitune kuendana na mgeni.
 
Watu wa daslam wengi wanalala stoo na wachache ndo wanakula maisha Sasa ukienda kwa jamaa anae lala stoo lazma akununie tu
 
Sasa ukienda ulaya si ndo utatukana .maana kule ni mara 1000 ya dar..yaan hawatak ujinga wa ndugu kabisaaa...maisha ni budget..ukiona unanuniwa ujue kwenda kwako pale ni kero.

Bak kwenu mkoan ndugu
 
Ndio maana watu wengine kukaribia kwa ndugu bila sababu za msingi hawezi kufika hata kusalimia tu, kwa sababu watu waliotangulia mahali fulani wanakua na tabia za ajabu.
 
SIO ROHO MBAYA MKUU TATIZO MAISHA YA DAR NI MAGUMU MNO NDO INASABABISHA HALI HIYO
Kuna siku nilishangaa mvua ilikuwa inaonyesha ikakatika , Ile natoka Tu bonge la mvua mbele yangu kuna mgahawa nikaenda kujikinga mvua akaja mwenye mgahawa akaniuliza unahitaji chai na nini? Nikajibu samahani nimejificha mvua alichonijibu nilijitosa kwenye mvua. Kweli watu WA Dar Wana roho za ajabu.
 
Hawana utu.
 
Dar ni uwanja wa mapambano,pambana ule,zubaa ulale njaa.Watu lundo rasilimali chache(Maji machache,Mamba wengi).Ukitaka fair life rudi Bush!
 
Yaani watu wanaendekeza dhiki Hadi aibu, mfano angeniacha nitulie ningeona aibu hata ningemuungisha Maji ya Mia tano. Watu kama hao ndio maana hawafanikiwi.
Sio lazima kumuungisha. Kujikinga mvua unampunguzia nini?
 
Sasa ukienda ulaya si ndo utatukana .maana kule ni mara 1000 ya dar..yaan hawatak ujinga wa ndugu kabisaaa...maisha ni budget..ukiona unanuniwa ujue kwenda kwako pale ni kero.

Bak kwenu mkoan ndugu
Ulaya watu wanagawa vyakula bure daily. Ukarimu wa watu nchi zilizoendelea ndio ulinganishe na Dar?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…