Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Katika kitabu cha Kutoka 3:5, Mungu alimwambia Musa: "Usikaribie hapa, vua viatu vyako miguuni, maana mahali unaposimama ni ardhi takatifu." Kwanini basi Wakristo wa leo hawatii agizo hilo la kuvua viatu wanapoingia kanisani, ilhali Musa aliambiwa hivyo?
Sababu ya Musa kuambiwa avue viatu imetajwa wazi na Mungu mwenyewe:
“Maana mahali unaposimama ni ardhi takatifu.” Ardhi ile ilikuwa takatifu kwa sababu ya uwepo wa Mungu. Nyakati hizo viatu vilionekana kuwa na uchafu kwa sababu ya kutembea juu ya mavumbi, tope, na uchafu wa kila aina. Kwa hiyo, kuvua viatu kilikuwa ni kitendo cha kujitakasa.
Labda unajiuliza tena: kanisani si kuna uwepo wa Mungu? Kama ndivyo kwanini Wakristo hawavui viatu? Ni kweli, kanisani kuna uwepo wa Mungu. Lakini katika Agano Jipya Mungu hakai mahali maalum tu. Anakaa ndani ya kila aaminiye. Yesu anasema katika Ufunuo 3:20
"Tazama, nasimama mlangoni nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nitakula naye, naye atakula pamoja nami."
Ili Yesu (ambaye ni Mungu) aingie na kukaa ndani yetu, ni lazima kwanza tuyavue matendo ya giza (Warumi 13:12). Kwa hiyo katika Agano Jipya, utakatifu unaonyeshwa siyo kwa kuvua viatu, bali kwa kuvua tabia za dhambi na kuvaa utakatifu wa moyo.
Ndiyo sababu tunaambiwa “Heri wenye moyo safi, maana hao watamwona Mungu.” (Mathayo 5:8)
Katika 1 Kor 6:19 tunajifunza pia kwamba hekalu la Mungu sio la matofali na mawe, miili yetu ndiyo hekalu la Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ni nafsi ya tatu ya Mungu. Ili aingie ndani yetu ni lazima mioyo yetu iwe safi. Hii ina maana kwamba utakatifu sasa unahusiana zaidi na moyo wa mtu, sio ardhi anayokanyaga au viatu anavyovaa.
Kwa maneno mengine, katika Agano Jipya, kuvua viatu hakumfanyi mtu kuwa mtakatifu. Mtu ambaye hajavua matendo ya dhambi, akivua viatu kabla ya kuingia kanisani, bado tu saa ya kutoka kanisani atavaa viatu na kuitumia miguu yake kwenda kuiba, kufanya uzinzi, kulewa, na kufanya dhambi nyingine.