Chukwu emeka
JF-Expert Member
- Jan 12, 2018
- 25,299
- 40,929
Biblia ina lugha ambayo kama unasoma kama msoma comments wa JEIFU huwezi kutoboa
Makafiri si mmeahidiwa mtaimba na kukata viuno? Naona imekuuma sana😄😄😄. Chuki imekujaa mpaka unaona wivu kobazi kupata bikra 72. Soma mathew 19 29 kuna wanaopata wake 100 ila hawajasema kama bikra.Kupenda na kupewa ni vitu viwil tofauti. Mimi nauliza kama mtu siyo kobazi akifa hapewi ile zawwdi yenu ya mabikra 72?
Nimekuelewa na hilo uliotoa ndio jibu sahihiHakuna sehemu hata moja ambayo Yesu katika Ibada zake aliwahi kuvua Viatu, kama angekuwa anavua na kututaka sisi tuvue, tungevua, lakini maadam hakufanya hivyo, wala hakutuambia sisi tuvue, basi hatufungwi na sheria hiyo, Mtu yupo huru, akiwa na Viatu, ruksa kusali navyo, kama mtu hana viatu pia hazuiliwi kusali.
Maana dhambi haikai kwenye kiatu, bali dhambi inakaa kwa mwenye kuvaa viatu, kwa hivyo kuwa na kiatu hakikuondolei dhambi, wala kutokuwa na viatu, hakukuondolei dhambi ulizo nazo.
Kutoka 12:11
"Tena mtamla hivi; mtakuwa mmefungwa viuno vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni pasaka ya BWANA."
Muhubiri 5:1
"Jitunze mguu wako uendapo nyumbani kwa Mungu; Maana ni heri kukaribia ili usikie, Kuliko kutoa kafara ya wapumbavu; Ambao hawajui kuwa wafanya mabaya."
Yeremia 2:25
"Zuia mguu wako usikose kiatu, na koo yako isiwe na kiu; lakini wewe ulisema..."
Dhambi ni najisi au sio najisi?Unatakiwa kufuatilia neno "najisi" linamaanisha nini sio kila kitu kichafu ni najisi
Jasho sio najisi
Fangasi pia sio najisi
Kinyesi kilicho tumboni sio najisi
Na suala la mtu kutolewa uchafu unapozikwa ni ili azikwe bila mabaki ya chakula tumboni lakini si kwa kigezo cha najisi uchafu uliopo tumboni sio najisi
Huyo aliyeuliza hilo swali nina uhakika atakuwa hajsoma content. Kasoma kichwa cha habari kakimbilia kujibu swali. Hii ni changamoto kwa Watanzania wengi- uvivu wa kusoma..Swali lako linaonyesha kana kwamba hujaelewa mantiki ya kwa nini jina la Musa limetajwa katika mada hii.
Sijamtaja Musa kwa sababu tunamfuata au tunataka kuiga kila alichofanya. La hasha. Nimemtaja Musa kwa sababu kuna watu wanaojaribu kuhalalisha utaratibu wa kuvua viatu kanisani kwa kutumia mfano wa Musa. Kwa maneno mengine, wao wanasema: “Mbona Musa alivua viatu aliposimama kwenye ardhi takatifu? Basi hata sisi tuvue.”
Kwa hiyo, nimetoa mfano wa Musa kwa lengo la kubatilisha hoja hiyo, si kwa lengo la kumfanya Musa kuwa kielelezo cha Ukristo. Musa hakuwa Mkristo, na hakuna mahali katika Agano Jipya ambapo Wakristo waliagizwa kuvua viatu kama utaratibu wa ibada. Yesu hakufundisha hilo. Mitume pia hawakulisisitiza hilo. Hivyo basi: kama sababu pekee ya kuvua viatu ni kwamba “Musa alivua,” basi sababu hiyo haina mashiko. Umenipata?
1. Dhambi sio najisiDhambi ni najisi au sio najisi?
Au tuanze na najisi maana yake? Unajisi sio uchafu
Wapi uliwaona majini?Kwann waislam wanafuga majini?
Yaan unavua viatu lakini nyumbani una majini sasa hapo unamvulia mungu viatu au unayavulia majini
Aje na jibu lililonyookaKwani Musa alikuwa mkiristo
Kwani wakati wa mussa kulikuwa na kanisa? Au wakati wa yesu kulikuwa na kanisa?
Nimekuelewa na hilo uliotoa ndio jibu sahihi
Swali kwako, je Yesu alikuwa mkiristo?
Umepigilia msumari kabisa; ntafurahi na hicho kikombe cha Castle_Lite ukikibwaga chiniMaana dhambi haikai kwenye kiatu, bali dhambi inakaa kwa mwenye kuvaa viatu,
Sasa kama yesu hakuwa mkiristo na alikuwa anafundisha mafundisho ya Musa, na Musa alivua viatu alipoingia kwenye nyumba takatifuYesu hakuwa Mkristo.
Alikuwa Myahudi.
Kipind chake kulikuwa na Mila na destur za Kiyahud na Yesu alizifuata.
Kulikuwa na Sinagogi.
Yesu aliingia sinagogi.
Pia walikuwa na utamaduni wa kuchagua msimamizi wa Sinagogi.
Sinagogi walikuwa wanafundisha misingi ya Dini za mababu zao na kufuata torati ya Musa pamoja na kuambiana Hadithi ambazo tumeziona agano la kale.
Swali umelenga lijibiwe na mrengo upi?Katika kitabu cha Kutoka 3:5, Mungu alimwambia Musa: "Usikaribie hapa, vua viatu vyako miguuni, maana mahali unaposimama ni ardhi takatifu." Kwanini basi Wakristo wa leo hawatii agizo hilo la kuvua viatu wanapoingia kanisani, ilhali Musa aliambiwa hivyo?
Sababu ya Musa kuambiwa avue viatu imetajwa wazi na Mungu mwenyewe:
“Maana mahali unaposimama ni ardhi takatifu.” Ardhi ile ilikuwa takatifu kwa sababu ya uwepo wa Mungu. Nyakati hizo viatu vilionekana kuwa na uchafu kwa sababu ya kutembea juu ya mavumbi, tope, na uchafu wa kila aina. Kwa hiyo, kuvua viatu kilikuwa ni kitendo cha kujitakasa.
Labda unajiuliza tena: kanisani si kuna uwepo wa Mungu? Kama ndivyo kwanini Wakristo hawavui viatu? Ni kweli, kanisani kuna uwepo wa Mungu. Lakini katika Agano Jipya Mungu hakai mahali maalum tu. Anakaa ndani ya kila aaminiye. Yesu anasema katika Ufunuo 3:20
"Tazama, nasimama mlangoni nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nitakula naye, naye atakula pamoja nami."
Ili Yesu (ambaye ni Mungu) aingie na kukaa ndani yetu, ni lazima kwanza tuyavue matendo ya giza (Warumi 13:12). Kwa hiyo katika Agano Jipya, utakatifu unaonyeshwa siyo kwa kuvua viatu, bali kwa kuvua tabia za dhambi na kuvaa utakatifu wa moyo.
Ndiyo sababu tunaambiwa “Heri wenye moyo safi, maana hao watamwona Mungu.” (Mathayo 5:8)
Katika 1 Kor 6:19 tunajifunza pia kwamba hekalu la Mungu sio la matofali na mawe, miili yetu ndiyo hekalu la Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ni nafsi ya tatu ya Mungu. Ili aingie ndani yetu ni lazima mioyo yetu iwe safi. Hii ina maana kwamba utakatifu sasa unahusiana zaidi na moyo wa mtu, sio ardhi anayokanyaga au viatu anavyovaa.
Kwa maneno mengine, katika Agano Jipya, kuvua viatu hakumfanyi mtu kuwa mtakatifu. Mtu ambaye hajavua matendo ya dhambi, akivua viatu kabla ya kuingia kanisani, bado tu saa ya kutoka kanisani atavaa viatu na kuitumia miguu yake kwenda kuiba, kufanya uzinzi, kulewa, na kufanya dhambi nyingine.
Musa alikuwa Myahudi. Kanisa la Kristu lilianza kwa Mitume wa KristuKwanini Wakristo hawavui viatu wakiingia Kanisani? Mbona Musa aliambiwa avue viatu?
Sasa kama yesu hakuwa mkiristo na alikuwa anafundisha mafundisho ya Musa, na Musa alivua viatu alipoingia kwenye nyumba takatifu
Swali: kwanini asiwafundishe wafuasi wake hakiwafundisha kuvua viatu wakiingia katika ibada, je unaamini hakiwafundisha?
Wakati musa anaambiwa avue viatu alikua anaingia wapi? Halafu tusaidie tafsiri ya kanisa, ni mtu au jengo?Katika kitabu cha Kutoka 3:5, Mungu alimwambia Musa: "Usikaribie hapa, vua viatu vyako miguuni, maana mahali unaposimama ni ardhi takatifu." Kwanini basi Wakristo wa leo hawatii agizo hilo la kuvua viatu wanapoingia kanisani, ilhali Musa aliambiwa hivyo?
Sababu ya Musa kuambiwa avue viatu imetajwa wazi na Mungu mwenyewe:
“Maana mahali unaposimama ni ardhi takatifu.” Ardhi ile ilikuwa takatifu kwa sababu ya uwepo wa Mungu. Nyakati hizo viatu vilionekana kuwa na uchafu kwa sababu ya kutembea juu ya mavumbi, tope, na uchafu wa kila aina. Kwa hiyo, kuvua viatu kilikuwa ni kitendo cha kujitakasa.
Labda unajiuliza tena: kanisani si kuna uwepo wa Mungu? Kama ndivyo kwanini Wakristo hawavui viatu? Ni kweli, kanisani kuna uwepo wa Mungu. Lakini katika Agano Jipya Mungu hakai mahali maalum tu. Anakaa ndani ya kila aaminiye. Yesu anasema katika Ufunuo 3:20
"Tazama, nasimama mlangoni nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nitakula naye, naye atakula pamoja nami."
Ili Yesu (ambaye ni Mungu) aingie na kukaa ndani yetu, ni lazima kwanza tuyavue matendo ya giza (Warumi 13:12). Kwa hiyo katika Agano Jipya, utakatifu unaonyeshwa siyo kwa kuvua viatu, bali kwa kuvua tabia za dhambi na kuvaa utakatifu wa moyo.
Ndiyo sababu tunaambiwa “Heri wenye moyo safi, maana hao watamwona Mungu.” (Mathayo 5:8)
Katika 1 Kor 6:19 tunajifunza pia kwamba hekalu la Mungu sio la matofali na mawe, miili yetu ndiyo hekalu la Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ni nafsi ya tatu ya Mungu. Ili aingie ndani yetu ni lazima mioyo yetu iwe safi. Hii ina maana kwamba utakatifu sasa unahusiana zaidi na moyo wa mtu, sio ardhi anayokanyaga au viatu anavyovaa.
Kwa maneno mengine, katika Agano Jipya, kuvua viatu hakumfanyi mtu kuwa mtakatifu. Mtu ambaye hajavua matendo ya dhambi, akivua viatu kabla ya kuingia kanisani, bado tu saa ya kutoka kanisani atavaa viatu na kuitumia miguu yake kwenda kuiba, kufanya uzinzi, kulewa, na kufanya dhambi nyingine.
Anakwenda kupakatwa na kidume Ibrahimu,kama alivyopakatwa LazaroKobazi bhana. Hivi kama mtu siyo kobazi akifa hapati ile zawadi yenu ya mabikra 72?